Nini umuhimu wa kuunda kamati kama hizi?

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,091
Jana nimepata fursa ya kusoma taarifa za kamati mbili zilizokuwa zinachunguza tukio la kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Channel ten Daudi Mwangosi. Lakini kikubwa nilichokuwa nakisubiri ni ripoti ya tume iliyokuwa imeundwa na Waziri Nchimbi ambayo niliamini kwamba ndiyo ingekuwa na nguvu ya kutuambia hasa nini kilitokea.

Kwanza niliangalia majina ya waliokuwa wanaunda kamati hiyo ya waziri Nchimbi;
Wajumbe wa Kamati hiyo ni:

  1. Jaji (Mst.) Steven Ihema – Mwenyekiti
  2. Bibi Pili Mtambalike – Mjumbe
  3. Kanali (Dkt. Eng) Wema Wilson Wekwe – Mjumbe
  4. Bwana Theophil Makunga – Mjumbe
  5. Naibu Kamishna wa Polisi Issaya Juma. Mngulu – Katibu
  6. Sekretarieti ya Kamati ni:
  7. Bi. Edith T. Assenga – Wizara ya Mambo ya Ndani
  8. Bwana Nasoro H. Msumi – Wizara ya Mambo ya Ndani

Kwa haraka haraka ukiangalia majina haya hapana shaka utajisikia amnai kwani lazima ufikirie kwamba kitakachotoka kwenye tume hii kitakuwa kile hasa kilichojiri. Sikuishia hapo, niliangalia pia hadidu za rejea walizopewa ili kufanikisha kazi yao ambazo nazo zilikuwa zinaonyesha ni namna gani wangeweza kuja na majibu ambayo sisi kama jamii tungeridhika nayo;
Kamati ilipewa Hadidu za rejea zifuatazo:

  1. Uhalali wa mkusanyiko ulioitishwa na CHADEMA eneo la Nyololo,Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa tarehe 02 Septemba, 2012 na kuwepo kwa uvunjifu wa amani.
  2. Kama yalikuwepo makubaliano au maelekezo kuhusu mikutano ya hadhara au maandamano nchini katika kipindi cha Sensa.
  3. Mazingira yaliyosababisha Jeshi la Polisi kutumia nguvu iliyosababisha kifo cha Marehemu Daud Mwangosi na wengine kuumizwa, na uwiano wa nguvu hiyo na tukio.
  4. Madai ya kuwepo uhasama kati ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa na chanzo cha uhasama huo. Aidha kuna madai ya kuwepo kwa orodha ya waandishi watatu (3) ambao Jeshi la Polisi limepanga kuwashughulikia.
  5. Uwepo wa Sheria, Kanuni au Taratibu zinazotoa uwezo kwa Jeshi la Polisi kuzuia mikusanyiko inayoitishwa na Vyama vya Siasa na Mamlaka ya Rufaa endapo vyama hivyo havitaridhika na amri hizo.
  6. Hali ya Mahusiano kati ya Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa nchini katika Utendaji kazi wao na Utii wa Sheria.

Nafikiri wengi wetu tutakuwa tuisoma ripoti ya hawa jamaa ambao napenda nikiri kwamba wameniangusha sana na wamejiangusha wenyewe na baadhi yao kuanza kushusha zile credibility zao mbele ya umma wa Watanzania. Siamini maneno kwamba kuna kitu hawakukitoa eti kwasababu kuna kesi iko mahakamani (wakati kwenye ripoti hii wamemtaja askari anayesemekana kuwa ndiye aliyefanya mauaji) sasa hapo nini unaficha zaidi? Mi naamini hii ndiyo ripoti yao yote na wala hakuna extras zozote walizonazo zaidi ya hizi walizotoa.

Ukiangalia mengi ya majumuisho ya ripoti yao utaona kwamba mengi yake yana majibu ya kisiasa zaidi ya majibu ya kitaaluma (ukizingatia kulikuwa na askari waliobobea kwenye upelelezi kama ndugu yangu Mngulu, waandishi waliobobea naamini kwenye investigative news kama dada yangu Pili pamoja na watu waliobobea kwenye tasnia ya kusikiliza na kisha kutoa maamuzi sahihi kwa kupima uzito wa pande tofauti na kama mwenyekiti wa kamati Mh. Jaji Ihema. Kama ningekuwa bungeni namimi jana ningefanya kitendo kama alichokifanya rafiki yangu Mwigulu, kamata tupa kule kwasababu that was "RUBISH"

Kuna sheria nyingi sana zimeelezwa humu na kwa bahati nzuri shughuli ya kamati hii ilikuwa pia inaagalia broad impact kwa maana ya kitaifa. Then unshindwa kujua kwamba kimsingi siku hiyo kulikuwa na mikutano ya vyama tofauti yaani CHADEMA wao walikuwa Iringa huku CCM wakizindua kampeni kule Bububu ambako alikuwepo Makamu wa Rais, as a non aligned kamati mlitakiwa muanze kuangalia hii double standard kwenye utekelezaji wa sheria moja na ndipo mgeanza kujua chanzo cha migogoro kinapotokea.

Baadae nililazimika kusoma ripoti ya wale waliotumwa na MCT ambayo pamoja na kwamba nayo ilikuwa Biased kwa maana ya kusimama upande wa Waandishi zaidi, lakini iliweza angalau kutupeleka kwenye mchakato mzima wa tukio tena wao wakiwa na ushahidi wa picha za video na mnato ambazo naamini hawa jamaa wa kamati ya Nchimbi wala hawakubother kuziangalia coz hawakutaka kuangalia kitu ambacho kingewapa mawazo ya kubadili ripoti yao ambayo ilikwishaandikwa tayari. Naamini kama wangeona hii angalau ile taarifa waliyopewa kwamba RPC alikuwa mbali na tukio la mauaji ya mwandishi wangelitupilia mbali kwani picha zinaonyesha alikuwa eneo hilo wakati akipigwa na kuna taarifa kwamba yeye ndiye alitoa ishara iliyopelekea mauaji.

Kwa maana ya akili ya kawaida ulikuwa ni upuuzi kusema shughuli za kisiasa zisiendelee wakati wa sensa wakati watu walikuwa wanaenda kazini na kuendelea na shughuli zao nyingine, whats the difference here kati ya watu kuendelea na shughuli zao na kwenda kwenye mkutano ambao kwa wakati huo wanaufanya kuwa mojawapo ya shughuli zao za kawaida?

Kimsingi its a stupid report ambayo siamini kwamba watanzania masikini ndio wametoa pesa zao kuwalipa hawa watu kwenda kufanya kazi hii ambayo naamini angepewa mtoto wa kidato cha pili angeifanya vyema kuliko hivi tena bila kuwa na weledi wowote ule kitu chochote.

Nachukia upuuzi na huu ni mojawapo ya puuzi hizo....
 
Back
Top Bottom