Nipo Ubungo stendi narudi kijijini hali ya mgao wa umeme wa Ngeleja imenishinda!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Aheri nirudi kijijini vava segito de yani nikiendelea kuwepo hapa mjini mwishowe nitaozea segerea bureeeee kisa Ngeleja na genge lake la ccm fu****k Tanesco!!Makampuni yangu yanazidi kufilisika na wafanyakazi hawaelewi somo, hali ni mbaya vandugu!!
 
Salaam zao, waambie huko wabadilike vyama vingi si vita kama wanavyodhania.... pia waelimishe waondokane na usemi wa TANU....CCM ndo chama chetu kimetulea tuendelee kukitetea...... Usisahau kuwapelekea mikate na mandazi huko ni adimu... Bon Voyage.
 
Salaam zao, waambie huko wabadilike vyama vingi si vita kama wanavyodhania.... pia waelimishe waondokane na usemi wa TANU....CCM ndo chama chetu kimetulea tuendelee kukitetea...... Usisahau kuwapelekea mikate na mandazi huko ni adimu... Bon Voyage.
Nashukuru narudi ktk zama zamaisha yetu ya vikoroboi! Chakufurahisha zaidi nimefika kwenye basi yani nimejihisi kama nishafika kijiji vile yani hapa ni mwendo wa Kamwene be mnogage, hureeeeeee wacha nikafaidi life ya bush!!!!
 
Wewe maisha yamekushinda kwa ujumla wake, usitoe visingizio vya umeme.
 
vahungilage mbevali, lkn hiyo koroboi nayo balaa mafuta ya taa bei juu.
 
Nashukuru narudi ktk zama zamaisha yetu ya vikoroboi! Chakufurahisha zaidi nimefika kwenye basi yani nimejihisi kama nishafika kijiji vile yani hapa ni mwendo wa Kamwene be mnogage, hureeeeeee wacha nikafaidi life ya bush!!!!
mkuu umepanda Upendo au Budget?
 
Na bado...

CCM wakimaliza kututafuna mjini na huu mgawo upnext ni vijijini. Mtalima sana lakini sehemu ya kuuza mazao kwa bei nzuri hamtapata na mkitaka kuyauza kimagendo nje ya nchi mtakamatwa na kuitwa wahujumu uchumi wa nchi. Baada ya miaka miwili kijijini kutakuwa kugumu mtakuwa mnashindia maembe yaliyotiwa pilipili na maji meengi hadi wanenu vitumbo vitawatoka kwa kukosa lishe bora.

Baada ya hapo watakuja wawekezaji toka ulaya ambao watasema wamekuja kuingia ubia na watanzania kwa ajili ya kutekeleza sera mufilisi ya Kilimo Kwanza, mtawakatia maeneo makubwa ya ardhi yenu yenye rutuba wataleta vifaa vya kisasa na ubia wenu utakuwa kugeuzwa vibarua katika mashamba yao, watachapa sana zenu na kuwatia mimba na kama ilivyokuwa afrika ya kusini huko vijijini litaanza taifa jipya la colored people ambao sijui watajiita afrikaner au wanyalu-kana.

Mungu akutangulie kiongozi, maisha yakikushinda unakaribishwa mjini tena usione aibu tutabanana kwenye mabanda ya uwani Tandale.
 
Mkuu unapanda basi gani? Lupelo Trans? nataka kuja nikupe kufurushi umpelekee dingi yangu. Na mimi nakuja huko huko mwezi ujao, tutakuja kuongea zaidi kuhusu kilimo cha vitunguu nasikia vina siko sana Kenya. Vitunguu havitahitaji umeme wa ngeleja.
 
Mkuu unapanda basi gani? Lupelo Trans? nataka kuja nikupe kufurushi umpelekee dingi yangu. Na mimi nakuja mwezi huko huko mwezi ujao, tutakuja kuongea zaidi kuhusu kilimo cha vitunguu nasikia vina siko sana Kenya. Vitunguu havitahitaji umeme wa ngeleja.
Nipo morogoro mida hii nimepanda Luwinzo Express!
 
Bora ubaki mjini. huko uendako hali ni mbaya zaidi mkuu.
Nakushauri ubadilishe biashara. Anza biashara ya vibatari na mishumaa inalipa sana kwa sasa.
 
Wadhungu wanasema eti Waafrika daima tuko busy kurudi tulikotoka,yawezekana hata hili swala la umeme ni Juhudi za CCM kuturudisha tulikotoka
 
Back
Top Bottom