Nitakupenda daima

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Baby Hujambo

Nimekaa hapa mbele ya computer yangu usiku huu , nafikiria leo nikuandikie kwa lugha gani , ili uelewe ninachotaka kusema , mwanzo nilitaka kuandika kwa kiingereza lakini nikasema mhh inawezekana baadhi ya maneno matamu nikakosa bora niandika kwa lugha yetu takatifu Kiswahili

Baby ni jambo la furaha sana kupata nafasi hii nyingine kukaa mbele ya computer kukuandikia kitu Fulani , kuna watu saa hizi wanalia wameumizwa na wapenzi wao kwa njia moja au nyingine , kuna wengine saa hizi wanafikiria kesho itakuwaje kwa sababu wamewauzi wapenzi wao , kuna wengine wameshakata tamaa ya maisha kwa sababu walijitoa sana kwa wapenzi wao mwishowe walikosa vyote walivyokuwa wanafikiria hapo mwanzo

Pole kwa kuongelea mambo hayo hapo juu lakini ni kukumbusha tu wajibu wako katika kuhakikisha mapenzi yetu kati yangu na wewe yanadumu na kuendelea kukua siku hadi siku , kila siku unaposoma ujumbe wako ujue tu kwamba nimekufikiria kuliko jana kwahiyo nakupenda zaidi natamani uwe karibu yangu ili maneno ninayoandika nikuambie moja kwa moja , ili ujisikie maalumu zaidi .

Pamoja na hayo mimi hapa nilipo naendelea vizuri sana , namshukuru mungu toka asubuhi mpaka sasa hivi umefika wakati wa kupumzika hakujatokea tatizo lolote zaidi ya moyo wangu kusikitika kwanini sikuwahi kukujua toka mwanzo nilipoanza kuwa na akili timamu nimeanza kukujua tu ukubwani , kwanini haya mapenzi ya sasa hivi sikuyapata huko kwingine kote ndio nakuja kuyapata sasa hivi ukubwani natamani ingekuwa hivyo toka mtoto mpaka sasa na hata ninapoaga dunia .

Ahsante sana kwa mapenzi ya dhati unayonionyesha na kunipa kwa kweli naamini mimi ndio mwanaume bora kuliko wote duniani na tukiwa na familia basi ntakuwa baba bora kuliko wote duniani nikiwa na wewe , kwa jinsi tunavyoishi sasa hivi nina ndoto na malengo mazuri sana kuhusu wewe sijawahi kuwa na wasi wasi wowote mpaka sasa hivi .

Baby naomba uendelee kuwa mwaminifu mvumilivu na mwenye malengo katika maisha yetu sote wawili , mie pia naahidi kuwa mwaminifu mvumilivu na malengo katika maisha yetu sote .

Napenda kukuahidi kukupenda , kukujali na kuwa na wewe wakati wote wa maisha yangu toka uliponijua sintojutia kukupenda wala kuwaza lolote baya kuhusu wewe kama yalikwepo basi yafute anza maisha na mambo mapya katika maisha yetu sote wawili

Nakupenda sana , naomba niishie hapa niende kukumzika sasa hivi
 
OOh Shy, you are not really shy!!
 
kaaaaz kwerkwer.
icon10.gif
 
Love For Display Only!

Kwangu imekaa kingonjera zaidi!

Go into real marriage life and see what it really reflects my dear!

In the name of `uchumba`, or any nasty games currently ongoing, you have every reason to say all those words on earth!

Weka yeye ndani uone jinsi hii maneno itakuwa!
 
shy ingia uwanjani uone utamu wa ngoma hayo maneno sijui kama utayakumbuka ukishakuwa naye himayani,manake hali ya mahusiano kwa sasa ni kuomba nusura tu mungu akpe mke/mume bora lakini sio wa kujisifia kama haya ya kwako. POLE KAKA/DADA.
nawakilisha mtazamo tu.
 
Love For Display Only!

Kwangu imekaa kingonjera zaidi!

Go into real marriage life and see what it really reflects my dear!

In the name of `uchumba`, or any nasty games currently ongoing, you have every reason to say all those words on earth!

Weka yeye ndani uone jinsi hii maneno itakuwa!

KakaJimmy, elewa kuwa ndoa ni wewe na mkeo mtataka iwe mtakavyo!!! Mmoja akibadilisha utaratibu wa awali, basi fahamu na mwingine ni automatic. Amini kuna ndoa ambazo zimekuwa na maisha ya mapenzi, uaminifu hadi mwisho, hata kama kuna some misunderstandings but zinakuwa minimal and solved in time. Usikae na donge moyoni hata kama ni ndogo kama mbegu ya haradhani. I have more than 20 years of dedicated marriage with four children!!! (ninaposema more than 20, just imagine numbers 20 <Y<35!!!!)
 
BABY

Ni mchana umefika hapa mjini dar es salaam , mchana wa leo hakuna jua kabisa kuna mawingu kama vile mvua inataka kunyesha , niko zangu hapa hata bado sijala chochote , nakutafuta kwenye simu hupatikani , nimeingia online pia sikuoni hata nimesikiliza radio kusikia kama utanitumia salamu za mchana pia sijasikia chochote

Basi nikaamua bora nikuandikie japo maneno machache ukisoma upate furaha mimi pia nipate furaha pindi nitakaposikia umesoma ujumbe wangu , ukipata nafasi naomba unijibu mpenzi kwa sababu nakupenda sana siwezi kujielezea .

Mpenzi hivi unajua huwa najisikiaje ninapoanza kukuandikia chochote ? unaweza kuhisi ujue ninavyojisikia lakini kwa ufupi ninapoanza kukuandikia chochote tu huwa nahisi niko juu na ninachoandika kinaenda kwa malaika Fulani aliyembinguni ambaye ni wewe .

Baby kama wanaume wengine wote hawajawahi kukufananisha wewe na kitu Fulani kizuri kama malaika mimi sikufananishi mimi nakuita wewe malaika na nikiandika barua tu najua inaenda kwa malaika

Malaika wana mapenzi ya dhati malaika ni wazuri malaika wanapendeza , malaika ni zaidi ya mrembo malaika ni zaidi ya maelezo ukimpenda malaika basi mbingu zitajua ,dunia yote itajua na kila mtu atatambua hilo

Wewe ni malaika jua hilo , nakupenda sana , nakutamani sana , nafikiria sana kuhusu wewe muda mwingi , napenda kuwa na wewe muda mwingi sema majukumu tu yanatufanye tuwe mbali mbali .

Napenda kukuhakikishia mapenzi ya dhati toka kwangu kuja kwako , na ndio namaliza kuandika hata hamu ya kula sina tena nangoja majibu yako mpenzi , nilikuwa na njaa kidogo hapo nyuma kwa kuandika kuhusu wewe tu njaa imeisha
 
ninachoandika kinaenda kwa malaika Fulani aliyembinguni ambaye ni wewe .

POLE SANA KWA KUMFANYA MWANADAMU MWENZAKO MALAIKA WAKO - ANGALIA hatua zako SHY - Kitabu cha Mithali kinasema"IKO NJIA IONEKANAYO NI NJEMA MACHONI PA MTU..... KUMBE MWISHONI NI NJIA YA UPOTEVU" Mtangulize Mungu kwenye mahusiano yako - usiendeshwe na HISIA - HUU NI USHAURI WA BURE
NIMEAMUA NIKUPE kama kweli uliyomwandikia mpenzi wako ni kweli au ...ndoto za alinacha
 
KakaJimmy, elewa kuwa ndoa ni wewe na mkeo mtataka iwe mtakavyo!!! Mmoja akibadilisha utaratibu wa awali, basi fahamu na mwingine ni automatic. Amini kuna ndoa ambazo zimekuwa na maisha ya mapenzi, uaminifu hadi mwisho, hata kama kuna some misunderstandings but zinakuwa minimal and solved in time. Usikae na donge moyoni hata kama ni ndogo kama mbegu ya haradhani. I have more than 20 years of dedicated marriage with four children!!! (ninaposema more than 20, just imagine numbers 20 <Y<35!!!!)
Mkuu Maane,miaka 20 kwenye ndoa mbaaaaado Mkuu,maana kama mke aliolewa at 25 sasa ndo kwaaaaaanza amekuwa mama mbichi wa 45 years young,mume naye hali kadhalika kama alioa at 30 ndo ana turn 50,umri ambao ni mbaya na hatari kweli kweli maana ndo cancer ya middleage crisis inapanda kichwani hasa kwani hapo sasa watoto wamekua na kuondoka nyumbani,malengo mengi ya kiuchumi kama kujenga nyumba unakuwa umeyatimiza,ka investment ka uzeeni kama kuwa na ka guest house unakuwa umejenga,kwa kifupi challenges za maisha zinapungua na boredom ina set in. Maane sijui wewe ni muumini wa dini gani lakini nakushauri wewe na mwenza kama mnasali endeleeni kusali na kuomba,maana sisi wengine tumeona mengi na tumeshika adabu kuhusu neno 'ndoa'. Wahenga walisema 'hujafa hujaumbika'.
 
Sasa huyu naye! Ananikumbusha tulivyokuwa ma-teenagers tulivokuwa tukiwaandikia wapenzi wetu kwa maneno kama: "Nakupenda sana, usiku silali nakuota wewe". Sasa huyu naye na utu uzima wake (au kijana?) anaandika mahaba ya ki-teenagers!
 
huyu hivi ni mtu mzima au kijana?
kama ni mtu mzima nadhani ndo wale ambao muda wa kuinjoi uliwapita sijui walikua wanakamua nondozzz?, sasa inabidi walipizie ukubwani hahahaaaaa
jamaa anaota ndoto za mchana!!.
 
kaka mapenzi sio kuongea sana.Mapenzi ni vitendo,kilichotakiwa ni mtu unaye mpend a ndiyo aonyeshe appriciation kwako na siyo wewe mwenyewe ujipe maujiko hooo nitakuwa baba bpora,shat up,How sure are u?!who told you that!?unaweza sema unatoa promise kwa demu wako but according to African culture there is no chance for making promice!you better know that!
 
Back
Top Bottom