Nitampataje mume mwenye vigezo hivi?

features zako ni zipi? maana hata mimi nimetafuta nimekosa. Nina features zote hizo ulizoziorodhesha.
 
All the best Suzy usichoke kufunga na kumuomba mungu akupe mme mwenye hizo sifa
Hakika yeye ni mwema ukiamini katika kweli hilo litatimia
 
Kweli kuna haja ya kuwa na Second ID kuombea wachumba, kutongozea na kuPM watu usiowajua. Maana nikichek muombaji ana siku 10 tu hapa JF. Sasa kama sio mdada mzoefu wa humu ndani ana hamu zake na noninooo nyeupe utajuaje?!!!
 
Haitaji mume huyo, unataka mwenye feature wewe feature unayo? Weupe au ufupi ndio nini kwenye ndoa. Watakumega sana halafu watakuacha kwenye mataa kwa sababu huangalii mambo ya msingi
 
Wapendwa nawasalimu!!

Ninatumai kila mtu ana sifa za ama mke au mume anayemtaka, rafiki zangu wa JF, napenda sana nipate mume mwenye vigezo hivyo hapo nilivyovitaja lakini kila siku imekua kinyume kabisa na matarajio yangu.

1. Awe Mkirsto
2. awe mweupe
3. awe na feature ya maisha, kwani fedha hutafutwa
4. awe mrefu wa wastani
5. kuanzia miaka 30 kuendelea

Dada yangu alishawahi kunitania kuwa eti niwatongoze wale ninaowapenda na nikitu ambacho siwezi hata kujaribu kufanya. Jamani nisaidieni au ndio niendelee kusubiri ubavu wangu kutoka kwa Mungu?

Naombeni mawazo yenu, pengine nafikiri hadithi za kujenga magorofa hewani.
Binti yangu Susy, usiwe na wasiwasi kwa maana hilo kama kweli ni hitaji lako, naomba nikupe dondoo kidogo:-
1.Peleka hitaji lako kwa Mungu Baba yeye anaheshimu na kupenda watu waoane kihalali.
2.Ingia gharama, kama unasema wewe ni Mkristo lazima ujitakase, uombe na kufunga, tenga muda hasa hata ikiwa ni baada ya saa za kazi.
3. Muone Mchungaji wa kiroho akupe maelezo zaidi, usende kichwa kichwa shetani atakuchomekea kanyabyoya na mtaishia pabaya. UBARIKIWE.
 
Wewe ndo una tatzo utaendelea tafuta mme mwe vigezo unavyotaka hadi Ukongoroke, Mme ni mme tu ili mradi mpendane kwa dhati!! Kwanza tutake radhi cie weusi na wafupi kwa kashfa zako.

Jamani binafsi nadhani hiyo sio kashifa, kwa sababu hata mimi napenda mwanaume mweusi kuliko mweupe. Hili nalo ni factor katk mahusiano kwa sababu nafsi yangu inamkubali mtu mweusi na mrefu kidogo kuliko mweupe mrefu, tena akiwa mweupe mfupi ndo kabisaaa sitaki hata kumtamani.
 
Susy nakushauri kitu kimoja vigezo 5 vyote ulivyotaja hapo unaweza kuambulia mwanaume mwenye vigezo 2 au 1 sasa kama utakuwa unahitaji mwanaume mwenye vigezo vyote usijidanganye unaweza kuishiwa kuchezewa bure halafu watu wakalala mbele be careful on what you are looking for kuna mambo ya msingi zaidi kuliko hivyo vigezo ulivyovitaja hapo.

Nafikiri unge-base zaidi kutafuta mwanaume ambaye utasaidiana naye kulea na familia na mwenye malengo hayo mengine ni muonekano wa mtu tu pia tabia ya mtu na vigezo ni vitu viwili tofauti unaweza ukapata mwanaume mwenye hivyo vigezo vyote lakini akakupa-frustrations mpaka ukajuta all in all muombe Mungu akupe mume mwema Mungu siku zote ukimuomba mkate hawezi kukupa jiwe so hauna budi kutanguliza maombi yako mbele za Mungu kwanza tena ikibidi hata kwa kufunga.

KILA LA HERI.

TF.
 
Hapa mtihani kama ndio muzee wa Maty katika kuPM ukaangalia picha unaweza kukuta unamtongoza upya mamsup! Nimejaribu kumPM nikashituka namPM Maty duh!!!:twitch:
 
:coffee::coffee::coffee::coffee:
 
Maneno yako swadakta mkuu huwezi amini nimejaribu kumsaidia kusachi kwenye google napata results kama zako tena baada ya kubadilbadili ila ukiweka kama anavyotaka yeye inajibu NO RESULTS FOUND:A S thumbs_down:
 
Jamani binafsi nadhani hiyo sio kashifa, kwa sababu hata mimi napenda mwanaume mweusi kuliko mweupe. Hili nalo ni factor katk mahusiano kwa sababu nafsi yangu inamkubali mtu mweusi na mrefu kidogo kuliko mweupe mrefu, tena akiwa mweupe mfupi ndo kabisaaa sitaki hata kumtamani.

Kwa nini huyu dada ameiga avatar yangu? huyu ana kashfa na ni nungayembe la mjini tu hili hana lolote, we dada badilisha hiyo avatar usinisababishie ban bwana?
 
Hapa nitaanzisha ID mbili kwa mpigo
Moja itakuwa ya kike ambayo avatar yake itakuwa matata kweli kweli. Hii ID najua itapata SENKS nyingi sana za kiume hapa JF, itazidi hata SENKS za CPU mwenyewe, itatumiwa sana PM na vibabu vya hapa JF na itakuwa maarufu sana ndani ya muda mfupi tu kuliko hata CPU

Ya pili itakuwa ya kiume. Hii itatumika kutongozea na kuPM hizi ID mpya za wadada wanajiofanya wanatafuta wachumba/waume ili hata kama huyo mdada alifungua ID mpya kugundua wanaume na vibabu vicheche hapa JF basi hadhi ya CPU inakuwa bado haijachafuka
 
Haitaji mume huyo, unataka mwenye feature wewe feature unayo? Weupe au ufupi ndio nini kwenye ndoa. Watakumega sana halafu watakuacha kwenye mataa kwa sababu huangalii mambo ya msingi

Jamani weupe, urefu na ufupi ni kitu cha muhimu kwenye ndoa pamoja na hivyo vingine vya utu wema,uchapa kazi, ucha Mungu nk nk!! Kwa sababu sio kila mtu nafsi yangu inamkubali, mi navutwa zaidi na mtu mrefu kidogo na namshiba huyo na kujisikia vizuri kutembea nae kuwa nae yani huyo ndo furaha na matanio yangu!! Mfano mi sipendi mtu mwenye ndevu nyingiii, yani zile ambazo hata ukinyoa leo kesho zimeshaota. Napenda mtu mwenye ndevu kidogo tu. Lakini kuna mwingine anampenda huyo mwenye madevu hata yakiwa kama yale ya kwene picha inayoitwa ya Osama!!
 
Maneno yako swadakta mkuu huwezi amini nimejaribu kumsaidia kusachi kwenye google napata results kama zako tena baada ya kubadilbadili ila ukiweka kama anavyotaka yeye inajibu NO RESULTS FOUND:A S thumbs_down:

kwani wewe huna vigezo hivyo nipate mkwe na uwe umemsaidia kijana mwenzio:coffee:
 
Kwa nini huyu dada ameiga avatar yangu? huyu ana kashfa na ni nungayembe la mjini tu hili hana lolote, we dada badilisha hiyo avatar usinisababishie ban bwana?

Maty pole unajua siioni avatar coz ya mobile, lakini Maty take it cool, nadhani kama ni mwelewa atabadilisha tu. Usiumize moyo wako kwa sababu hiyo sio picha yako halisi. Potezea halafu tuone ana/tapata faida gani kama ameamua kufanya hivo kwa kusudi lolote juu yako. Just be cool my love!!
 
Hapa mtihani kama ndio muzee wa Maty katika kuPM ukaangalia picha unaweza kukuta unamtongoza upya mamsup! Nimejaribu kumPM nikashituka namPM Maty duh!!!:twitch:

hahahaaaaaaa huyu dada ananitafutia ban uzalendo ushaanza kunishinda
 
Back
Top Bottom