Nipe Buku nikupe Mia nane!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,723
Kuna hii Biashara ya Fedha imezuka kwa kasi sana katika baadhi ya maeneo ya Arusha. Ukifika kituo cha basi kinaitwa Kwa Dr Mohamed, opposite na Summit Centre unakutana na Vijana wanapanga hela (coins) barabarani na kuziuza, ambapo ukitoa 1,000/= unapewa 800/=. Kutokana na shida ya chenji, makondakta wanaingia mkenge huu na kuzinunua!

Napenda kufahamu, je hii biashara ni halali?

Pia je kuna athari zozote za kiuchumi kwenye mzunguko wa fedha kutokana na biashara ya namna hii?
 
Hii biashara sio halali na nakumbuka km mwezi saa umepita BOT walishapiga marufuku hii biashara na kusema fedha haiuzwi so ni biashara BATILI.
 
tegeta mwenge ipo, ukitaka chenji ya 500 wanalamba 50 na ukitaka chenji ya 1000 wanalamba 100
 
Hii ni effect ya kushuka kwa thamani ya hela zetu, kila mtu ana noti kubwa na wachache wana sarafu na noti ndogo.Matokeo yake chenji shida.

BOT hawana haja ya kupiga marufuku hii biashara, in any case black markets zinatokea wanachotakiwa ni kuzidisha supply ya change zinazotakiwa na kuweka system ya watu kuweza kupata chenji katika strategic locations.

Haya mambo ya command system hayaendani na realities za uchumi.Mara nyingine action solve problems better than highanded policies.
 
Back
Top Bottom