Nitakuwa StarTV Tuongee Asubuhi Kesho Tar 13/03/2012 - Mada ya Uzazi Salama ...Utepe Mweupe

HKigwangalla

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
717
971
Nimealikwa Star TV Tuongee Asubuhi kesho tar 13/03/2012 saa moja kasoro robo na Bw. Jacob Markus ambapo tutaongelea Utepe Mweupe (white ribbon) ... mambo ya Uzazi Salama, moja kati ya maeneo yangu ya interest (kuwatetea akinamama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano) na niliyoyafanyia kazi kwa muda mrefu zaidi wa maisha yangu ya kitaaluma na moja ya sababu za mimi kugombea Ubunge!
 
Kweli lisemwalo lipo......, ila nafikili ni too late maana mweshimiwa keshamaliza tatizo na jamaa hang'oki....
Kila la kheri na mada yako
 
Nimealikwa Star TV Tuongee Asubuhi kesho tar 13/03/2012 saa moja kasoro robo na Bw. Jacob Markus ambapo tutaongelea Utepe Mweupe (white ribbon) ... mambo ya Uzazi Salama, moja kati ya maeneo yangu ya interest (kuwatetea akinamama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano) na niliyoyafanyia kazi kwa muda mrefu zaidi wa maisha yangu ya kitaaluma na moja ya sababu za mimi kugombea Ubunge!

Jiandae na maswali kuhusiana na madai yaliyosababisha mgomo wa madaktari.
 
Je,nikweli Dr kigwangalla nimtetezi wa akina mama? mbona ulikuwa kimya wakati serikali Inayoongozwa na chama chako Ikikukabidhi shangingi {VX} nakupitisha mpango wa kupeleka BAJAJI kwenye vituo vya afya{zahanati} ili ziwabebe akina mama wajawazito? je,wewe unaweza kuluhusu mkeo akishikwa na uchungu atumie usafili huo kwa barabara za vijijini....au mliamua kupima uelewa wa akina mama wakitanzania?

TANZANIA YENYE NEEMA NI YETU SOTE.
 
nimealikwa star tv tuongee asubuhi kesho tar 13/03/2012 saa moja kasoro robo na bw. Jacob markus ambapo tutaongelea utepe mweupe (white ribbon) ... Mambo ya uzazi salama, moja kati ya maeneo yangu ya interest (kuwatetea akinamama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano) na niliyoyafanyia kazi kwa muda mrefu zaidi wa maisha yangu ya kitaaluma na moja ya sababu za mimi kugombea ubunge!

chonde chonde kaka mkubwa, tumeshapata taarifa kuwa mmeshaletewa muswada mtakao ujadili bunge lijalo kuhusiana na hayo makitu ya uzazi wa mpango, kwa niaba ya wana pro-life nakuomba uzungumzie yaliyomo ndani ya mpango wa mungu, na siyo mkajadili na kupitisha sheria ya utoaji mimba ambayo ipo chini ya kivuli cha mada yako, naomba mumuogope mwenyezi mungu na huo mchongo unaoletwa na watu weupe chini ya kivuli cha ''safe motherhood''
 
ukiongelea gari kwa wabunge, unamaanisha chombo cha kuwafikisha kwa wananchi majimboni na ni cha muhimu...hiyo ni gharama ya demokrasia tusiyoweza kuikwepa...
 
usisahau kugusia kiasi ambacho mnatenga kwa ajili ya akina mama na watoto na kiasi hicho kinatumikaje
wanawake wanakosa delivery kit wakati fedha zimetengwa
 
ukiongelea gari kwa wabunge, unamaanisha chombo cha kuwafikisha kwa wananchi majimboni na ni cha muhimu...hiyo ni gharama ya demokrasia tusiyoweza kuikwepa...

Mkuu swala la pikipiki bajaji kubeba wajawazito unalionaje? Maternal mortality bado ni issue, hospitali nyingi huduma duni ukizingatia hata hospitali ya mkoa kukosa theatre, mfano Mawenzi Hospital, hapo bado hatujawajali kina mama
 
Dokta lets be serious even for a second, VX kweli ndo garama ya democracy kama unavyotaka kuwaaminisha wanajamii!!!!!!! kama kweli eneo lako la kitaaluma ni akina mama na watoto tafaadhali usituletee habari za bajajikwani ni lazima ujue kuwa tunacho ongelea ni kizazi kijacho cha watanzania ambao ujaji wao unategemea usafiri wa bajaji, suluhisho la eneo lako lakitaaluma ni kuangalia rasilimali tulizo nazo na kuzitumia kutatua matatizo ya akina mama na watoto.Plz usije na takwimu za misaada ya wajomba toka ughaibuni.
 
Umeshakunywa maji ya bendera ya kijani huna la maana wewe!
sana sana utatetea sera za kipuuzi za chama ambacho kimechoka, hakina mawazo ya kuwasaidia watanzania wanyonge!
 
Jf moderator1,usishangae kwa wepesi wa majibu kwa maswali mazito kwa viongozi,ndo zao izo. Kwao kila kitu ni simple tu na hasa kama kinawahusu wananchi.

I wonder maana kwa hali halisi hilo lilikuwa sio jibu lake kabisa
V8 kwa bajaj na unasema eti hi halali yako kuwa nalo kwa sababu ya gharama za democracy
 
ukiongelea gari kwa wabunge, unamaanisha chombo cha kuwafikisha kwa wananchi majimboni na ni cha muhimu...hiyo ni gharama ya demokrasia tusiyoweza kuikwepa...

Dr.Kigangwala hebu angalia hoja ya msingi kabla ya kujibu. Hoja ya msingi sio mbunge kukosa usafiri,hapana. Tatizo ni kwamba kwanini nyinyi wabunge mnatumia magari ya kifahari huku zahanati za vijijini magari yao ya kubebea wagonjwa (ambulance) ni vibajaji? Na pia ukaulizwa kama mkeo ni mjamzito na anakwenda kujifungua utakubali kumpakia kwenye kibajaji? Nafikiri sasa utakuwa umeelewa,tunasubiri majibu yako Dr. Hamisi Kigangwala ambae kwa wasiofahamu wewe ndio ulikuwa Mwenyekiti wa kamati teule ya bunge ya kuchunguza sakata la JAIRO.
 
ukiongelea gari kwa wabunge, unamaanisha chombo cha kuwafikisha kwa wananchi majimboni na ni cha muhimu...hiyo ni gharama ya demokrasia tusiyoweza kuikwepa...

kama kweli wewe ni mtetezi wa mama zetu naomba uwe wa kwanza kuiomba serikali iuze mashangingi yenu yote.................................!kisha iwanunulie magari ya nafuu................................ili pesa ya hayo mashangingi ikasaidie kina mama zetu wajawazito.........................................UNAWEZA...................???
 
Mtampaswua kichwa mhishimiwa! mnampa maswwali magumu wakati uwezo wa kuyajibu hana...analojibu ndio jibu lake zito...ladba hawezi kufikiria zaidi ya hapo....hakuna mtu ndani ya ccm aliye na nia ya dhati ya kuwakomboa watz....kila m2 yukpo ktk kujitengenezea maisha! vivyo hivyo hata kwa HK
 
mkuu,umefunga mjadala
 
Back
Top Bottom