Nitajiuzulu ikithibitishwa - Sadick

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki, ametishia kujiuzulu endapo itathibitika kuwa amechakachua posho katika milipuko wa mabomu iliyotokea katika kambi ya Jeshi Gongo la Mboto.
Sadiki amesema kuwa, licha ya wakazi kuwa na wasiwasi juu ya ujenzi wa nyumba na kuhisi huenda zoezi hilo halitakamilika amesema zoezi hilo litakamilka na kudai atajiuzulu endapo itathibitishwa kula fedha hizo na kutengwa kwa fungu la watoa tathimini.

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, na kusema kazi ya kufanya tathmini ni ya serikali.

Hayo yamekuja baada ya malalamiko ya maofisa wanaofanya tathimini za nyumba kudai posho na ambapo fungu la posho hizo hazikutengwa na serikali na maofisa hao kudai kutafunwa kwa posho.

Amesema ujenzi wa nyumba utaanza mara baada ya kukamilika kuwalipa fidia watu wote ambao nyumba zao zilipigwa na milipuko ya mabomu

Pia Sadiki alisema zoezi la ufyatuaji wa matofali ya kujengea utaanza mara baada ya kumalizika kwa tatizo la umeme kumalizika katika mitambo ya kufyatulia matofali ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
 
Back
Top Bottom