Nishati na madini Count down: Maamuzi mazito yanakuja

Kwa ccm kuonesha (walau kama gesture) kutambua tatizo la umeme ni vizuri kwanza wamtose Ngeleja! Hakuna mtu mwenye imani na huyu Waziri.

Kwa wanaojua, nini kitatokea kama bajeti ya Wizara itakataliwa?

Jamani eeh! Ngeleja ni golikipa tu wa hii wizara ila uwanjani wapo wengi walioboronga na kusababisha Ngeleja kuachia magoli . Cha muhimu hapa kipenga kipulizwe mechi imalizike na kila mchezaji awajibishwe kwa kucheza kizembe akiwemo mwaamuzi kushindwa kusimamia mechi(JK). Mechi hii ipigwe siku nyingine ambayo wachezaji watakuwa fiti kutumia akili zao na si kucheza kama walevi na watu wenye mtindio wa ubongo.
 
Jamani twende mbele turudi nyuma: Mimi binafsi nachukia sana nchi kuwa gizani lakini mbona Ngeleja anakuwa mbuzi wa kafara? Hivi kosa la Ngeleja ni lipi? Ni kwamba hashauri vizuri au ni kwamba nchi haina pesa za kuwekeza kwenye umeme? Hivi hili ni suala la Ngeleja binafsi au ni suala la Serikali nzima?
Siku zote huwa nasema kama wewe ni Waziri ni unaona mambo hayaendi vizuri jinsi wewe unavyotaka kwanini usijiuzulu kuepusha lawama ambazo zinaelekezwa kwako ambazo kimsingi inawezekana zisiwe zinakuhusu directly kuendelea kukaa maana yake unakubali kuwa you are part and parcel of the failure na hata watu wakikulaumu basi usilalamike ukiona kama unaonewa ni bora kukaa kando kuepusha kuwa unasimangwa kila saa na jina lako kutajwa kwenye midomo ya kila mtanzania kuwa wewe ndio chanzo cha mgao wa umeme.
 
Ngeleja hawezi kukwepa lawama hata kama mfumo ni mbovu. Mbona Magufuli anaonekana kupambana ndani ya mfumo huo mbovu? Nani asiekummbuka saga ya Mrema wa Tanroads? Shukuru Kawambwa alionekana kama mtoto kwa huyu Bwana, lakini it took Magufuli weeks to show him the door! Na kama kweli Ngeleja ni mchapa kazi basi wabadilishane wizara na Magufuli kama hautasikia bei ya kujenga barabara (per km) inapanda mara dufu!
 
Jamani eeh! Ngeleja ni golikipa tu wa hii wizara ila uwanjani wapo wengi walioboronga na kusababisha Ngeleja kuachia magoli . Cha muhimu hapa kipenga kipulizwe mechi imalizike na kila mchezaji awajibishwe kwa kucheza kizembe akiwemo mwaamuzi kushindwa kusimamia mechi(JK). Mechi hii ipigwe siku nyingine ambayo wachezaji watakuwa fiti kutumia akili zao na si kucheza kama walevi na watu wenye mtindio wa ubongo.

golikipa gani huyo mwe mpiga pelnati kapaisha nje yeye anauokota mpira na kuurudisha ndani ya goli lake?
 
Siku zote huwa nasema kama wewe ni Waziri ni unaona mambo hayaendi vizuri jinsi wewe unavyotaka kwanini usijiuzulu kuepusha lawama ambazo zinaelekezwa kwako ambazo kimsingi inawezekana zisiwe zinakuhusu directly kuendelea kukaa maana yake unakubali kuwa you are part and parcel of the failure na hata watu wakikulaumu basi usilalamike ukiona kama unaonewa ni bora kukaa kando kuepusha kuwa unasimangwa kila saa na jina lako kutajwa kwenye midomo ya kila mtanzania kuwa wewe ndio chanzo cha mgao wa umeme.

Mkuu nimekuelewa vyema. Kwangu mimi nadhani hili suala la mgao si suala la Ngeleja ni suala la serikali nzima. Mkuu kama unapangiwa budget kidogo ukiwa kama Waziri utafanyaje labda upate safari za nje ili ukawaombe wakubwa wakupe misaada kinyume na hapo hata ukipewa wewe sasa hivi hiyo wizara tutakupiga madongo tu!! Vipa umbele vya serikali inabidi vibadilike ili serikali iwekeze kwenye umeme na kulimaliza hili tatizo vinginevyo kila waziri wa nishati atapata joto ya jiwe kama Ngeleja. Najua Ngeleja ana mapungufu yake lakini kwenye umeme mimi naona kama anabebeshwa mzigo ambao si wake!
 
Nyimbo ndio zilitawala zaidi.

UMEME UTAKUWA HISTORIA...NDANI YA MWEZI MMOJA TATIZO LITAKUWA LIMEKWISHA...WIZARA IMEJIPANGA KUHAKIKISHA UMEME UNAPATIKANA NDANI YA SIKU 90 na nyimbo nyingine nzuuri, ambazo jitihada zingeelekezwa katika ununuzi wa Mitambo na kusaka njia mbadala ya Umeme hapa tungekuwa tunaongea mengine.

Au ita koleo ni koleo tu, Nyimbo hizi mara kadhaa zilipishana hata na watandaji wa TANESCO kwa kuzikanusha na wakati fulani zilimtia katika wakati Mgumu sana Idris Rashid mpaka akang'oka.

Ndugu Ngeleja nahisi alikuwa hawasikilizi sana wataalam
 
Ngereja ndo anaongoza hiyo wizara, tunategemea kuona concrete reasons zinazosababisha kuwepo na mgao wa umeme kwa muda mrefu kiasi hiki tena bila kujua ni lini tutakuwa na umeme. Amekuwa shujaa wa kutoa ahadi kibao ambazo ni hewa, hata kama kuna miradi mingi ya umeme inayojengwa lakini si sababu ya kutuweka gizani kwani hii ni nchi ina sheria zake, ina mipango yake na inawatu wake wanaolipa kodi nikiwemo namimi.
 
Taarifa zisizo rasmi kutoka chanzo chetu cha Uhakika mjini Dodoma zinatuaarifu ya kuwa mjadala wa kuinusuru Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini bado wajumbe wanakinzana kwa lipi hasa liwe azimio la jumla.Kundi moja linaafiki kufumba macho kupitisha Bajeti hiyo kwa mabadilishano na Nafasi ya Ngeleja, Yaani Ondoka tupitishe Bajeti yako. Walau ukijiuzuru tutapoza hasira za watanzania.Upande mwingine haukubaliani na Njia hii Mbadala ukiendelea kushikilia msimamo wa kutounga mkono Bajeti hiyo. Hatari ya kutopita kwa Bajeti ni kuvunjwa kwa Kikao cha Bunge linaloendelea kwa Mujibu wa Kanuni na kuandaliwa Bajeti mpya. Jambo ambalo kundi la awali linalitazama kama litakuwa matumizi mabaya ya fedha katika kipindi hiki ambacho Uchumi wa Taifa unazidi kudorora.Yote haya yanaendelea huku shauku kubwa ya watanzania ni kuona nishati ya Umeme wa Uhakika unapatikana.Tunapanga silaha zote mapema kufuatilia Mjadala LIVE kutoka Mjengoni.Stay OnlineADIOS
Mkuu tunashukuru kwa taarifa na la msingi plz utujuze lolote litakalojili hapa Dom tulipo wengine
 
Ngeleja hawezi kukwepa lawama hata kama mfumo ni mbovu. Mbona Magufuli anaonekana kupambana ndani ya mfumo huo mbovu? Nani asiekummbuka saga ya Mrema wa Tanroads? Shukuru Kawambwa alionekana kama mtoto kwa huyu Bwana, lakini it took Magufuli weeks to show him the door! Na kama kweli Ngeleja ni mchapa kazi basi wabadilishane wizara na Magufuli kama hautasikia bei ya kujenga barabara (per km) inapanda mara dufu!

Hapo ndipo penye shida sasa. Kama kuna system inayofanya vizuri hatutegemei mtu mmoja mmoja kupambana kivyake. Ni vyerma system ikawa inafanya kazi. Mkuu system haiwezi kumtegemea mtu mmoja; kam ni hivyo hiyo si system tena! Sijui kama magufuli atafanya vizuri kwenye barabara kama wakati wa Mkapa.
 
Taarifa zisizo rasmi kutoka chanzo chetu cha Uhakika mjini Dodoma zinatuaarifu ya kuwa mjadala wa kuinusuru Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini bado wajumbe wanakinzana kwa lipi hasa liwe azimio la jumla.
Jambo ambalo kundi la awali linalitazama kama litakuwa matumizi mabaya ya fedha katika kipindi hiki ambacho Uchumi wa Taifa unazidi kudorora.

Nadhani hawajui maana ya matumizi mabaya ya fedha....kupitisha bajeti ya hovyo na kurudi kwenda kujipanga kizuri kiipi? kweli hawa ni vichwa maji..............haya ujuze mwaya Mpwa
 
Moja ya vitu ambavyo vita tia doa Legacy ya JK ni hii wiazara ya Nishati na Madini. Tangu 2005, watu wamechaguliwa kuongoza hii wizara siyo kwa ajili ya competence bali zaidi ni kiurafiki. Kuanzia Msabaha, Karamagi, na Ngeleja plus Malima.
Kwa miaka hii iliyobaki itabidi kuweka watu wachapa kazi na ingependeza angewashirikisha wapinzani katika hili (kwa manufaa ya Taifa). Siyo wizara hii peke yake. Angefanya hivyo pia kwa wizara ya uchukuzi.
Ikishindikana kabisa tulete expartriates.
 
Nadhan IPTL ndo iliyokuja kuharibu kila kitu na mambo ya mipango ya muda mfupi nayo yameharibu sana, kama umeme wa maji umeshakuwa ni tatizo, kiwira si kuna makaa ya mawe, kule singida kuna upepo wa kufa mtu hata na jua nalo lipo sana nchini achilia mbali gesi ambayo wawekezaji walivyojimilikisha.

Hapa serikali inatakiwa ifanye kitu, wazungu wanasema it has to do something, Mimi ningekuwa nahusika na bajeti ya serikali kwa muda wa miaka miwili hadi mitano vipaumbale ingekuwa ni umeme na miundo mbinu halafu baadaye ndo tunarudi kwenye mambo yetu ya kila siku kama elimu, afya, chakula na maji.
 
Nitashangaa sana kama magamba wataikataa bajeti ya Nishati. Watajibaraguza huku na kule ili waonekane kama vile wameweka maslahi ya nchi mbele lakini mwisho wa siku bajeti hiyo itapita kiulaini na Mawaziri Wachovu Ngeleja na Malima kuendelea kupeta pale Nishati huku nchi ikiendelea kuwa gizani.
 
Mkuu nimekuelewa vyema. Kwangu mimi nadhani hili suala la mgao si suala la Ngeleja ni suala la serikali nzima. Mkuu kama unapangiwa budget kidogo ukiwa kama Waziri utafanyaje labda upate safari za nje ili ukawaombe wakubwa wakupe misaada kinyume na hapo hata ukipewa wewe sasa hivi hiyo wizara tutakupiga madongo tu!! Vipa umbele vya serikali inabidi vibadilike ili serikali iwekeze kwenye umeme na kulimaliza hili tatizo vinginevyo kila waziri wa nishati atapata joto ya jiwe kama Ngeleja. Najua Ngeleja ana mapungufu yake lakini kwenye umeme mimi naona kama anabebeshwa mzigo ambao si wake!
Kwanza kuna tatizo between Wizara yenye na TANESCO leo hii nenda Wizarani ukiwa na idea ya kuondoa tatioz la umeme kama watakusikiliza hii kitu inafanywa na deal na Ngeleja hawezi kusema kuwa hajui whats going ndio maana anaendelea kukaa kwenye huo uwaziri peacefuly angekuwa Waziri ambaye anajua uwajibikaji ungekuta ameishajiuzulu badala ya kuendelea kupiga blah blah sijui hata kama ukienda Wizarani leo ukaomba short term and long term plan sijui kama ipo on board zaidi ya kusikia wanayaongea mdomoni tu.

Mimi sidhani kama Tanzania tuna tatizo la mgao wa umeme, kila siku mara Tanesco wameleta majenereta halafu unaambiwa eti genereta litaanza kufanya kazi by next year hilo genereta ni la aina gani??? Imefikia wakati sasa tuseme enough is enough haiwezekani nchi tokea mwaka 91 tuna matatizo ya umeme halafu mkuu wa nchi akiulizwa anatoa majibu mepesi eti "It's mother nature" Sudan na nchi nyingine za kiarabu watasemaje wakati hawatumii vyanzo vya maji kupata umeme.

Vitu vingine vinatia hasira sana mtu ukiendelea kuongea kila siku mtu una incur huge operational cost kwenye mafuta ku-run business wao wako busy wanapiga propaganda
 
Nadhani hawajui maana ya matumizi mabaya ya fedha....kupitisha bajeti ya hovyo na kurudi kwenda kujipanga kizuri kipya? kweli hawa ni vichwa maji..............haya ujuze mwaya Mpwa

Wakishavuruga ndio wanatambua kumbe huwa na matumizi yapo, ila wakati wa kufuja huwa hakuna sala Mtume
 
Hakikisha outlook ya simu yako ipo configured tp JF Mobile...Tutaleta yote muhimu yanayotokea huko...Yupo na kiungo Buchnan

Sawa mkuu sa hivi nachaji tu simu yangu ili hata wakichukua umeme wao nitakupata kupitia JF mobile.
 
Back
Top Bottom