Nisaidieni tafsiri ya ndoto hii

mr brocken

Senior Member
Apr 2, 2015
166
48
Usiku wa kuamkia leo niliota ndoto inayohusiana na uchaguzi mkuu inchini Burundi, picha ilianza ivi nilipata safari ya kikazi inchini burundi na nilitakiwa kuripoti kazini huko siku kadhaa baada ya uchaguzi mkuu wa urais, sasa nikiwa safarini nilifanikiwa kuingia inchini Burundi na kupata nyumba ya kulala wageni mjini Bujumbura lakini nikiwa kwenye nyumba ya kulala wageni nikiwa natua tu begi langu chini nikasikia mlio mkubwa sana unaofanana na bomu, nikajisogeza dirishaji na kuchungulia nje, dah nilichokiona kinasikitisha sana, watu wengi wanakimbia ovyo wengine wanaenda kusini, kaskazini, mashariki, na wengine wanagongana ovyo, watu wengine wamelala mabarabarani sijui kama ni wazima au ni wafu, wamama wanakimbia ovyo wengine wakiita majina ya watoto wao, mara nikaona makundi makubwa ya watu wakiwa wamevaa vinyogo usoni wakiwa wameshika silaha za kienyeji, watoto wa shule wanakimbia ovyo wengine wako kwenye mifereji ya barabarani yaani hali inatisha sana,mwisho kabisa nikamuona marehemu baba wa taifa la tanzania ametokezea kwa juu akiwa amewabeba watu wengi nami nikamrukia tukaanza kupaa angani wakati huo huo nikamuona baba wa taifa anamnyoshea kidole rais Pierre na watu wengine waliovalia suti nyeusi, na upande mungine kuna watu wengine wakiwa wameshika mawe na nagongo na upande mungine kuna watu wameshika silaha za kisasa, na tukiwa bado angani nikamuuliza baba wa taifa la tanzania ivi nini kimetokea, akaniambia hizi fujo au vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyosababishwa na tume ya uchaguzi kushindwa kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa siku zilizopangiliwa wakati huo huo rais pierre akiwa anafanya maandalizi kujitangaza mshindi.... .
Sasa leo kutwa mzima nilikuwa naitafakari ndoto hii, na kupata majibu kazaa moja wapo likiwa ni kumbe vita nyingi zinazotokea hapa duniani zinasababishwa na wana siasa,
Sasa wewe mwezangu umejifunza nini kutokana na ndoto yangu hii
 
Back
Top Bottom