Nipo njia panda

.........
........Huyo wa miaka 26 nadhani hajatulia, hadi anataka kujishikisha mimba kwa ajili mje mfunge ndoa...........mhhhhhhh!! Mie ananitia mashaka mbona ana kihere here sana cha kuolewa?Ila mwenyewe umesema hapo ndipo moyo wako ulipo hivyo mkaka wewe mwenyewe chagua pumba na mchele hapo.

......Huyu wa 34 nahisi mtulivu japo umri umekwenda lakini hakupigii kelele za ndoa, na wewe ndio unamfahamu vizuri unasema hana makuu na anajiheshimu........umri sioni tatizo sana kama kweli umempenda, japo inapendeza mwanaume kumzidi mwanamke kiumri.Huyu wa 34 naona kama anafaa japo wewe naona kama humpendi kivileeeeeee!!

.

Wadada wazee waliojichelewesha huko utawajua tu kwa jinsi wanavyoteteana. Kijana mwenzangu nakushauri usioe ajuza huyo wa miaka 34, itakula kwako! Hapo menopause bado miaka 5 tu, mnaanza crisis ndani! Unapochukua kitu angalia na shelf-life yake bro.
 
Wa kuolewa ni huyo wa 26 bana, unataka jamaa aoe ajuza? Au nawe Belinda umeshajichelewea zako huko unatetea wazee wenzio ili hiyo kitu ionekane kawaida? No way. Huyo wa 34 asubiri wazee wenzie. Lakini jamaa ni kicheche siyo siri! Ni tabia mbaya hii aliyofanya.

Mtu B hapa issue si uajuza wa one of wadanganyikaz, issu e hapa ni huyu jamaa asiye muaminifu, asiyejielewa wala kujitambua anataka nini kwenye maisha yake.
mbele ya macho yangu hustahili kumuoa hata huyo binti wa 26 yrs..........jitafakari na ujue what do you exactly want in life.
mwisho wa siku unaweza ukawakosa wote kwa taarifa yako!!!
 
pole sana, ni kweli umejitakia hayo mwenyewe kwa kuwa na wapenzi wawili na kuwapa matumaini ya ndoa wote.

kwa maelezo yako huyo mchumba mkubwa ndie anaekufaa, na umeshampotezea muda mwingi na bahati nyingi kwani kama ulivyosema ametulia hana makuu anakusubiri wewe.

kwa upande mwingine huyu dogo inaelekea hukumpenda kwa dhati bali kwa umri wake mdogo atakua anakufanyia vile vitu ambavyo huyu mkubwa hajafanya au anakupagawisha ndio maana unafikiri umempenda sana. hebu jaribu kumwambia huko tayari kwa ndoa sasa hivi uone kama atakuwa nawe tena. tena mwambie sasa hivi kabla hajaja huko kuchukua mimba!

usichukue umri kama kisingizio, nina rafiki yangu ambae wazazi wake baba ni mdogo na mama ni mkubwa kiumri lakini ndoa yao ya miaka zaidi ya 40 natamani yangu ingekua na upendo au ustaarabu kama yao.

Mshirikishe Mungu katika maamuzi yako kwani mke mwema ni zawadi kutoka kwa Mungu. kila la kheri

Walewale! Usidanganyike kaka
 
na mambo kama haya yanapelekea kuchagua kucko kesho unakuja jutia maisha, tamaa zanawasumbua sana! hapo hata kama ni tamaa lakini ulitakiwa ucheze karata zako vizuri kwa kumwambia mmoja ukweli hata akiamua kuendelea na uhusiano lakini ajue hauna future.....anza moja au mwambie mmojawao ukweli.
 
]Wadada wazee waliojichelewesha huko utawajua tu kwa jinsi wanavyoteteana. Kijana mwenzangu nakushauri usioe ajuza huyo wa miaka 34, itakula kwako[/COLOR]! Hapo menopause bado miaka 5 tu, mnaanza crisis ndani! Unapochukua kitu angalia na shelf-life yake bro.

ndio mana mnashikwaga mackio, upeo wa baadhi yenu wa kuchagua mke ndio unawapelekaga pabaya!
 
Wadau naombeni ushauri wenu nipo njia panda,Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 29 sasa,nipo njia panda katika kutoa maaamuzi,nina wachumba wawili lakini sijui ni yupi nimchague awe mwenza wangu wa maisha, mmoja amenizidi umri yeye kwa sasa ana miaka 34.

Yeye tangu utotoni tulikuwa tunaishi jirani, tulizoeana sana kama kaka na dada na familia zetu zinajuana vizuri, kwa bahati nzuri mimi nilipokuwa masomoni nchini Africa ya kusini, na yeye pia alikuwa anafanya kazi nchini humo, kwa hiyo tukazidi kuwa marafiki, lakini mwaka 2007 tukajikuta tunaangukia kuwa wapenzi, kwa kweli tulipendana sana na kuzidi kuwa karibu sana, na kusema kweli huyo dada ni dada asiye na makuu na pia anajiheshimu sana,

Tuliendelea na mapenzi yetu mpaka mwaka 2008 mwishoni ambako mimi nilimaliza masomo yangu na yeye pia akawa anamaliza mkataba wake wa kufanya kazi nchini humo.wote tukarudi nyumbani Tanzania, lakini mimi mwanzoni wa 2009 nikapata nafasi ya kwenda USA kuendelea na masomo zaidi, na kumuacha yeye Tanzania kwa kuwa alikuwa anafanya kazi tayari.

Kwa bahati mbaya au sijui nzuri, nilipofika US kuna msichana mmoja ambaye alikuwa rafiki yangu high school Tanzania, mimi nilikuwa Shaban Robert na yeye alikuwa Mziziima , Yeye ana umri wa miaka 26.Alinipokea na kusema kweli huyo msichana nilimpenda sana tena sana tangu tulipokuwa high schoool japokuwa sikuwahi kumwambia,tukawa marafiki tena.

lakini katika huo urafiki wetu tukajikuta tunangukia kuwa wapenzi, kusema ukweli sijawahi kupenda kama ninavyompenda huyu msichana. na nakubali kuwa nilifanya kosa kubwa la kutomueleza ukweli kuwa mimi tanzania nimeacha mtu.

Lakini mwishoni wa 2009 yeye alimaliza shule na wazazi wake wakamtafutia kazi Tanzania kwa hiyo ikambidi aniache mimi nikimaliza masomo na yeye kurudi Tanzania, kwa matumaini ya kuwa nikimaliza na mimi nitarudi Tanzania tufunge pingu za maisha.Hapo ndio tatizo linapokuja, wote wawili wananisubiri nirudi, japokuwa yule wa kwanza haijawahi pita siku bila kunipigia simu, na pia najua ananipenda sana lakini naogopa naona amenizidi sana umri inaweza kuleta matatizo hapo baadaye.

Japokuwa yeye tunajuana vizuri sana nje ndani, na anajiheshimu sana tena sana na hata mama yake anajua mimi ndie mchumba wake pia uwa ananipigia simu naongea na mama yake pia , Lakini mimi nampenda sana huyu wa pili japokuwa huyu wa pili yeye inaweza pita hata siku tatu hajanipigia simu wala messegi, na pia naona kama yuko desperate sana na kuolewa, maana anataka kufanya mambo kwa haraka sana, mpaka nakuwa nahisi anaweza pata mtu huko nyumbani ambaye tayari ameshasettle akamuoa.

japokuwa naye mama yake ananijua mimi ndie mchumba wake na hata dada yake na kaka yake wanajua hilo,nilikuwa niiende tanzania likizo mwezi huu lakini nimearisha kwa kuogopa itakuwaje nikifika Tanzania maana wote wananisubiri, na huyu wa pili alitaka sana nije eti anitambulishe kwa wazazi wake na mimi nimtambulishe kwa ndugu zangu, hapo ndio roho yake itatulia maana kwa sasa hana uhakika kama mimi ni wake kweli.

Na juzi huyu wa pili kanipigia simu anasema kwa kuwa siendi Tanzania yeye atakuja huku US mwezi wa tisa ili eti nimpe mimba then tuwe na kitu ambacho kitatufanya tuwe pamoja.Na yule dada wa kwanza naye anataka kuja huku x-mas japokuwa yeye ajasema kama anataka mimba au lah ila nahisi naye ni hilo hilo anataka, sasa hapo ndio maisha yangu yanapokuwa magumu mpaka nakosa raha naombeni sana ushauri wenu wadau tafadhari japokuwa najua mimi ndie nimejitakia yote hayo lakini naombeni ushauri, yupi ananifaa kati ya hao nichukue uamuzi?​

Si muoaji wewe bado.. mihemko na woga wa kukabiliana na matatizo ulojisababishia ndio yakusumbua broda..JITAMBUE KWANZA... jiulize unahitaji mkeo wa maisha aweje..jiangalie unaweza kuwa mume bora kwa mwanamke wa aina ipi.. angalia hao wenzi wako kila mmoja TBS zake kwa vigezo uivojiwekea na hatimaye uchukue maamuzi magumu ya kumchagua mmoja na kumtosa mwingine... Itz ur mess.. clean it!!:pound:
 
If you want to be happy in your marriage, you must do justice to your heart just now & marry the women you truely love. I had the same problem, my xGF was 2 years older than me, almost everybody, including some church elders adviced me to leave her, all I had to do was to find a good reason to leave her without hurting her so much. Currently, you cant foresee what will happen when your wife gets old, lets say she is 45yrs & you are 40yrs, most males at this age are the ruthless fatakis in the current generation .i.e. most sexually active than their counterpart females. Am sorry ladies if you will be offended by this, I repeat, do justice to your dear heart gentleman & marry your dream woman.
 
huna uaminifu wa mapenzi, kwani ulipokuwa unaenda usa kimasomo tayari
mlikuwa mmesitisha mkataba wa mapenzi na huyo mpenzi wako wa kwanza?

umekutana na huyo ulokuwa unasoma naye sekondari umemsahau ulokutana
naye A. Kusini

utakutana na uliyekuwa unasoma naye shule ya msingi ulimpenda sana
ingawa hukuwahi kumwambia na utakuja hapa tena kuomnba ushauri,
inaonekana kuwa hiyo ni tabia yako tu, hebu jaribu kuwa mtulivu katika
swala mahusiano, maana kusafiri huwa hakuishi, utajaenda mahari pengine
utakutana na mwingi, tabia ikizoeleka inakuwa sehemu ya maisha yako
kuwa makini sana na hili
 
g'mrng dearest!...hope upo bien..naona watu wanatafuta wacumba kama wanachagua nyanya vile.

inasikitisha.......mi chichemi wala chiongei!!! hivi hili soko la EA si limegusa hata sekta hii??
 
Walewale! Usidanganyike kaka

Wadada wazee waliojichelewesha huko utawajua tu kwa jinsi wanavyoteteana. Kijana mwenzangu nakushauri usioe ajuza huyo wa miaka 34, itakula kwako! Hapo menopause bado miaka 5 tu, mnaanza crisis ndani! Unapochukua kitu angalia na shelf-life yake bro.
Mafataki utawajua tu! una uhakika gani kuwa hawa wadada wanaotoa ushauri ni wazee waliojichelewesha.
Uzuri ni kwamba hakuna mtu atakayeishi maisha ya mwenzie.Endeleeni na 'ujana' wa kipumbavu lakini apandacho mtu ndicho atakachovuna!
What goes around comes around!
 
Sijajua wakati unafanya hayo ulikuwa unawaza nini hatima yake ...umeyakoroga
Cha msingi hapo ni wewe na moyo wako ndio mwamuzi tunaweza kuongea mengi na kuandika page zaidi ya kumi mwisho wa siku uamuzi wako ndio muhimu katika future yako.
Katika uchaguzi wako usiangalie umri kuna watu wanajipenda sana unamkuta ana 40 yrs ukadhani 30 ni mambo ya kujimake tu.
Ila hako katoto ka 26 kanakotaka mimba kabla ya ndoa kana hatari kweli.
1. Ni dhambi kwa mungu
2. Kakibeba hiyo mimba kisha usikaoe itakuwaje ?
Kuwa muwazi na mkweli kwa hao kina dada
Piga magoti mshirikishe mungu wako jibu utalipata .....

Sikujua kama wapo wengi hivi! Ushauri wa kuoa ajuza ni wa kuuogopa kama ukoma na ukimwi!

Huyo wa 26 hata kama anataka mimba ni haki yake, ndio wakati wake. Huyo wa 34 hata ukimpa hiyo mimba atakwenda kiliniki na labour akiwa 35 akakutane na wa miaka 20 mbona aibu! Halafu hapo ni kama ana bahati ya kuipata hiyo mimba. Na wataalamu wanatuambia umri unaofaa kupata mimba usizidi 35, sasa niambie kaka unataka kuchukua kitu siku ya expiry date?

Hapa ni oldies wanatetea oldies wenzao ili tuzoee tuone ni kawaida, lakini kamwe haifai. Ni sawa na gays wanavyojitahidi kutushawishi kuwa ndoa zao ni sahihi, na wanalisema mara nyingi na kupiga kelele sana ili baadae izoeleke na kukubalika kama ambavyo tumeona.

Ndoa baina ya kijana na ajuza haikubaliki, napinga kabisa. Hao wakaolewe na wazee wenzao wafarijiane kimtindo. Lakini kama ni suala la kumega tu, poa, lakini kuoa itakula kwako kaka.
 
Mafataki utawajua tu! una uhakika gani kuwa hawa wadada wanaotoa ushauri ni wazee waliojichelewesha.
Uzuri ni kwamba hakuna mtu atakayeishi maisha ya mwenzie.Endeleeni na 'ujana' wa kipumbavu lakini apandacho mtu ndicho atakachovuna!
What goes around comes around!
:biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1:
 
una umri gani bwana mdogo?...
naogopa sana kumshauri mtu ambae naamini atakuwa chini ya 25....!
 
Mkuu zimbo,

- Huwezi kuwa na "wachumba" wawili: uchumba ni 1o1 - ukishakuwa na zaidi ya mmoja hiyo inaitwa "profanity"

- Acha dhambi: fanya maamuzi sahihi: funga ndoa
 
Mafataki utawajua tu! una uhakika gani kuwa hawa wadada wanaotoa ushauri ni wazee waliojichelewesha.
Uzuri ni kwamba hakuna mtu atakayeishi maisha ya mwenzie.Endeleeni na 'ujana' wa kipumbavu lakini apandacho mtu ndicho atakachovuna!
What goes around comes around!

halafu mie ckujua 34 yrs tayari mtu umekuwa ajuza, mbona ninafanya kazi na wakaka wana 34 n above na hawajaoa nao ni maajuza au ina apply kwa wanawake tu?
 
Sikujua kama wapo wengi hivi! Ushauri wa kuoa ajuza ni wa kuuogopa kama ukoma na ukimwi!

Huyo wa 26 hata kama anataka mimba ni haki yake, ndio wakati wake. Huyo wa 34 hata ukimpa hiyo mimba atakwenda kiliniki na labour akiwa 35 akakutane na wa miaka 20 mbona aibu! Halafu hapo ni kama ana bahati ya kuipata hiyo mimba. Na wataalamu wanatuambia umri unaofaa kupata mimba usizidi 35, sasa niambie kaka unataka kuchukua kitu siku ya expiry date?

Hapa ni oldies wanatetea oldies wenzao ili tuzoee tuone ni kawaida, lakini kamwe haifai. Ni sawa na gays wanavyojitahidi kutushawishi kuwa ndoa zao ni sahihi, na wanalisema mara nyingi na kupiga kelele sana ili baadae izoeleke na kukubalika kama ambavyo tumeona.

Ndoa baina ya kijana na ajuza haikubaliki, napinga kabisa. Hao wakaolewe na wazee wenzao wafarijiane kimtindo. Lakini kama ni suala la kumega tu, poa, lakini kuoa itakula kwako kaka.
toa ushauri na si ku sahauri mtu kwa kutumia mawazo ya mtu binafsi, ikiwa umri mzuri kupata ujauzito ni miaka 35, unataka kuniambia kuwa wanawake wote wanaozaa wakiwa na umri wa miaka zaidi ya 35 wanafanya makosa? ama wanzaa mapoza? mbona wengine tumezaliwa mama zetu wakiwa ni watu wazima na hakuna athari zozote, ama wewe ulizaliwa na kibinti? na kama ulizaliwa na kibinti basi kilibakwa, maana usitake kuniambia binti aliyeolewa akiwa na miaka 26 na katika ndoa yake amebahatika kupata watoto 7 wote aliwa zaa under 38 to 35
 
Mkuu zimbo,

- Huwezi kuwa na "wachumba" wawili: uchumba ni 1o1 - ukishakuwa na zaidi ya mmoja hiyo inaitwa "profanity"

- Acha dhambi: fanya maamuzi sahihi: funga ndoa
mkuu nilitaka nikugongee thanx kile kitufe cjakiona, kikubwa ni kufanya maamuzi
yenye kukufanya uwe karibu na Mungu
 
Back
Top Bottom