Nisaidieni kumuokoa mke wangu mtarajiwa

Grader

JF-Expert Member
Feb 23, 2009
445
64
Ndugu zangu,nawaomba mnisaidie kwani mke wangu mtarajiwa siyo muaminifu kwani anazini hovyo na watu kila anavyoona yeye sijui nifanyeje?
1. yeye anafundisha kwenye shule moja huko Tabora na mimi nafanya kazi kwenye kampuni ya ujenzi Dar.
2. Namsaidia kila kitu ikiwa pamoja na wazazi wake pia LAKINI kweli kunguru hafugiki na kila kukicha anaendeleza dozi ya wanaume.
3. Wakati wa likizo ndiyo kubwa zaidi amenidanganya anakuja huku Dar,kumbe amekwenda kwa mwanaume mwingine.
4. Bibi yake anamjua huyo jamaa mwingine anamfichia.
5. Ndugu zangu nitaongea mengi LAKINI moyo unaniuma hali ambapo nimempenda mtu lakini ananifanyia hivyo hali ambapo nimegharamia hela nyingi kwenye mahali pekee ni Tsh 1,200,000/-
 
yan hapo wala huhitaj ushauri,Ukikumbuka UKIMWI upo na unaua then jibu utalijua
 
Ndugu zangu,nawaomba mnisaidie kwani mke wangu mtarajiwa siyo muaminifu kwani anazini hovyo na watu kila anavyoona yeye sijui nifanyeje?
1. yeye anafundisha kwenye shule moja huko Tabora na mimi nafanya kazi kwenye kampuni ya ujenzi Dar.
2. Namsaidia kila kitu ikiwa pamoja na wazazi wake pia LAKINI kweli kunguru hafugiki na kila kukicha anaendeleza dozi ya wanaume.
3. Wakati wa likizo ndiyo kubwa zaidi amenidanganya anakuja huku Dar,kumbe amekwenda kwa mwanaume mwingine.
4. Bibi yake anamjua huyo jamaa mwingine anamfichia.
5. Ndugu zangu nitaongea mengi LAKINI moyo unaniuma hali ambapo nimempenda mtu lakini ananifanyia hivyo hali ambapo nimegharamia hela nyingi kwenye mahali pekee ni Tsh 1,200,000/-

Grader pole saana kaka... Kweli umependa... Na wewe hapo ullipo hapo sidhani kama hata waweza kubali ushauri... Kwa muktadha wa kufahamu yooote hayo nilo weka blue bado unataka ushauri na bado umejiandaa kutoa mahari ya 1.2... We kaka wewe Mwanaume wa wapi? Dah! Kweli Umejaliwa roho nzuri.... Naomba elezea... Unataka ushauri wa kumbadilisha tabia ama wa jinsi ya kuvumilia? Maani ni dhahiri mpango wa kumuoa uko pale pale.... Na take note: Lazima atakuendesha hivo just brace yourself.
 
1,200,000 ni ndogo sana kushinda uhai wako pamoja na uthamani wako, huwezi kuishi na kicheche hata siku moja ukawa na amani moyoni, hapa piga chini uanze maisha mapya wanawake wako wengi tena wenye heshima na adabu, kumbuka tabia ni sawa ngozi kuibadilisha sio kitu rahisi
 
Pole kaka, mapenzi sio mateso. Anayekupenda hawezi kukufanya usononeneke na kukosa raha. Chukua hatua.
 
Ushauri juu ya hatua za kuchukua umepata, sasa umeshamtumia sms kuwa umemwacha rasmi???
 
Paka mapepe huyu hakufai, pesa inatafutwa sio uhai asikulete maradhi,shukuru mungu umemjua mapema, usisikitike wapo wengi wasio kua na dhiki za roho kama za huyu ....
 
  • Thanks
Reactions: Sal
hakuna wanawake wengine...wambie wa kurudishie chako usepee 1.2 maishaa haya parefuuu
 
Pole kaka,wewe ni mwanaume wa aina yake huyo mwanamke atakuwa hakupendi atakuwa amekuweka kama kitega uchumi..
 
Unataka ushauri gani tena zaidi ya kumpiga chini???? Umeshayajua yote hayo tena unataka ushauri gani?? Fanya maamuzi we mwanaume sijui wa wapi???
 
Kaka kama hiyo one point two unaiona kubwa endelea nae halafu tutakuzika ndani ya mwaka huu unaomba ushauri wanini kwa kiruka njia kama huyo hebu muache haraka sana kabla hajakuletea magonjwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom