NIONAVYO MIMI-Nafasi za ajira jeshi la POLISI zipunguzwe!

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Asalaam Aleikum wana JF; Nimesikitishwa na kitendo cha jeshi letu tukufu la polisi kupotosha hali halisi ya tukio lililotokea Arusha kupitia vyombo vya habari. Kwa maoni ya wengi majeruhi ni wengi kuliko walio ripotiwa,hii inajenga hofu huenda na waliopoteza maisha wakawa zaidi ya idadi iliyotajwa! Vile vile inavyoonekana Polisi walikuwa chanzo cha vurugu katika maandamano hayo! Si Arusha tu; katka mgomo wa kwanza wa UDOM uliowahusisha kitivo cha sayans ya jamii,wanafunzi hao walipigwa mabom ya machoz huku wakiwa wamekaa chini kuashiria amani! Baada ya hapo walifuatwa walipokimbilia na kupigwa virungu na kufanyiwa kila hali ya unyama bila kurudishiwa chochote na vijana hao na wengi waliumizwa sana mpaka kulazwa kwa siku kadhaa! Katka mgomo mwngne wa chuo hcho kitivo cha Elimu,vijana walipigwa mabom ya machoz hata kabla ya kuelezwa lengo la kuandamana kwao! Nimetumia matukio hayo machache ya hv karibun lakin ni mengi ambayo yamefanywa na polisi dhidi ya raia pasipo sababu ya msingi. Mf. Mauaji ya Z'bar ya mwk 2000, vurugu baadhi ya maeneo wakati wa uchaguzi,n.k! Nionavyo mimi serikali ipunguze nafasi za ajira kwani wapo wengi na kazi za kufanya ziko chache yawezekana ndio maana wanajiajiri kusababisha vurugu ili wapate cha kufanya! Kazi ya polis ni kulinda raia na mali zao;sasa wanapochokoza raia na kuleta machafuko katka jamii; tuendelee kuwapa ajira?? Kufanya hvyo sio kuzidi kuongeza hali ya kuvuruga amani yetu? HONGERA JWTZ,endeleeni kulinda mipaka yetu!
 
Back
Top Bottom