Nipeni pole,wakaka/wababa nisaidien kujua 7bu ya baadhi yenu kufikia kufanya upuuzi

Pole mwaya, haya mambo yanakera asikwambie mtu! Mi mwenyewe niliwahi nusurika na hii kitu, tulikuwa tumesimama kwenye daladala na nyuma yangu alikuwepo huyo mbaba alotaka kunifanyia huo ubazazi. Yaani ka bahati ikatokea nikageuka, my dear nilibaki kuduwaa........!!
Asante mwaya,yani mm mwenyewe mbona nimebaki na mshangao wamaisha,yani nilikera ile picha inajirudia mawazo kila wakati,sijui hawa watu wanapatwa na nn?
 
dah pole sana cantalisia uwe unatembea hata na kiwembe ungemtoa hata sikio akome

Pole dia, hata mimi iliwahi kunitokea, sijui hata huwa wanamatatizo gani, msemo wa bebii ungekuwa na kiwembe ungemtahiri paleplae
 
Kuna case kama hizi nimeishawahi kuzisikia na kuziona, ingawa huwa nakaa najiuliza tatizo linakuwa ni nini hadi ufikie to that extent nafikiri kuna watu huwa wanahitaji kwenda kumuona Psychiatrist
 
Pole sana da Canta,...ila nafikiri huyo jamaa ni punguani,...amejidhalilisha na kutudhalilisha watu wa jinsia yake
Asante Igwe binafsi nahic km hana tatizo basi sijui tena mungu anajua kilicho akilin mwake!
 
yani kama amelala mzungu wa nne na mkewe ndo akuharibie siku asbhi yote iyo dear loh pole sana wanaume hawa khaaa........................
Asante Bebii,jaman si angemalizia hata bafuni wakati anaoga mambo gani yakuleteana mikosi asubuhi asubuhi!
 
Pole dia, hata mimi iliwahi kunitokea, sijui hata huwa wanamatatizo gani, msemo wa bebii ungekuwa na kiwembe ungemtahiri paleplae
Asante Ram,kwakweli nashukuru kwani mnanisaidia kuwaaminisha watu kuwa haya mambo yapo na watu wanatufanya!
 
Kuna case kama hizi nimeishawahi kuzisikia na kuziona, ingawa huwa nakaa najiuliza tatizo linakuwa ni nini hadi ufikie to that extent nafikiri kuna watu huwa wanahitaji kwenda kumuona Psychiatrist
Kwakweli hili linakera hasa anayekufanyia anaonekana ni mtu mwenye akili timamu,na mtu wa hivi sijui hiyo akili yake inaweza kuwaelewa hata hao wataalamu wa saikolojia!
 
Yeah_something is clicking in ma head!..inawezekana hivi vitu vipo na vinafanyika kwenye jamii yetu_maake naona watu wengi wanashuhudia,.....ila its more than inhuman...ngoja namuona naye Bebii anachungulia hapa chini alete ushuhuda wake na namna alivyo deal nalo,....poleni sana

Yaani IGWE hawa watu sijui wana roho gani. Hawaogopi wala hawana aibu. Kweli mtu mzima na akili yako unathubutu kufanya jambo la namna hiyo? Na izo zipu sijui zinafunguliwaga saa ngapi.
 
pole sana mpenzi, natamani ningekua humo kwenye daladala nisingemwachia hivihvi!!!
 
Habari zenu wadau,leo nimekuwa na asubuhi mbaya sana na hata itapelekea kuifanya siku yangu nzima ya leo kuwa mbaya,nikiwa njian nakuja kazini asubuhi kutokea mwenge kuja posta,nashukuru nilipata siti sio ya dirishan,gari ilikuwa imejaa sana watu wengi walikuwa wamesimama,pembeni yangu alikuwepo mbaba kwa kumkadiria ni km miaka 35-40 hivi alikuwa nadhifu na shati lake lilikuwa na jina la benki moja kubwa hapa mjini,yule baba kadri safari ilivyoendelea alizidi kunisogelea mpaka akawa ameegemea kile kiti na kunigusa kwenye bega la kushoto akiwa anatizama dirishan.

Kutokana na hali ya hewa ya leo ya mvua kulikuwa na folen sana tulipofika maeneo ya moroco nikawa nasinzia ila sio usingizi mzito,nikawa nahisi km kuna kitu kinanipapasa au km kusugua kwa mbali nikafumbua macho nikamwangalia yule baba naye akaniangalia nikawa sijaelewa kitu nikaendelea kulala,baada ya muda tena ile hali ikaanza nikisikilizia kwa muda nikiwa bado sijagundua kinachoendelea nikamtizama tena yule baba hakunitizama akawa anaangalia nje,nikendelea kulala ila nikiwa nasubiri ule msuguo uanze,na kweli haikupita mda ukaanza tena kwa nguvu na kwa kasi nikafumbua macho nakuangalia ile sehemu, yule baba alikuwa amefungua zipu ya suruali yake na anasugua uume wake kwenye mkono wangu kati ya kiwiko na bega,kwakweli nilishituka sana na yeye wala hakujua km nimemuona akaendelea na mchezo wake.

wandugu gafla sikujua nifanyeje nilipata hasira nikajikuta nimesimama gafla na kumchapa kofi kali yule baba kabla hasema kitu nikapiga na lingine akabaki amepigwa butwaa suruali iko wazi watu bado wanamshangaa mie nikamwita konda nakuomba asimamishe gari yule baba ndio akastuka na kukimbilia mlangoni akitashuka watu wakamzuia wakanza kumpiga wakizani ni mwizi na ameniibia nikawaambia sio mwizi msimpige akashuka huku akiwa anafunga suruali maeneo ya ubalozi, watu wakanza kuniuliza kwann nimempiga niliwaelezea kilichotokea walishangaa na baadhi kunilaumu kwann sikuacha wampige sikuweza kusema kitu nilinyamaza nikiwa na hasira kupita kiasi,

kwanza nipen pole balaa hili ambalo nimekuwa nikisikia story tu kwa watu na magazetini, na nawauliza wababa/wakaka ni kitu gani kiasababisha baadhi yao kufanya vitendo hivi,ni makusudi au ni hali inayowakuta bila kujitambua au nikuendekeza tamaa za kijinga?nawasilisha.
Pole sana Bi Cantalisia hayo ni mambo yakijinga yanafanywa na watu wajinga ktk jamii!!!!!!!!Ila kwa ushauri wangu usitoe nafasi kwa mtu kukufanyia vitu namna hiyo!!!!!!! Kila wakati uwe alert na mazingila yaliyo kuzunguka, chukua hatu haraka mtu yeyote akijabu kefeki situation, be very serious and sensitive to the saroundings!!!!!!! Don't dose in public busses or vehicles, u will be robbed!!!!!!
 
pole mwaya.....wanaume ndio zao siku hizi tena bora umetoa hii ili waone uvundo wao wanaoufanya kwenye magari
cz mi binafsi wk iliyopita nlipanda gari lililojaa sana wakt nakuja kazini asbh
si unajua mambo ya kusimama...nikawa nimesimama cha ajabu kuna kaka kila gari likiyumba bs ye yuko kwa nyuma yangu
yan yuko usawa wa makalio yangu heeeeeeeee minikaona anazidi nlichomwambia kaka naomba ujiheshimu hata kama gari liko full huwezi kuambatana na mm kiivo bwana........ndo kuondoka kwake
 
dah pole sana cantalisia uwe unatembea hata na kiwembe ungemtoa hata sikio akome

aaaaaaagrrrrrr weweeeeeeee wachaa wembe noumer hata kama ni azabu hiyo imepitiliza, dah nimesisimka ulivyotaja wen=mbe kwa maeneo nyeti kama hayo...

hii stori sidhani kama inaukweli kwa mtu kutoa dudu yake na kukuwekea kwenye mkono labda ni kichaa huyo. KAMA ni kweli basi pole sana next time mpe ngumi jiwe ya pua, vibao vya wanawake haviumi, ngumi ya pua ndo safi
 
Yaani IGWE hawa watu sijui wana roho gani. Hawaogopi wala hawana aibu. Kweli mtu mzima na akili yako unathubutu kufanya jambo la namna hiyo? Na izo zipu sijui zinafunguliwaga saa ngapi.

nafikiri wana roho ya shetani_wanaogopa lakn hawana aibu mkuu
 
Yeah_something is clicking in ma head!..inawezekana hivi vitu vipo na vinafanyika kwenye jamii yetu_maake naona watu wengi wanashuhudia,.....ila its more than inhuman...ngoja namuona naye Bebii anachungulia hapa chini alete ushuhuda wake na namna alivyo deal nalo,....poleni sana
Asante mkuu,hata mie naona ni tatizo hili limetukuta wengi sijui hii nayo ni fashen au ni ugonjwa mungu anajua!
 
pole sana mpenzi, natamani ningekua humo kwenye daladala nisingemwachia hivihvi!!!
Asante Mama D,ni kweli na ndio maana abiria wengine walianza kumpiga,wanawake tunakutwa na mengi jaman!
 
Back
Top Bottom