Nipeni majibu wanajamii - hili linapaswa lifahamike

We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
814
380
Wana jamii naomba mnipe majibu kwa haya yafuatayo baada ya paragraph ifuatayo:

Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana kwa muda mrefu sasa utendaji wa kazi wa vyombo vya usalama vya nchi hii, na hasa Jeshi la Polisi, ambalo ndilo lipo karibu au ndilo lenye dhamana ya ulinzi wa raia na mali zao. Naomba majibu kwa yafuatayo,

1. Hivi watu walioajiliwa ktk kazi ya upolisi si watanzani na hawana ndugu zao hapa Tanzania?

2. Hivi kazi ya Polisi ni kazi ambayo huhitaji kutumia akili zako kama binadamu halisi bali kufuata amri tu?

3. Ni Saikolojia gani inayofundishwa ktk kazi ya upolisi, ambayo inakufanya ukiwa polisi, uwakane ndugu na jamaa zako na kufanya mambo kama huna akili kabisa?

4. Hivi ni kweli ukiwa polisi mnatakiwa kumsikiliza mtu mmoja tu kati ya watu millioni 46? Kwa mfano mtu huyo mtu mmoja akiwaagiza polisi anzeni kuua watu, polisi inabidi wafanye hivyo bila kuchukua tahadhari?

5. Ikiwa kama huyo mtu wanayepokea maagizo yake ameaanza kupata Kichaa na kupoteza fahamu na kutoa amri za maangamizi, polisi watafuata tu, au wanahitaji kuchunguza kwanza?

6. Naomba mnijuze, kwani hayo niliyoyaeleza hapo juu, ndiyo yanafanywa na polisi wa Tanzania.
 
Nahisi baadhi yao hawakubaliani na hiyo hali bali kiapo ndo kinawafunga
 
Kifungo kitu gani? Ila najua sababu, polisi akivaa gwanda anajiona ndo mwisho na hakuna mtu mwenye nguvu kama yeye bila kufuikiria yeye ni kibaraka tu kwani wengi wanaojifanya kuwa na kiherehere hawna vyeo. ajira yao ipo hewani tu, na wakifukuzwa kazi wakirudi mtaaani wanapigika ile mbaya. Kwa ujumla mimi nawachukia sana polisi kwakuwa hawatumii akili, naweza kuwafananisha na simimizi. akishakuwa na bunduki basi anajiona ni mungu. Hivi hata Mwema ambaye amashafanya kazi au kwenda nchi za ulaya kiziara anashindwa kujifunza kutoka kwa polisi wa huko kuwa wakati wa maandamano kazi yao polisi ni kulinda waandamanaji na wao binafsi wasipigwe na waandamanaji na sio kingine. umeona wapi wazungu wanapigwa wakiandamana? anashinwa kuigwa hilo? mtuhumiwa akikamatwa hapigwi hata kidogo lakini hapa kwetu wanakukwaruza na chupa hadi ufe? na hivi wengi wao ni watoto wa mjomba ambao wamefeli form iv ndo wanajiona wana security kubwa sana jeshini. Angalia familia zao ni hovyo kabisa ila wao ndo wanajiona wababe sana tu
 
Kuna mambo mengi yakuangalia ktk maswali yako,
Nionavyo mimi, polisi ni binadam kama sisi na kazi yake kuu ni kulinda usalama wa Raia na mali zao,
Usalama wa Raia na Mali zao, ndio kazi kubwa ya Polisi wetu,
Hapa sasa ni wakati gani analinda usalama wa Raia na ni raia yupi ndio kwenye mtihani,
Mfano kama kuna maandamano na ktk maandamano hayo waandamanaji wanavunja vioo vya magari na kurusha mawe ovyo ovyo.
Polisi anatakiwa awalinde hawa waandamanaji, kwa sababu ni RAIA
Polisi huyu inabidi alinde hili gari lisivunjwe kioo, kwa sababu ni MALI ya RAIA
Sasa basi anaemlinda ndio huyo anaharibu mali, inakuwaje?
Hivyo unaweza kuona jinsi Polisi huyu alivyowekwa kati hapa.
Nionavyo Polisi anatakiwa kuwasimamia waandamanaji RAIA wasidhurike na pia at the same time alinde mali za RAIA zisiharibiwe, wakati wote.
 
Back
Top Bottom