Nishati na madini Count down: Maamuzi mazito yanakuja

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Taarifa zisizo rasmi kutoka chanzo chetu cha Uhakika mjini Dodoma zinatuaarifu ya kuwa mjadala wa kuinusuru Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini bado wajumbe wanakinzana kwa lipi hasa liwe azimio la jumla.

Kundi moja linaafiki kufumba macho kupitisha Bajeti hiyo kwa mabadilishano na Nafasi ya Ngeleja, Yaani Ondoka tupitishe Bajeti yako. Walau ukijiuzuru tutapoza hasira za watanzania.

Upande mwingine haukubaliani na Njia hii Mbadala ukiendelea kushikilia msimamo wa kutounga mkono Bajeti hiyo. Hatari ya kutopita kwa Bajeti ni kuvunjwa kwa Kikao cha Bunge linaloendelea kwa Mujibu wa Kanuni na kuandaliwa Bajeti mpya. Jambo ambalo kundi la awali linalitazama kama litakuwa matumizi mabaya ya fedha katika kipindi hiki ambacho Uchumi wa Taifa unazidi kudorora.

Yote haya yanaendelea huku shauku kubwa ya watanzania ni kuona nishati ya Umeme wa Uhakika unapatikana.

Tunapanga silaha zote mapema kufuatilia Mjadala LIVE kutoka Mjengoni.

Stay Online

ADIOS
 
hapa CCM imefikia patamu sana, ngoja tuwapime hawa watu kama wana nia kweli ya kujivua Magamba -- hili la ngereja ndiyo GAMBA KUU - LIVUENI tuone.
 
Bajeti ya jumla ilishapita,hii ya ngeleja haiwezisababisha kikao/bunge kuvunjwa period
 
thankx mkuu, tunasubiri mambo ya mjengoni leo kwa hamu kubwa! ngereja aache utoto, abwage tu manyanga!!
 
Kwa ccm kuonesha (walau kama gesture) kutambua tatizo la umeme ni vizuri kwanza wamtose Ngeleja! Hakuna mtu mwenye imani na huyu Waziri.

Kwa wanaojua, nini kitatokea kama bajeti ya Wizara itakataliwa?
 
Kwa ccm kuonesha (walau lama gesture) kutambua tatizo la umeme ni vizuri kwanza wamtose Ngeleja! Hakuna mtu mwenye imani na huyu Waziri.

kwa mtizamo wangu ngeleja sio tatizo. uozo ameukuta. kawa wanataka kuwin watu, wasafishe kuanzia mwanzo wa tatizo. ngeleja kujiuzulu haitajibu matatizo ya umeme
 
Mkuu nafikiri hizi wanazofanya ni mbwembwe tu ili watanzania waone kuwa walikuwa wanahangahika kufanya maamuzi mazito kumbe wapi, mimi sioni ugumu uliopo hapo zaidi ya wabunge kujifanya wako kwenye wakati mgumu wakati ni jambo ambalo linawezekana ndiyo yale yale badala ya kuangalia maslahi ya taifa wanaangali maslahi wa Waziri wa Wizara husika na Wizara yake, pure total lack of accountability.
 
Naona kijana Makamba anaivizia hiyo nafasi kwa kasi!! Lakini cha msingi hapa wizara nyingi hazikuwa na nafasi ya kupitishiwa budget lakini kwa sababu umeme unagusa sana kila mtu tena kila dakika moja basi ndo maana tunaona hii wizara kimeo.

Msukuma mwenzangu ajiuzuru, wizara nayo isafishe uozo wote, hata kama ni kuniita mimi waniite nitapiga kazi na huo mgao utakuwa historia.
 
wasipitishe hata kama anajiuzulu,tumechoka

Jamani twende mbele turudi nyuma: Mimi binafsi nachukia sana nchi kuwa gizani lakini mbona Ngeleja anakuwa mbuzi wa kafara? Hivi kosa la Ngeleja ni lipi? Ni kwamba hashauri vizuri au ni kwamba nchi haina pesa za kuwekeza kwenye umeme? Hivi hili ni suala la Ngeleja binafsi au ni suala la Serikali nzima?
 
Mkuu nafikiri hizi wanazofanya ni mbwembwe tu ili watanzania waone kuwa walikuwa wanahangahika kufanya maamuzi mazito kumbe wapi, mimi sioni ugumu uliopo hapo zaidi ya wabunge kujifanya wako kwenye wakati mgumu wakati ni jambo ambalo linawezekana ndiyo yale yale badala ya kuangalia maslahi ya taifa wanaangali maslahi wa Waziri wa Wizara husika na Wizara yake, pure total lack of accountability.

Ubaya hapa ni siasa za Jukwaa zaidi, Ukweli uwajibikaji haupo. Unasoma upepo ukikaa vizuri unalalia huko huko ila leo ni kipimo chao japo najua majibu mepesi kama yale ya PM kwa maswali mazito ni kawaida.
 
kwa mtizamo wangu ngeleja sio tatizo. uozo ameukuta. kawa wanataka kuwin watu, wasafishe kuanzia mwanzo wa tatizo. ngeleja kujiuzulu haitajibu matatizo ya umeme
Yeye ndio Waziri mwenye dhamana na aliyepewa jukumu kwenye Wizara ya Nishati na Madini kama yeye hana majibu nani mwenye majibu? Au ndio huyo mkuu aliyemuweka madarakani??? Kujiuzulu maana yake ume-accept responsibility ni bora kuiuzulu kuliko kuendelea kukaa unapigiwa kelele usiku kucha halafu unadanganya watu mara JITIHADA mara UPEMBUZI YAKINIFU mara TUNAJITAHIDI mara MIPANGO ENDELEVU
 
Jamani twende mbele turudi nyuma: Mimi binafsi nachukia sana nchi kuwa gizani lakini mbona Ngeleja anakuwa mbuzi wa kafara? Hivi kosa la Ngeleja ni lipi? Ni kwamba hashauri vizuri au ni kwamba nchi haina pesa za kuwekeza kwenye umeme? Hivi hili ni suala la Ngeleja binafsi au ni suala la Serikali nzima?

Ukisoma vizuri ile thread ya Mwanakijiji inaendorse mtazamo wako Mkuu hapa kuna mushkeli
 
Ubaya hapa ni siasa za Jukwaa zaidi, Ukweli uwajibikaji haupo. Unasoma upepo ukikaa vizuri unalalia huko huko ila leo ni kipimo chao japo najua majibu mepesi kama yale ya PM kwa maswali mazito ni kawaida.
Halafu jinsi watu walivyo na high expectation utashangaa inakuwa vice versa bajeti hiyo inapita Waziri huyo anaenda zake kujipongeza tunabakia kusema tu wabunge wa CCM wajinga
 
Taarifa zisizo rasmi kutoka chanzo chetu cha Uhakika mjini Dodoma zinatuaarifu ya kuwa mjadala wa kuinusuru Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini bado wajumbe wanakinzana kwa lipi hasa liwe azimio la jumla.

Kundi moja linaafiki kufumba macho kupitisha Bajeti hiyo kwa mabadilishano na Nafasi ya Ngeleja, Yaani Ondoka tupitishe Bajeti yako. Walau ukijiuzuru tutapoza hasira za watanzania.

Upande mwingine haukubaliani na Njia hii Mbadala ukiendelea kushikilia msimamo wa kutounga mkono Bajeti hiyo. Hatari ya kutopita kwa Bajeti ni kuvunjwa kwa Kikao cha Bunge linaloendelea kwa Mujibu wa Kanuni na kuandaliwa Bajeti mpya. Jambo ambalo kundi la awali linalitazama kama litakuwa matumizi mabaya ya fedha katika kipindi hiki ambacho Uchumi wa Taifa unzidi kudorora.

Yote haya yanaendelea huku shauku kubwa ya watanzania ni kuona nishati ya Umeme wa Uhakika unapatikana.

Tunapanga silaha zote mapema kufuatilia Mjadala LIVE kutoka Mjengoni.

Stay Online

ADIOS

Changanya na hii:

Tunataka Gold itunufaishe. Hizi opportunities tsizikilize tu kwenye bomba, ni za kweli. Hata mfumuko wa bei ya mafuta umebadilisha kabisa Middle East. Kwa nini tushindwe kutumia resources zetu kama Gold?
Nawasilisha:

Destitute and yet we have lots of resources. Read this:-
•Gold prices rallied to record highs above $1,600 an ounce in Europe on Monday as investors spooked by the euro zone debt crisis and the threat of a U.S. default bought into the metal as a haven from risk.

•Data from U.S. futures regulator the Commodity Futures Trading Commission showed on Friday that managed money sharply raised bullish bets in U.S. gold futures and options in the week ended July 12 as bullion prices rallied.

•Stock markets fell in Europe as bank stocks came under pressure after capital stress tests failed to dispel fears about the regional debt crisis.

"The stress test result was met with a lukewarm response with focus again switching back to Europe. When that happens gold is often allowed to perform despite the dollar strengthening at the same time," said Hansen.
Sovereign default fears are growing in both Europe and the United States. The United States is struggling with deficit reduction talks ahead of the White House's July 22 deadline on a deal to raise the $14.3 trillion debt ceiling.

On the foreign exchange markets, the euro slid 0.8 percent against the dollar. Sovereign debt worries led investors to shift funds into safe-haven currencies like the Swiss franc and cut exposure to riskier assets.

Gold rallied across a number of major currencies, also hitting record highs in euro, sterling, South African rand and Canadian dollar terms.
"Investors are increasingly looking to gold as a safe haven as the U.S. dollar, pound sterling and the euro continue to devalue against stronger currencies such as those of Canada, Australia, Norway and Switzerland,"
Source: Reuters
 
Back
Top Bottom