mimi ni msichana nina 26
years, nina boyfriend wangu tumeanzana tokea chuo lakini huwa haonekani
kunijali ananitafuta akiwa na shida zake za............, nilimsemaga
akajirekebisha kidogo, badae tukawa tunaongelea mipango ya ndoa na
akasema ataenda kuongea kwao, alirudi ananiambia kwamba mama yake
anataka mtu wa kabila lake (mkurya) lakini anasema yeye ananipenda
nisihofu nisubirie labda mama yake atabadilika. Msimamo wake kutwa ni
visingizio mama anaumwa, sijui kazi anatoka usiku, simu yenyewe napigiwa
jumamosi akiwa na shida hata sielewi na ananigagania eti nisimwache na
hataki hata niwe na mtu ananifatilia kweli. Naombeni ushauri je huyu mtu
ananipenda hajui kuonyesha mapenzi au ananipotezea mda, na suala la
mama kweli anaweza kubadilika au changa la macho?