Nisaidieni

Dena Amsi

R I P
Aug 17, 2010
13,082
4,260
Huwa najiuliza mara nyingi kuwa ki au vi hutumika kwa vitu kama sikosei maana mimi si mtaalamu wa lugha, lakini linakuja swali langu kwanini walemavu wanatumiwa na maneno kama wao ni vitu?

Mfano: Kipofu, kilema, kiziwi - vipofu, vilema, viziwi nk

Inamaana wao ni vitu???

Wataalaamu nisaidieni hapa
 
Haya mambo ya ngeli nimeshayasahau, ila kwa kwa kumbukumbu kidogo nadhani zipo dhana mbili kuhusu Ngeli.. Utaweza kujua tofauti ya vitu na watu (viumbe hai) kwa kuangalia mifano yangu inayofuata.

Kipofu, kiziwi, (kijana pia) - Amekula, anacheza, ameanguka -- watu (ngeli ya KI-A)
Kiti, kiberiti - kimeanguka, kimepotea--- vitu (ngeli ya KI-KI)

Vipofu, vijana - wanakula, wanacheza, wanaanguka --- (Ngeli ya VI - WA)
Viti, Viberiti - Vimeanguka, vimepotea (ngeli ya VI-VI)

Ukitazama utaona kuwa hata neno -kijana, vijana- linaingia katika kundi la vipofu na viziwi, naamini yapo maneno mengine ambayo yanaingia hapo pia..
Wataalamu wa lugha watafafanua zaidi.
 
Huwa haiangaliwi upatanisho wa maneno tu KI-VI bali neno lenyewe.
Matumizi yake:
Umoja na wingi wa KI-VI unahusu vitu tu ikiwa neno limeanza na KIti au CHumba
Mifano
1. KI-VI kwa vitu kama vile kiti kimevunjika /viti vimevunjika
2. Chumba kimepakwa rangi /Vyumba vimepakwa rangi
Ikiwa neno linahusu binadamu, wanyama na wadudu, upatanisho unakuwa A-umoja/ WA- wingi hata kama neno litaanza na KI.
Mifano:
Kipofu amepotea njia/ vipofu wametoa njia
Ki pepeo anaruka/ Vipepeo wanaruka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom