nitamjuaje mwenye simu yenye namba za airtell?

ejom

Member
Jan 19, 2009
28
4
nimepigiwa simu na mtu namba zake ni za Airtel katika kuongea kaaza kunitukana sasa ninataka kujua huyu mtu ni nani nitumie njia gani kumpata
 
kama amejisajili utampata......nenda ofisi za airtel.......lakini kwa nini akutukane hivyo?....au inawezekana ni wrong number?
 
nimepigiwa simu na mtu namba zake ni za Airtel katika kuongea kaaza kunitukana sasa ninataka kujua huyu mtu ni nani nitumie njia gani kumpata

Sometimes mambo kama haya unayapotezea tu (kama mnavyosema vijana wa siku hizi)! Utafuatilia mangapi ndugu yangu dunia yenyewe hii? Au ndio mtindo wake siku nyingi? Kama ni mara nyingi, well, unasababu ya kufuatilia ili asiendelee, lakini kama ni mara moja, ahh! Achana nae (usije ukatumia energy na pesa zako kwa mambo ambayo hayatakupa manufaa yeyote) Unaweza kufuatilia ukakuta jamaa/bibie kakosea namba - na ikawa kesi kama tunazoambiwa za jamaa wanaouza ng'ombe washinde kesi ya kuku!!

Ndugu yangu mmoja husema hivi: "Yanakuwa matusi au kashfa kama tu:

  • Ni hadharani, au
  • Umekubali yawe matusi."
Someone else once said: "Nobody can make you inferior without your consent"
 
So simple ndugu yangu,
Sajili namba yako kwenye huduma ya AirTell PESA then jaribu kutuma hela kwenye hiyo namba automatic jina la huyo mtu litakuja.
Kwa kampuni yoyote ya simu siku hizi ni rahisi sana kujua namba ya mtu kwa njia hiyo.
 
mtumie msg fupi tu ili roho yako iridhike: ''acha ushamba wewee'',then mpotezee!usishushwe sukari na mtu ambaye he/she doesnt matter in ur life
 
Nitumie namba yake kwenye PM kuna jirani anafanya Airtel nitakutumia jina lake na anakoishi.
 
...............
...........
Someone else once said: "Nobody can make you inferior without your consent"

Huyu "Someone" ni Eleanor Roosevelt, alikuwa mke wa Rais wa zamani wa Marekani Franklin Delano Roosevelt. Rais huyu alipata kuongoza Marekani kwa vipindi vinne (si mfululizo nadhani) na aliongoza Marekani wakati wa Great Depression na Vita ya Pili ya Dunia. Aliridhia kuanzishwa kwa "Manhattan Project" kufuatia barua ya Dr. Albert Einstein juu ya uwezekano wa kuengeneza mabomu ya nyuklia. Yalitengenezwa mawili, moja la Plutonium jingine la Uranium 235, miji ya Hiroshima na Nagasaki ikawa wahanga. Aliyeruhusu kupigwa Japan ni Rais Harry Truman kwa Kuwa Roosevelt alikuwa amekwishafariki.

Thanks for the quotation.
 
Nitumie namba yake kwenye PM kuna jirani anafanya Airtel nitakutumia jina lake na anakoishi.

Kampuni hairuhusu kutoa taharifa za mteja...labda kama huyo jamaa ataamua kwenda polisi,kisha polisi wakaja kufuatilia taharifa za huyo mtu (kiaamidili zaidi)
 
Au umetembea na demu wake Kama ww mwanaume au umetembea na mume wake kama ww mwanamke. Hilo utalitatua mwenyewe
 
So simple ndugu yangu,
Sajili namba yako kwenye huduma ya AirTell PESA then jaribu kutuma hela kwenye hiyo namba automatic jina la huyo mtu litakuja.
Kwa kampuni yoyote ya simu siku hizi ni rahisi sana kujua namba ya mtu kwa njia hiyo.

Hiyo ni trial and error,kama huyo mtu ajasajili huduma ya airtel pesa hauwezi jua jina na unaweza mfaidisha kupata hela,nenda katoe malalamiko yako ofisi za airtel.
 
Hiyo ni trial and error,kama huyo mtu ajasajili huduma ya airtel pesa hauwezi jua jina na unaweza mfaidisha kupata hela,nenda katoe malalamiko yako ofisi za airtel.

nakubaliana na wewe kwamba kama wewe umesajiliwa na huduma za pesa afu unayemtafuta hajasajiliwa huwezi kulipata jina lake. Ila ktk upande wa kutuma pesa jaribu kuwa mjanja, yaani unapotuma pesa tuma pesa zaidi ya salio lako, huwa pesa hazitaenda na utapokea ujumbe kuwa salio lako halitoshi kutuma pesa. La sivyo ukituma pesa zilizochini ya salio lako lazima upoteze. Nawasilisha hoja wadau.
 
uliwezaje kuvumilia

akutukane? Mimi mtu kama

huyo nakata simu tu, ya nini

nikae kuumiza kichwa na

kichaa! Alah!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom