Elections 2010 Nini Tofauti ya Mramba, Chenge NA Mwakalebela?

Mtu66

Senior Member
Jun 26, 2007
165
3
Nini tofauti ya hawa watu wawili katika medani sa siasa za CCM?
Kwanini jina la Pesambili lirudi ili hali yuko mahakami tayari kwa tuhuma vile vile?
Hivi tunaongozwa na CCM ya Vichaaaaa??

33nhx69.jpg

Fredrick Lameck Mwakalebela

2hoh8ra.jpg

Basil Pesambili Mramba
 
Tofauti ipo ndiyo maana wamekuwa treated tofauti.

unataka uambiwe kila kitu? tehetehe
 
Huyo mmoja tuhuma zake zipo kwenye kupata hicho cheo ila huyo mwingine anatuhuma kwenye kitu kisicho na uhusiano na anachogombea.
 
Sawa wote hawa siwanashitakiwa na kesi zao ziko mahakamani inakuwaje mmoja anatolewa
alafu mwingine anaachwa au monica mtandao?
 
Mbona wengi tu wana tuhuma lakini wamepitishwa; Blandes anakesi ya rushwa mahakamani lakini nae kapitishwa!! Kikwete anausongo na majina ya watu wa Mbeya nini?
 
Sio Mramba peke yake mwenye tuhuma aliyepitishwa, wako wengine kama vile Blandes ambae nae ana kesi ya rushwa mahakamani lakini amepeta!! Jakaya inaelekea akiona majina yanayofananafanana kama vile watu wa mkoa wa Mbeya yanampa taabu kidogo, anakumbuka walivyompiga mawe!!
 
Hapa kinachohitajika ni wale waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa ili wapate nafasi hizo wanazozitaka. Kwa lugha rahisi ni wale waliotaka uongozi kwa rushwa na wamefikishwa mahakamani? Huyo Blandes naye kafikishwa? Mbona kila kitu tunakimbilia kudhani ni mkoa fulani?? Hebu tejenge hoja na si tuvizie huruma.
 
Hivi hujui kuwa Mramba ni mshirika wao mafisadi wa siku nyingi? Hiyo ndiyo tofauti yake na Mwakelebela. Fungua macho:glasses-nerdy:
 
:playball:mramba na kikwete wako kwenye orodha ya mafisadi lakini mwakalebela hayumo ndo maana kuna tofautiiii
 
Hapa kinachohitajika ni wale waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa ili wapate nafasi hizo wanazozitaka. Kwa lugha rahisi ni wale waliotaka uongozi kwa rushwa na wamefikishwa mahakamani? Huyo Blandes naye kafikishwa? Mbona kila kitu tunakimbilia kudhani ni mkoa fulani?? Hebu tejenge hoja na si tuvizie huruma.

Maajabu yenyewe ya serikali hii ni kwamba huyo Blandes ana kesi mahakamani ya rushwa ya uchaguzi wa 2005; uchunguzi ulikuwa haujakamilika lakini sasa umekamilika na ndio maana kafunguliwa kesi!!
 
Mbona wengi tu wana tuhuma lakini wamepitishwa; Blandes anakesi ya rushwa mahakamani lakini nae kapitishwa!! Kikwete anausongo na majina ya watu wa Mbeya nini?
Inawezekana!
Lakini niilishaandika humu ndani kwenye thread ya MwakB kufikishwa mahakamani. Iringa ni ya pekee, kihistoria hili jimbo lina wenyewe. MwakB kauwawa na kamati ya siasa ya mkoa wa Iringa. hao wengine walitajwa vizuri na kamati zao. Ukiangalia vigezo vilivyotajwa na Chiligati kwa mwakB ni maadili na hili ni neno lina funga semi, muulizeni maadili manake nini?
 
wakati mwingine unaweza fikiri ccm wanavuta majani (kama mashati yao ya kijani yanavyoonyesha), ni kama wafuasi wa bob marley vile. sijui walisahau?, hakuna tofauti yoyote. the issue here ni mtu kutoonekana ni mtenda makosa bila mahakama kuthibitisha hivyo. mwakalebelea kwa sasa hajawa proven guilty, yuko innocent kama vile mramba alivyofanya tu. wote hao ni innocent. na mramba ndio hatari kuliko mwakalebela kwasababu mramba ubadhilifu wake ndo uliingiza hasara kubwa ya mabilioni kwenye nchi yetu, pamoja na kwamba bado ni suspect, hakutakiwa kutofautishwa na mtoa rushwa mwakalebela, wote wako sawa kabisa. hapo ndo utaona namna ccm wanavyolindana. naona kwasasaivi maji yanataka kuwafika shingoni, wanatapatapa kila walanolifanya ni aibu tu. yetu macho.

kwa watu wa iringa, monica mbega hawafai kabisa, hamieni wote chadema au cuf kuwakomesha, kwasababu miaka yote hiyo huyo monica mbega ambaye at the same time alikuwa mkuu wa mkoa mwingine ambao si wa iringa, hana faida. miaka yote hiyo inatosha. mwakalebelea pamoja na mbega wote hawafai. mwakalebele mtoa rusha hana maana, na amelikoroga atalinywa lote. ndo kwishnei hiyo labda aende kweney business tu, siasa ameshakoroga, TFF ameshakoroga...kila kitu chali. basi TFF alikuwa anaiba sana kama kauchaguzi tu ka iringa hako ndo amefanya hivyo. tatizo wala rushwa wanaamini kuwa hawawezi kukamatwa? mweeee,

Watu wa iringa nawapa pongezi kitu kimoja. mwakalebela ni mtu wa Rungwe kule mbeya, lakini amepata wafuasi wengi sana iringa kwa wahehe, hii inaonyesha namna tz tusivyokuwa na ukabila, mchaga anaweza kwenda kugombea sumbawanga, mhehe akaenda kugombea songea etc kitu ambacho nchi zingine hakiwezekani.
 
Sawa wote hawa siwanashitakiwa na kesi zao ziko mahakamani inakuwaje mmoja anatolewa
alafu mwingine anaachwa au monica mtandao?

Mramba ameshashinda kesi hata kabla haijaisha kusikilizwa na Mwakalebela alishashindwa hata kabla kesi haijapelekwa mahakamani! As simple as that.
 
Nimesikitika sana na kukwazika sana kutokana na jinsi mambo ya siasa yanavyoendeshwa hapa tz. Suala la Mwakalebela pamoja na mambo mengine yameudhi sana watu wengi, hii nchi inavyoonyesha kuna wenye haki ya kupendelewa kadharika kuna wenye haki ya kuonewa, ndiyo maana sitashangaa kuona wale ambao wamepingwa na wananchi kwa nguvu ya kidemokrasia tutawaona wakiteuliwa na kurudishwa ndani ya ulingo wa kisiasa kwa njia wanazozijua wenyewe, hilo halina ubishi. Kuhusu ndugu yetu, Rafiki yetu Mwakalebela naamini alichinjiwa hukohuko iringa na kamati ya siasa ya mkoa au vyovyote vile, Dodoma ilikuwa kusomewa Dua tu ya kumuewaka mahali pabaya. Ndio maana mimi na siasa:frusty:
 
Huyo mmoja tuhuma zake zipo kwenye kupata hicho cheo ila huyo mwingine anatuhuma kwenye kitu kisicho na uhusiano na anachogombea.

Sijakubaliana na wewe kwa hoja hiyo yenye bold.
Mkuu wa wilaya Betty Machangu alikamatwa na PCCB kwa kugawa rushwa na amepitishwa na sisiemu hiyo hiyo.
Tukubaliane kwamba katika chama hiki kuna double standards. Nukta.
 
Back
Top Bottom