Nitaisafisha BoT - Ndulu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Kama kweli una nia ya kuisafisha BOT basi aanza na kuwafukuza kazi wale wote waliohusika na malipo hewa ya shilingi 133 bilioni na uhakikishe wanatiwa ndani mara moja ili wasivuruge ushahidi. Hiyo ndio inastahili iwe hatua yako ya kwanza, vinginevyo itakuwa ni usanii tu ambao umeshatuchosha.

Nitaisafisha BoT - Ndulu

na Joseph Senga
Tanzania Daima

GAVANA mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, amesema jukumu lake la kwanza litakuwa ni kusafisha mazingira machafu ndani ya taasisi hiyo nyeti, ambayo inakabiliwa na tuhuma mbalimbali za ubadhirifu.
Ndulu ambaye ndiye aliyetangazwa kuchukua nafasi ya Daudi Balali, aliyeachishwa kazi jana, aliyasema hayo jana hiyo hiyo wakati alipofanya mahojiano ya ana kwa ana na Tanzania Daima ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Alisema anatambua wasiwasi ambao umewajaa Watanzania ambao sasa hawana imani na Benki Kuu, kutokana na tuhuma za ubadhirifu katika taasisi hiyo kubwa na nyeti.

"Nitahakikisha tunasafisha kwa kila hali chombo hiki ili kurudisha imani ya Watanzania, hasa kutokana na maovu haya ya ubadhirifu mkubwa wa fedha uliojitokeza. Hiki ni chombo cha Watanzania, nawahakikishia kwamba nitasimamia hilo kwa nguvu zangu zote," alieleza.

Aidha, alikitaja kipaumbele chake cha pili katika wadhifa wake huo mpya kuwa ni pamoja na kuweka nguvu na akili zote katika kudhibiti mfumuko wa bei ili kuufanya uchumi uendelee kuwa imara na usioyumba.

Akielezea mikakati ya kukamilisha hilo, alisema atahakikisha anaanzisha mipango ya kiuchumi itakayofanikisha kushuka kwa kiwango cha riba, ili kuwawezesha wananchi kukopa katika mabenki.

Kipaumbele cha tatu ambacho alikitaja gavana huyo mteule ni kusimamia vizuri uendeshaji wa mabenki, ili kujenga kizazi kipya kwa kuwapa nafasi zaidi vijana ambao wana uwezo na nguvu kubwa.

Akizungumzia kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo, Profesa Ndulu alisema uteuzi huo ameupokea kwa moyo mmoja na kwamba Rais Kikwete ameonyesha kuwa ana imani kubwa kwake.

Alisema kutokana na imani hiyo, atajitahidi na yeye kwa upande wake kutoa mchango mkubwa katika kuiendesha taasisi hiyo.

"Kwa ujumla nimefurahi sana, pamoja na hali ngumu, lakini rais ana imani na mimi kuwa nitatoa mchango mkubwa kurudisha hadhi ya BoT, ninamheshimu sana, ninamfahamu vizuri, nimewahi kushirikiana naye wakati nikiwa Mwenyekiti wa kwanza wa TRA, nitampa support ya kiakili na nitakuwa mkweli," aliongeza.

Profesa Ndulu pia alisema atatoa ushirikiano mkubwa kwa timu iliyoundwa na rais, ambayo itayafanyia kazi kisheria matatizo ya ubadhirifu uliobainishwa kupitia ukaguzi uliofanywa na Kampuni ya Ernst & Young.
 
Wakati wa maneno umepita tunataka vitendo,kinachoruponza tz ni maneno ya kisiasa lakini serikali ingekuwa inafanyia kazi maoni ya kitaalamu tungekuwa mbali.Kuoneana aibu kuishe tuwaige wa Rwanda wana zero tolerance to corruption and embellezlement.Mhe.Ndullu tunahitaji kuona vitendo
 
Jamani nadhani ndio maana watu wanasema watanzania tunaongea sana. Watu wamechoshwa na kusikiliza hizo ngonjera tunataka vitendo na tuone matokeo.

Ndio kasema tumpe nafsi ajipange ila sasa watanzania hatutaki tena maneno bwana ni uwajibikaji. Tunataka tuone output, tumeshachoshwa na ahadi kuanzi viongozi wetu wa juu hadi mademu wetu ni ahadi kila kukicha.

Wajibisha waliotuhumiwa mara moja ndio tuone unafanya kazi Prof Usije ukawa nawe uankuwa mwanasiasa. Otherwise tumtakie kila lakheri na Mungu amsaidie asiingiwe na tamaa za ufisadi maana watu wanateuliwa wakiwa na mikono misafi wakifika huko wanabadilika.
Mungu bariki Tanzania.
 
Most of the time maprof ni watu wa principles I hope it will be the same kwa uyu ndugu yetu.
Japo awaonee huruma watanzania wanaotaabika ata the expense of few vultures.
All the best Prof Ndulu
 
Am sure Prof Ndulu atairekebisha BoT kwani nadhani ameshaona yaliyotokea kwa mwenzake aliyekuwepo (Balali). Kwahilo nampongeza sana Kaka JK kwa marekebisho aliyoyafanya,let us wait and see the repacation
 
Sijui kama anakumbuka hili. Mihemko na mbwembwe zikaishia mikononi mwa wanasiasa wasioipenda nchi yao. Wakaweka ndani ya benki yetu watoto wao ili wafanikishe wizi wao.
 
Umhh, aliongea hayo maneno 2008 kumbe , yule mkuu anayemtetea huyu jamaa sijui yuko wapi
 
Kama kweli una nia ya kuisafisha BOT basi aanza na kuwafukuza kazi wale wote waliohusika na malipo hewa ya shilingi 133 bilioni na uhakikishe wanatiwa ndani mara moja ili wasivuruge ushahidi. Hiyo ndio inastahili iwe hatua yako ya kwanza, vinginevyo itakuwa ni usanii tu ambao umeshatuchosha.

Nitaisafisha BoT - Ndulu

na Joseph Senga
Tanzania Daima

GAVANA mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, amesema jukumu lake la kwanza litakuwa ni kusafisha mazingira machafu ndani ya taasisi hiyo nyeti, ambayo inakabiliwa na tuhuma mbalimbali za ubadhirifu.
Ndulu ambaye ndiye aliyetangazwa kuchukua nafasi ya Daudi Balali, aliyeachishwa kazi jana, aliyasema hayo jana hiyo hiyo wakati alipofanya mahojiano ya ana kwa ana na Tanzania Daima ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Alisema anatambua wasiwasi ambao umewajaa Watanzania ambao sasa hawana imani na Benki Kuu, kutokana na tuhuma za ubadhirifu katika taasisi hiyo kubwa na nyeti.

"Nitahakikisha tunasafisha kwa kila hali chombo hiki ili kurudisha imani ya Watanzania, hasa kutokana na maovu haya ya ubadhirifu mkubwa wa fedha uliojitokeza. Hiki ni chombo cha Watanzania, nawahakikishia kwamba nitasimamia hilo kwa nguvu zangu zote," alieleza.

Aidha, alikitaja kipaumbele chake cha pili katika wadhifa wake huo mpya kuwa ni pamoja na kuweka nguvu na akili zote katika kudhibiti mfumuko wa bei ili kuufanya uchumi uendelee kuwa imara na usioyumba.

Akielezea mikakati ya kukamilisha hilo, alisema atahakikisha anaanzisha mipango ya kiuchumi itakayofanikisha kushuka kwa kiwango cha riba, ili kuwawezesha wananchi kukopa katika mabenki.

Kipaumbele cha tatu ambacho alikitaja gavana huyo mteule ni kusimamia vizuri uendeshaji wa mabenki, ili kujenga kizazi kipya kwa kuwapa nafasi zaidi vijana ambao wana uwezo na nguvu kubwa.

Akizungumzia kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo, Profesa Ndulu alisema uteuzi huo ameupokea kwa moyo mmoja na kwamba Rais Kikwete ameonyesha kuwa ana imani kubwa kwake.

Alisema kutokana na imani hiyo, atajitahidi na yeye kwa upande wake kutoa mchango mkubwa katika kuiendesha taasisi hiyo.

"Kwa ujumla nimefurahi sana, pamoja na hali ngumu, lakini rais ana imani na mimi kuwa nitatoa mchango mkubwa kurudisha hadhi ya BoT, ninamheshimu sana, ninamfahamu vizuri, nimewahi kushirikiana naye wakati nikiwa Mwenyekiti wa kwanza wa TRA, nitampa support ya kiakili na nitakuwa mkweli," aliongeza.

Profesa Ndulu pia alisema atatoa ushirikiano mkubwa kwa timu iliyoundwa na rais, ambayo itayafanyia kazi kisheria matatizo ya ubadhirifu uliobainishwa kupitia ukaguzi uliofanywa na Kampuni ya Ernst & Young.
Benno Ndulu failed "to walk the talk"; he lied and cheated the nation and consequently the nation suffered losses of multi billion shillings; ATUMBULIWE haraka.
 
After all these years he has done nothing till last week when His excellence President Magufuli went in to reveal bolshit that has been going on since then. Can he read his 2008 statement??? Nchi hii kusema kweli imekwisha kabisa
 
Mkuu BAK, ulikuwa wapi kiongozi? Tumekuulizia sana hapa mtandaoni bila jibu. Karibu sana!.

Kama kweli una nia ya kuisafisha BOT basi aanza na kuwafukuza kazi wale wote waliohusika na malipo hewa ya shilingi 133 bilioni na uhakikishe wanatiwa ndani mara moja ili wasivuruge ushahidi. Hiyo ndio inastahili iwe hatua yako ya kwanza, vinginevyo itakuwa ni usanii tu ambao umeshatuchosha.

Nitaisafisha BoT - Ndulu

na Joseph Senga
Tanzania Daima

GAVANA mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, amesema jukumu lake la kwanza litakuwa ni kusafisha mazingira machafu ndani ya taasisi hiyo nyeti, ambayo inakabiliwa na tuhuma mbalimbali za ubadhirifu.
Ndulu ambaye ndiye aliyetangazwa kuchukua nafasi ya Daudi Balali, aliyeachishwa kazi jana, aliyasema hayo jana hiyo hiyo wakati alipofanya mahojiano ya ana kwa ana na Tanzania Daima ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Alisema anatambua wasiwasi ambao umewajaa Watanzania ambao sasa hawana imani na Benki Kuu, kutokana na tuhuma za ubadhirifu katika taasisi hiyo kubwa na nyeti.

"Nitahakikisha tunasafisha kwa kila hali chombo hiki ili kurudisha imani ya Watanzania, hasa kutokana na maovu haya ya ubadhirifu mkubwa wa fedha uliojitokeza. Hiki ni chombo cha Watanzania, nawahakikishia kwamba nitasimamia hilo kwa nguvu zangu zote," alieleza.

Aidha, alikitaja kipaumbele chake cha pili katika wadhifa wake huo mpya kuwa ni pamoja na kuweka nguvu na akili zote katika kudhibiti mfumuko wa bei ili kuufanya uchumi uendelee kuwa imara na usioyumba.

Akielezea mikakati ya kukamilisha hilo, alisema atahakikisha anaanzisha mipango ya kiuchumi itakayofanikisha kushuka kwa kiwango cha riba, ili kuwawezesha wananchi kukopa katika mabenki.

Kipaumbele cha tatu ambacho alikitaja gavana huyo mteule ni kusimamia vizuri uendeshaji wa mabenki, ili kujenga kizazi kipya kwa kuwapa nafasi zaidi vijana ambao wana uwezo na nguvu kubwa.

Akizungumzia kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo, Profesa Ndulu alisema uteuzi huo ameupokea kwa moyo mmoja na kwamba Rais Kikwete ameonyesha kuwa ana imani kubwa kwake.

Alisema kutokana na imani hiyo, atajitahidi na yeye kwa upande wake kutoa mchango mkubwa katika kuiendesha taasisi hiyo.

"Kwa ujumla nimefurahi sana, pamoja na hali ngumu, lakini rais ana imani na mimi kuwa nitatoa mchango mkubwa kurudisha hadhi ya BoT, ninamheshimu sana, ninamfahamu vizuri, nimewahi kushirikiana naye wakati nikiwa Mwenyekiti wa kwanza wa TRA, nitampa support ya kiakili na nitakuwa mkweli," aliongeza.

Profesa Ndulu pia alisema atatoa ushirikiano mkubwa kwa timu iliyoundwa na rais, ambayo itayafanyia kazi kisheria matatizo ya ubadhirifu uliobainishwa kupitia ukaguzi uliofanywa na Kampuni ya Ernst & Young.
 
BOT ni jipu au tezi dume. Haiwezekana hata Chase Manhatan hawana wafanyakazi wengi.
Dunno kwanini HR BOT haina initiative za kupeleka wafanyakazi wao banks kama African Development Bank, Asian Development Bank,IMF,Switz etc
Unakuwa ba watu wasomi lakini wana mawazo static not proactive and dynamic very rigid. Tuige Nigeria na Ghana jamani huwezivkuwa na senior economist anaishia magogoni tu data zake kila siku ni za mikoa hii 26 sijui. Au Forex dealer ambaye anaishia data za vibenki vyetu tuu.
~
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom