nishaurini jamani

hana haya huyu! anasema kabisa nataka niingie chumbani kwako! anasema saingine nataka niende toilet lkn ctak toilet ya nje nataka ya chumban kwako!

Mtolee nje mwambie mama huku ni chumbani kwetu kuna choo kingine tena ni kisafi unaweza kutumia hicho. Kuhama karibu naye ni muhimu sana kama mnaweza kufanya hivyo la haiwezekani basi mwambie mumeo yanayojiri ingawaje kwa jinsi anavyompenda mama yake anaweza asitie neno. Pole sana.
 
Mambo mengine ni umri, bado uko kwenye steji ya kudeka.

Unajikanganya, mara useme umeshazoea matusi ya mama mkwe, mara useme mnaishi vizuri na wifi zako, mara wifi anakupekua.

Am too old for this aisee.
 
Mambo mengine ni umri, bado uko kwenye steji ya kudeka.

Unajikanganya, mara useme umeshazoea matusi ya mama mkwe, mara useme mnaishi vizuri na wifi zako, mara wifi anakupekua.

Am too old for this aisee.[/
cjapekuliwa na wifi angu hata cku moja! hujaelewa wapi kwengine?
 
hana haya huyu! anasema kabisa nataka niingie chumbani kwako! anasema saingine nataka niende toilet lkn ctak toilet ya nje nataka ya chumban kwako!

kwa hiyo akikwambia hivyo na wewe unamfungulia? Si umwambie hapana sio heshima? Kwani ukimkatalia akianza kuchonga wewe unachubuka ng'ozi? Unyonge wako ndio unaokuponza.

Hebu mlete kwangu huyo mkweo kwa wiki mbili tu nimnyooshe
 
thx ndugu yangu! cku ile alipofungua walet yangu nlishtuka na kujikuta namwambia "hapana mama usifungue ifunge" akacheka anasema unaogopa nn???unadhan ntakufumania! da! nlikaa kimya tu

hukutakiwa kumwambia 'hapana mama' ulipaswa kumpokonya hiyo wallet, then unamwambia tabia hiyo huipendi. Full stop
 
hakuna kitu kibaya kama kuishi ndani ya ndoa kwa woga
funguka mama mwmabie live mumeo na pia mama mkwe mweleze live tena sema wakiwa wote
maisha ya ndoa ni ww na mumeo mama mkwe hana nafasi ya kuwaingilia hata kidogo
kuwa mkali linda ndoa yako na fuata ushauru wa badili tabia na boss, HAMENI.
HUYO BAZAZI HAFAI KUITWA MAMA MKWE.
 
Naamin unatakiwa kujiamini na kukemea yote ambayo si sahihi au yaendayo kiyume na yatakiwayo kwako .. kwnza unatakiwa kuamini pale ni kwako nna mmeo kwa maana hiyo maamuzi ni yako na mwenzi wako na si mtu mwingine haijalishi ni nani. pia ni vyema mkashauriana na mmeo mkahama hapo mlipo kwani kukaa karibu na wakwe tayari mnayakaribisha matatizo madogo madogo ambayo yanaweza kuwasababishia magomvi ya mara kwa mara na kuyumbisha ndoa yenu.. ulipomkuta kafungua walet kimsingi ulitakiwa kumweleza ikiwezekana hata kumkemea kuingia chumbani kwako kwani si vyema akaingia pasi mtu au mhusika wa rum kuwepo ..
 
hapo ushauri ni kuhama
kwenda kuishi mbali na huyo 'mwehu'

hivyo sio visa
huyo ni mgonjwa.....mumeo angekuwa muelewa
mngempeleka hospitali kwanza

Nakubaliana na wewe kuwa kukaa nyumba moja au karibu na mama mkwe ni janga kwenye ndoa nyingi
Lakini pia sikubaliani na wewe kumuita huyu mama mwehu just kwa kuamini maneno ya upande mmoja
 
umekuwa mpole mno i guess... desperate situations require desperate measures... be tough!
 
we kongosho uwe unasoma vzur thread za watu sio unakurupuka anaepekua pochi sio wifi soma tena usikurupuke kama bao la kwanza
 
Big One, bora ungekuwa small two.

Niwe nimekurupuka au nimejikurupua, ugomvi wa kitoto huu, siwezi toa suluhisho zaidi ya huyu binti akue, period.

we kongosho uwe unasoma vzur thread za watu sio unakurupuka anaepekua pochi sio wifi soma tena usikurupuke kama bao la kwanza
 
Last edited by a moderator:
kwa ushirikina ndo mwenyewe haswaa! anayapenda sana! amemloga mumewe hadi basi lkn Mungu mkubwa atanisaidia

pole sana dada kwa maswahibu yote. km una uhakika ni mshirikina.. omba sana Mungu azungumze naye km we ni mkristo. kemea nguvu za giza na tabia ya mkweo. Mungu ni mwema na hapendi uteseke ktk ndoa yako. kakupa mume mwema na ndiye msimamizi wa ndoa yako.cmama imara ktk nafasi yako. wahenga husema "mchawi mpe mtoto alee"mkemee mkweo kwa adabu, mseme anapokosea ucogope!
 
Dada korino pole kwa haya unayopitia. Ni kazi sana kulea ndoa kama alivyosema Jestina ila nakwambia kazi siyo kuilea bali kazi ni kuamua kuilea ndoa. ushauri wangu kwako ni huu na ukichanganya na wajumbe wengine utapata pa kutokea.

kwanza kwa muda wa mwaka mmoja, bado hujaona ma dia so just keep and wait to see more. Kwanza huyu mama ni miongoni mwa wale wazazi ambao hata kama mtoto wao amekuwa na kuona basi anataka awe contol rum ya hiyo familia ya mtoto wake. Huyu hutamani kuona kila kitu kinafanyiwa correspondence kwake mfano kama kuna mgeni aambiwe, kama kuna mipango ya maendeleo ashirikishwe kitu ambacho huwa sikipendi kabisa. mama huyu hufikia hata kutaka kujua kuwa mumeo anakupa nini na kwa wakati gani.

Tabia nyingine ambayo ni mbaya hapa naiona kwako na kwa mumeo,( nisamehe sana kwa haya na si nia yangu bali tunataka kujenga tu). ninyi sidhani kama wakati mnaoana mlikuwa mmefikia umri wa kuoa kiakili.(samahani initetee). kwanini nasema haya mngekuwa mmekuwa kiakili kiasi cha kufikia mentally kuoa basi jambo la kwanza kabisa mngekuwa na saying juu ya maisha yenu wenyewe. na kama mngelitaka hili mngejifunza kuwa huru kwa kukaa mbali na wazazi wa pande zote mbili. hili wala haliihitaji mtu akuelimishe. mwendo wa dk 10 unaousema na pata picha kuwa ni mtaa mmoja huo. Hapa mlikosea sana na nafikir mlipokuwa mnapanga kuish ahapo mlilenga kupata msaada wa karibu kutoka kwa ndugu wa mume tena naona jins mumeo alivyokuwa anakuaminisha juu ya kupata cheap labour hasa utakapojifungua. hili ndilo kosa kubwa mlilolifanya. hata kama ni kazi mlitakiwa mwende kupanga mbali na hiyo familia wakwe unawaona once in a blue moon.

cha kufanya sasa ongea na mumeo pasi kumficha ila kwa utaratibu kwa nidhamu, na kwa hisia sana ili akuelewa. tena wakati unamuelewesha juu ya hii hali hakikisha uwe vigezo vyako vimewapita hao ndugu wa mume, hapa namaanisha yale ya kwako kama mke uwe umeyatimiza kwa nidham ya hali ya juu. jitahd usikurupuke mweke mumeo kwenye mstari kimahaba kwa muda kidogo hadi ufanikiwe kuiteka akili yake, ukisha fanikiwa basi mweleze tena ukiwa na solution ila dont mention it mpaka yeye apropose. atakacho kipropose yeye basi hakikisha kinakufavour wewe kwa kiasi kikubwa. Ukitaka kumnunua vizuri huyo mumeo basi vijizawadi visikosekane, mpatie hata kama ni vijisoksi tu ili kumteka zaid.

katika solution taka kuhama eneo hilo kapange nyumba mahali ambapo ni mbali zaid na wao na ukienda huko simama wewe na mumeo mjitegemee. hakikisha kila kitu mnafanya wewe na mumeo wala usitake ushauri kwa upande mwingine. pia jiaminishe manake kutakataka misaada ukweni ndipo kunakoleta shida sana kati ya wanandoa.

kuna post niliwah kuandika nikatoa kanuni ya kuish na mama mkwe ni leo nairudia tena kwa ajili yako
- muheshimu kuliko mama yako
-usiwe mchoyo
- usiwe na ukaribu naye hata kidogo
- hakikisha mumeo anatimiza wajibu wake kwa mama yake.
- asijue mambo yako ya ndani hata kidogo chumbani kwako ni siri yako pia.
-umwombe mungu sana manake yeye ndiye atupaye hekima za kuweza kuish katika ndoa zetu
Hebu jaribu haya.
 
Last edited by a moderator:
solution ya hilo tatizo lako ni wewe kuhamia mbali na mama mkwe wako ili muwe mnaonana mara chache kwa hamu,wamama wengine watoto wao wanataka wawamiliki hata kama wakioa!wewe mpende kama kawaida ila akili kichwani kwako muhame hapo,na kuwa makini na chumba chako.
 
pole sana ndio maisha ya ndoa za kibongo. ata hivyo ni upepo tu utapita. muombe mungu akupe busara ya kutatua hilo tatizo.
 
Kuingia kwenye ndoa nazidi kugundua ni UAMUZI mgumu. Khaa likikupita kwa mume, walikuta kwa mama mkwe, likikupita kwa mama mkwe walikuta kwa mawifi na mashemeji. Duh Mungu akusaidie tu dada, akupe hekima ya kupita kwenye hilo jaribu.
 
Hili la mama mkwe ni tatizo kubwa,
kila upande ni mama mkwe,
kwa kweli sitatamani kuishi jirani na mkwe wangu
naogopa kukosana.
 
Back
Top Bottom