Mrs Patrick
Member
- Feb 2, 2012
- 13
- 0
nina rafiki yangu amekuja kuomba ushauri: ana mpenzi wake wana uhusiano wa mwaka mmoja. wanaishi mbalimbali, na tangu waanze uhusiano wameonana mara mbili tu ambayo ni mwezi wa kumi mwaka jana na mwezi wa kwanza mwaka huu.ila mwanzoni mwa uhusiano wao mkaka alikuwa anampigia simu sana, walikuwa wanachat pia. ila tatizo linakuja ni kwamba saiv yule mkaka kabadilika. mara ya mwisho wameonana ni january, na mpaka sasa hawajaonana. na hata walivyoonana alikuta message za wasichana wengine, ila huyo mkaka akasema hao wadada ndo wanamtaka.sasa rafiki yangu akimwambia waonane, mkaka anasema yupo busy na shule. saiv shule kamaliza lakini anatoa visingizio kibao. na pia mara nyingi hapatikani kwenye simu anasema sehemu aliyopo kuna shida ya umeme. sasa anashindwa kumuelewa mpenzi wake huyo, nimshauri vipi jamani.