Nini wajibu wa Tume ya Katiba? au tunaendeshwa na hisia?

Paul S.S

JF-Expert Member
Aug 27, 2009
6,402
3,242
Baada ya Raisi kutangaza Tume ya katiba kumeibuka mjadala kwa baadhi ya watu kuona kuwa dini fulani inapendelewa dhidi ya din nyingine, na kupelekea kuhisi kutakuwa na kuipendelea dini yenye wajumbe wengi kwenye mchakato mzima wa kupata katiba mpya.

Uzi huu nataka tujikite zaidi kuangalia kazi za tume ya katiba na zitaathiri vipi mchakato mzima iwapo wajumbe wa dini fulani watakuwa wengi zaidi kama ilivyo sasa.

Naamini kabisa tukizijua vizuri kazi na mipaka ya tume ya katiba tutakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kujua kama uwiano wa dini unanafasi au ni hisia za kidini tu

Binafsi naamini kama ilivyo kawaida yetu waTz huwa hatuteuani kwa vigezo vya dini bali uwezo wa mtu binafsi kulingana na alichoteuliwa

Kwa chochote unachodhani kitasababishwa na uwiano huu uliopo basi tujikite kueleza "how" kulingana na kazi za tume ili tuelimishane

Kwa kuanza kama kuna anayezijua vizuri kazi za tume angetuorodheshea kwa mjadala zaidi
 
Back
Top Bottom