Nissan x trail mwenye uzoefu nazo msaada

Gamaha

JF-Expert Member
Jul 17, 2008
3,815
4,860
Waungwana heshima mbele kwa wote, Jamani mwenzenu nimepata vihela kidogo nataka kuagiza gari angalau ninayo ipenda, napenda sana nissan x trail lkn sijui kuhusu hizi gari je zina matatizo gani sugu, vipi upatikanaji wa spare parts na gharama za spare parts muungwana yeyote kama anajua hizi gari pls naomba nijue ili nisiingie mkenge, pesa yenyewe nimepata kwa manati sana loh.
 
Kamanda X-Trail ni gari bomba sana ni imara, fuel efficient, na large space kama unafamilia ni gari worth it. Mie nawashangaa watu wanashabikia Rav-4 but Rav4 2 ndio X-Trail.

Kinacholalamikiwa ni bei za spare za X-Trail ni expensive but ukifunga spea moja unasahau sasa kipi ununue spea rahisi za rav-4 halafu ukae kila wiki ukibadilisha au ufunge kitu usahau nakuachia mwenyewe ujaze

kila la kheri
 
Ndugu yangu
Gari hiyo ni nzuri sana on and off the road. Spare hivi sasa si matatizo ila kama una hela ya manati achana nayo kwani ukitaka kuishi vizuri na gari hii regular service is a must na bwana mzee si unajua nissan tena?
 
Dashboard yake sikuipenda....kama trekta bana

Mie kila nikiicheck hii gari huwa naona kama vile inaendeshwa kwa "remote", manake walivyoweka hiyo dashbord utadhani iliwa stragegically ili iweze kupokea mionzi vyema bila kujali kuwa umekaa siti ya nyuma au ya mbele.

Ila model mpya sasa dashbord imekaa poa, taabu ni kama ujuavyo tena tunajinafasi kwa used tu!
 
Acha kama ni gari yako ya kwanza wawezakufa kwa force over area!

he he nimegundua mkuu kumbe ni pressure loh sijui physikia ilipotelea wapi any way niambie basi angalau kasababu why nife na force over area
 
Waungwana heshima mbele kwa wote, Jamani mwenzenu nimepata vihela kidogo nataka kuagiza gari angalau ninayo ipenda, napenda sana nissan x trail lkn sijui kuhusu hizi gari je zina matatizo gani sugu, vipi upatikanaji wa spare parts na gharama za spare parts muungwana yeyote kama anajua hizi gari pls naomba nijue ili nisiingie mkenge, pesa yenyewe nimepata kwa manati sana loh.

Unataka kuagiza wapi, ni ya mwaka gani, na kwa kiasi gani...tuanzie hapa kwanza.
 
Huu ni msimu wa kilimo kwanza , ulizia bei ya matrekta ntakwambia hapa India ni kiasi gani.
 
Huu ni msimu wa kilimo kwanza , ulizia bei ya matrekta ntakwambia hapa India ni kiasi gani.

he he mkuu trecta ntalima wapi mimi ndugu yangu hapa dar tunahangaika sana na dala dala jamani loh,
 
Huu ni msimu wa kilimo kwanza , ulizia bei ya matrekta ntakwambia hapa India ni kiasi gani.

Mkuu mimi nina shida kweli na trekta hebu nipe bei na gharama za kuisafirisha kuja Dar. Isiw iliyochoka sana lakini.
 
Waungwana heshima mbele kwa wote, Jamani mwenzenu nimepata vihela kidogo nataka kuagiza gari angalau ninayo ipenda, napenda sana nissan x trail lkn sijui kuhusu hizi gari je zina matatizo gani sugu, vipi upatikanaji wa spare parts na gharama za spare parts muungwana yeyote kama anajua hizi gari pls naomba nijue ili nisiingie mkenge, pesa yenyewe nimepata kwa manati sana loh.

Nina rafiki yangu nikiwa huko bongo aliwahi kuipaki hiyo gari mwaka mzima kwakuwa Control box ilikufa, hata sijui amefikia wapi, kikubwa ni kwamba spareparts availability ya hiyo gari ndio issue kwa hiyo mzee kama ni gari yako ya kwanza, mmh...fikiria mara mbili, lakini kam vijisenti vimekutembelea na una uhakika vitaendelea kukutembelea, aaah, kula kitu roho inapenda. Ni hayo tu mkuu Gamaha.
 
Back
Top Bottom