Nitapambana na mafisadi hadi kifo

Amejiunga katika kikundi cha MAFISADI. Hukumbuki zile bilioni ?

Kweli fedha zinabadili sana mitizamo ya watu..jamaa alikua mkali kwelikweli.
Ndio maana naona hawa wakosoaji wetu wasipewe vyeo kwani wanaweza kubadilika. Na pia imefika wakati wa kuwa na mawaziri nje ya wabunge.
 
Hapo umesema, kazi ya bunge ibaki kuwawajibisha mawaziri.
 
nakumbuka mama sitta alivyokuwa kwenye kile chama cha walimu alikuwa anaandaa maandamano na migomo kila siku kuhakikisha walimu wanakuwa na maslahi mazuri.
mungu si athumani JK akampa shavu katika wizara ya elimu na ndo akawa waziri, sasa walimu wakawa wakiandamana ye anawaambia tulieni kwanza matatizo yenu yanashughulikiwa msiandamane...so hata huyo mama kilango anapiga kelele tu ila akipewa uwaziri ataufyata tulii
 
Ni kweli kabisa tumeona wengi wanawasha moto bungeni ili wakumbukwe tu hamna kingine, mama sita alikuwa mkali kweli na migomo mingi imetokea wakati wa uongozi wake, lakini siku hizi katulia kama sio yeye aliyekuwa anahimiza migomo. Mzindakaya kaongwa mabilioni ya kuanzishia kiwanda chake cha kusindika nyama na yeye kakaa kimya, alifika wakati wa kutetea uozo wa EPA kuwa hakuna tatizo.

It can happen kwa mama Kilango, na yeye akapewa ulaji atakaa kimya. Mnakumbuka na Mh. majogo, the same story
 
Kweli fedha zinabadili sana mitizamo ya watu..jamaa alikua mkali kwelikweli.
Ndio maana naona hawa wakosoaji wetu wasipewe vyeo kwani wanaweza kubadilika. Na pia imefika wakati wa kuwa na mawaziri nje ya wabunge.

Wakuu,

Pamoja na kuikosoa serikali, binafsi ningetaka kuona wabunge wetu wanasimamia maendeleo kwenda wilaya zao.

Ni rahisi kuimba mafisadi kila siku kuliko kukaa na wananchi huko wilayani na kujaribu kutatua matatizo yao katika juhudi ya kujiletea maendeleo yao.

Naona kwasasa kila mtu amepeleka nguvu yote kwenye mafisadi na kusahau kabisa priorities zingine za taifa.

Hata ufisadi leo ukipotea kwa asilimia 100 bado Tanzania na Watanzania tutaendelea kuwa maskini. Ni muhimu mno kuweka kipaumbele pia kwenye uchumi na hasa unaowahusu watu wetu moja kwa moja.

Imekuwaje kilimo kinazidi kwenda chini huku mahitaji ya mazao kama ya chakula yanaongezeka?

Ningependa kuona watu kama akina mama Malecela wanatumia muda pia kuwasaidia wakulima, vijana na wafanyabiashara wadogowadogo kule jimboni kwao ili waweze kuongeza uzalishaji na hivyo kujiletea maendeleo.

Vita dhidi ya mafisadi sawa ni muhimu lakini sambamba na hivyo vita lazima tuelekeze nguvu kubwa kwenye uzalishaji hasa huko wilayani.
 
Niliona Majuzi Mama Kilango Alikuwepo Huko Same Katika Ufunguzi Wa Kiwanda Cha Tangawizi Na Aka Contribute Shilingi Milioni Tatu, That's Good, And It Means They Are Starting To Pay Attention Kwa Watu Wanaowawakilisha, Na Mb Mwakyembe Naye Hakosekani Sana Jimboni Kwake Kyela Katika Utatuzi Wa Matatizo Ya Anaowawakilisha That's Also Good, Keep It Up.
 
Mamaparoko,

Ni vizuri kama wanatoa misaada. Ila wasiwasi wangu mimi ni kwamba hiyo misaada haitufikishi popote sisi kama nchi na pia hata huko wilayani.

Ninachoongelea mimi ni kusaidia wananchi wetu ili waweze kushiriki moja kwa moja kwenye shughuli za uzalishaji na maendeleo.

Kama umeongelea kufungua hicho kiwanda ni jambo zuri, lakini itakuwa nzuri zaidi kama hao wabunge na viongozi wengine watasaidia kuwafanya hao wananchi washiriki kuzalisha hizo tangawizi kwa kutumia kilimo bora na matokeo yake kuweza kujiendeleza wenyewe.

Hii ya matajiri kutoka mjini na kwenda kutoa msaada na kuondoka nafikiri bado sio dawa ya umaskini wetu.

Hapa ndipo wengi wetu tuna matatizo makubwa, tunaona tukienda huko wilayani na kuwapa watu pesa za kula mara moja na kuondoka basi tumesaidia lakini huenda misaada tegemezi kama hiyo ndio inatufanya tuendelee kulemaa.

Japo misaada ni muhimu lakini mimi naona tungewekeza zaidi kwenye kuwawezesha watu wetu through kilimo bora, ufugaji bora, uwajibikaji wa wataalamu walioko wilayani kwenye maendeleo ya kila siku na mengineyo ingelikuwa ni msaada mkubwa zaidi.

Naamini mbunge anayewajibika hata kama hana pesa, anaweza kuwa na msaada mkubwa zaidi kwenye jimbo lake kuliko watu kama akina Nkono ambao wanamwaga mapesa na kuondoka.
 
Back
Top Bottom