Nitapata wapi mahindi maalumu kwa ajili ya kutengeneza pop corn (bisi)?

Kig

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
1,076
455
wadau naomba mnijulishe; Je kuna mahindi maalumu ya kutengezea bisi za biashara (yaani kuuza)?
Kama kuna mahindi maalumu yanapatikana wapi kwa bei gani?
 
Supermarket yoyote yapo, ulizia wahudumu tu, yanakua katika makopo
 
yapo mengi tu katika supermarkets, yamefungwa ktk packets au small boxes. Angalia Game mlimani city
 
wadau naomba mnijulishe; Je kuna mahindi maalumu ya kutengezea bisi za biashara (yaani kuuza)?
Kama kuna mahindi maalumu yanapatikana wapi kwa bei gani?

ni PM, nita ku-suply hata tons, am serious
 
Nawashukuru sana wadau kwa kunijibu thread yangu na kunipa majibu ya kile nilichokuwa nakihitaji.
 
MimI NIPO DAR. NITATEMBELEA SEHEMU ZOTE WADAU WAMESEMA NIONE BEI INAKAAJE

Nenda kwa Wahindi Shoppers Plaza, Shirji's na kwingineko. Imalaseko wamefilisika siku hizi, duka lao moja tuu City Centre, sababu ushindani umekuwa mgumu dhidi ya Wahindi. Kariakoo sanaa ya kutengeneza mahindi ya popcorn hawaijui.
 
Mkuu kig tafadhari nisaidie kama unajua bei ya mashine ya popcorn kibango bongo zinapatikana wapi? Tafadhari.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom