GHOST RYDER
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 1,025
- 475
Nishati na Madini siku 21 zimekwisha
Huku Jairo akisukumiwa Tuhuma nyingine jana kama njia na kamtego hivi kupoteza lengo na kuwasahaulisha Watanzania uozo katika Bajeti ya Awali ya Wizara hiyo iliyogonga mwamba mwezi uliopita, siku zao 21 zimekwisha na Jumamosi wanarejea tena Bungeni kuwasilisha Bajeti yao itakayosomwa kwa siku moja na kisha kuputishwa ama kutopitishwa.
My Take:
- Unafiki wa wabunge na makundi utaona yanavyofanya kazi Jumamosi.
- Sina shaka semina zimeshapigwa vya kutosha kama ilivyookolewa Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi
- Mie binafsi sitegemei muujiza wowote kesho wala jipya zaidi ya Bajeti kupita katikati ya Giza
- Ahadi zitajaa zenye ladha saafi kama asali na wingi wa hoja za kinafiki kama mkia wa kondoo
ADIOS