Nishati na madini Count down: Maamuzi mazito yanakuja

Kwa ccm kuonesha (walau kama gesture) kutambua tatizo la umeme ni vizuri kwanza wamtose Ngeleja! Hakuna mtu mwenye imani na huyu Waziri.

Kwa wanaojua, nini kitatokea kama bajeti ya Wizara itakataliwa?

Jamani huu ni mwaka wa ngapi umeme ni wa wasiwasi? Badala ya kumtoa sadaka mtu mmoja natamani magamba wote wangepigwa chini.
 
Pinda kamfukuza kazi jairo! Mbuzi wa kafara wakati wanafunga majenereta ubungo kufunika kombe ndani ya wki tatu
 
Hapa tunacheza na wao CCM wanataka kuonyesha gesture kwa watanzania at least they are trying to outsmart Upinzani Bungeni lakini hawana dhamira ya kweli .Issue hii ni nzito mno .Ngeleja hakuwa na hana uwezo wa kuwa waziri wa ile Wizara but karudishwa pale si kwa bahati mbaya people wake up .Ngeleja ni corrupt na watu wote walio fika kwake na nia yaa kulegta umeme bila ruishwa walipigwa chini kabisa na analinda madhambi ya mkuu .Katibu mkuu kaja pale ni mpya huyu kumpa mzigo si sahihi kwani yeye atafanya nini wakati mwisho wa siku ni Ngeleja mwamuzi?Shida hapa ni CCM na JK mwenyewe wala si KM kama wanavyo taka tuamini .Pale kwa Ngeleja utapata kazi yeyote kama una 10% mbele.Kama CCM wako serious mbona hatuoni wana shughulika na walio toa hongo? Hii ni kashfa kubwa Ngeleja na alitakiwa kuwa nje ya ofisi lakini bado yupo leo mnasema nini ? Haya naendelea kusoma lakini huu ni mchezo tu .

Umeme na madini unawapa rushwa kubwa sana wakubwa na ndiyo maana hawako tayari kuiachia tanesco .Ngeleja amekalia proposal kibao za wazalisha umeme hata hajibu lolote wazungu wanalia na hawataki kuamini kwamba Tanzania ana shida .Nina ushahidi wa kampuni moja inaitwa Genesis walikuja Tanzania toka US wakataka kuzalisha umeme wa 2000mw .Hadi leo hawajajibiwa na Ngeleja aliwaambia mradi uelekezwe kwake ndiyo atakubali wakashangaa sana .Waka spend muda waka change the whole proposal ya kutoka kuvuna umeme maeneo ya Arusha na kuupeleka kwenye National Grid lakini wakalazimika ku change na hadi sasa Ngeleja kakaa kimya .Walikuja mwaka Jana mwezi wa 2 na walikaa Tanzania siku 14 .

Walikutana an Ngeleja na wataalam wake wote na hata tanesco kwenye board room lakini muulize Ngeleja walijibu nini hadi sasa .Wazungu wale wana andika kitabu kinaitwa we lost in Tanzania for Corruption.
 
Jamani twende mbele turudi nyuma: Mimi binafsi nachukia sana nchi kuwa gizani lakini mbona Ngeleja anakuwa mbuzi wa kafara? Hivi kosa la Ngeleja ni lipi? Ni kwamba hashauri vizuri au ni kwamba nchi haina pesa za kuwekeza kwenye umeme? Hivi hili ni suala la Ngeleja binafsi au ni suala la Serikali nzima?

Nakubaliana na wewe kwa upande mmoja kuwa kama Ngeleja ana kosa, kujiuzulu kwake hakutatatua tatizo katika wakati mfupi (short term) au wa kati. Ila kinachoeendelea nadi ya CCM ni kutafuta namna ya kupata support na haiwezekani sana bila kutoa mbuzi wa kafara sababu hili si suala la Ngeleja binafsi. Ki msingi wizara imeshindwa na akijiuzulu hatakuwa kwa sababu yeye kashindwa ila wizara anayoiongoza imeshindwa. Kama akibwaga manyanaga, hakuna atakayechukua nafasi yake na kuwasha umeme full time kesho. Hakuna!
 
Mambo tayari bunge limeahirishwa mpaka kesho.bajeti ipo pending waziri mkuu kaomba wiki3 wakatafute mikakati ya umeme wa dharura then bajeti itarudi kujadiliwa tena.ila mwisho wa jairo unanukia.
 
Waziri mkuu,mizengo kayanza peter pinda ameomba wizara ya Nishati na Madini ipewe muda wa wiki tatu zaidi ijipange kutoa bajeti yake.Hali halisi inaonesha kwamba bajeti ya wizara ya nishati na madini haijitoshelezi hasa katika tatizo kuu linaloikabili nchi(Tanzania) i.e mgao mkali wa umeme.Pia waziri mkuu adai kukereka mno na maelezo na majibu mkato ya katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini,atamani angekuwa na mamlaka ya kumvua uongozi huyo katibu mkuu.Waziri mkuu ameliwasilisha hili suala la huyu katibu mkuu wa nishati kwa rais JMK aliyeko wizarani Afrika kusini.
 
Lakini kumuwajibisha Jairo na kuwaacha mawaziri wake waendeleze sinema ya mgao inatia shaka juu ya hoja ya KULINDANA kwa wanasiasa..je ina maana perm sec aliandika barua hiyo ya kuchangisha 50m za lobbying bila ya waziri kujua?
 
Kaazi kweli kweli!! naona wanatufanya sisi wananchi mapoyoyo...Mie nshachoka na siasa za humu nchini kwetu.
 
Kwanini hicho ambacho watajipanga in the next three weeks wasingejipanga in the previous three weeks...
 
Kaazi kweli kweli!! naona wanatufanya sisi wananchi mapoyoyo...Mie nshachoka na siasa za humu nchini kwetu.
 
Waziri mkuu,mizengo kayanza peter pinda ameomba wizara ya Nishati na Madini ipewe muda wa wiki tatu zaidi ijipange kutoa bajeti yake.Hali halisi inaonesha kwamba bajeti ya wizara ya nishati na madini haijitoshelezi hasa katika tatizo kuu linaloikabili nchi(Tanzania) i.e mgao mkali wa umeme.Pia waziri mkuu adai kukereka mno na maelezo na majibu mkato ya katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini,atamani angekuwa na mamlaka ya kumvua uongozi huyo katibu mkuu.Waziri mkuu ameliwasilisha hili suala la huyu katibu mkuu wa nishati kwa rais JMK aliyeko wizarani Afrika kusini.

Huyu naye anahitaji kujiuzulu maana kazi imemshinda. Si ndiye huyu alitoa kauli za kutojua kwa nini Watanzania ni maskini na pia. "Mafisadi wa EPA ni matajiri wakubwa nchini, kama watakamatwa basi nchi itawaka moto." Pinda naye hafai nafasi yoyote katika Serikali naye pia aachie ngazi.
 
Lakini kumuwajibisha Jairo na kuwaacha mawaziri wake waendeleze sinema ya mgao inatia shaka juu ya hoja ya KULINDANA kwa wanasiasa..je ina maana perm sec aliandika barua hiyo ya kuchangisha 50m za lobbying bila ya waziri kujua?

Jairo ndio wamemtoa kafara ili kuwakingia kifua wachofu akina Ngeleja na Malima, sijui kwa maslahi ya nani?
 
Sinema ndiokwanza inaanza sasa..............ngoja tuone mambo...........TZ bana..........
 
After three weeks maamuzi 'MAGUMU' nategemea yatatolewa EL hureeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee...........
 
Mambo hapa yako uchi kabisa haiwezekani Katibu Mkuu kuchangisha pesa ili kufanikisha kupitisha bajeti ya waziri wake bila Waziri kujua. Baada ya wiki tatu tunataka yafuatayo kwanza bajeti mpya yenye kutekelezeka, Pia tunataka waraka wa kujiuzulu Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu wake Wote wawajibishwe kila mmoja kwa nafasi yake.
Nimesikia BBC kwamba makali ya mgao yataongezeka baada ya mabwawa kuzidi kukauka. Hawa jamaa wanafanya nini angalau wangekuwa wanatueleza ukweli tungewavumilia.
 
Back
Top Bottom