Nini tofauti ya maneno haya?

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Neno-KIBURI
Neno-JEURI

Maneno haya kama ya shabihana lakini naona kama ya natofauti kimaana!
 
Kiburi ni hali ya kuwa na dharau ya kuzaliwa nayo, yaani mtu ana kuwa mjeuri kila wakati hata kama hastahili.

Jeuri inaweza kuwa ni ya muda kisha mtu akajirekebisha au ikatokea mtu akawa anajeuri baada ya kupata kitu fulani kinachomfanya kujiona yupo tofauti na wengine.
 
Kiburi ni hali ya kuwa na dharau ya kuzaliwa nayo, yaani mtu ana kuwa mjeuri kila wakati hata kama hastahili.

Jeuri inaweza kuwa ni ya muda kisha mtu akajirekebisha au ikatokea mtu akawa anajeuri baada ya kupata kitu fulani kinachomfanya kujiona yupo tofauti na wengine.
Mkuu mbona vitu hivi kama vinaingiliana??au nikitu kimoja??
 
Wakuu naomba nijuzwe pia tofauti ya maneno haya na matumizi yake katika sentensi.
neno, Nafuu
neno, Afadhali
 
KIBURI -Hii ni hali ya mtu kuwa na jeuri
JEURI- Hii ni hali ya mtu kuwa na kiburi
Asante kwa kunielewa
 
Kiburi ni Hali ya mtu kuwa na Aina fulani ya dharau lakini Mara nyingi inakuwa ndani kwa ndani. Inaweza kuwa mtu hasalimii au akitumwa haendi na akiulizwa anakaa kimya hajibu kitu. Sio lazima aseme ila matendo yake yanaonesha dharau

Jeuri sasa ndio kiboko. Mtu hajali na anaonesha dharau wazi wazi na anatamka kabisa. Mtu anakuwa na uwezo wa kukufanya kitu chochote hata kama ni cha kukuumiza kwa makusudi lakini huwezi kumfanya kitu. Hii inakuwa inalindwa na nguvu kutoka nje ya huyo mtu. Yaweza kuwa ana nguvu ya ziada sababu anatumia hela zake kuwahonga walinda usalama au walinda sheria, yaweza kuwa anatumia cheo chake katika jamii kutokufanywa kitu au urafiki wake/undugu wake na wanaotakiwa kumshughulikia

Katika summary, kiburi ni tabia/nguvu iliyo ndani ya mtu hata akiwa mnyonge vipi ila Jeuri Mara nyingi inaletwa na nguvu au Hali kutoka nje ya mtu
 
Wakuu naomba nijuzwe pia tofauti ya maneno haya na matumizi yake katika sentensi.
neno, Nafuu
neno, Afadhali
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AFADHALI'

Neno afadhali katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino: [Ngeli:i-/i-] hali yenye unafuu; hali bora zaidi.

2. Kivumishi: tamko la kuonesha hali bora na ya kufaa zaidi ikilinganishwa na hali zingine.

3. Kielezi: bora kuliko; nafuu kidogo.

Kuna methali: Afadhali ya Musa kuliko ya Firauni.

Kuna msemo: Afadhali mchawi kuliko mfitini.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili afadhali (soma: afdhwalu/afdhwala افضل) lina maana zifuatazo:

1. Kitenzi: Amefanya bora.

2. Nomino: Amekuwa mbora zaidi.

3. Nomino: Ziada na wingi.

4. Nomino: Kichobaki, salio.

Kinachodhihiri ni kuwa neno afadhali ( soma: afdhwalu/afdhwala افضل) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno afadhali halikubadili maana yake ya msingi katika lugha ya asili - Kiarabu.
 
Neno-KIBURI
Neno-JEURI

Maneno haya kama ya shabihana lakini naona kama ya natofauti kimaana!

Kiburi ni mtu mwenye dharau

Jeuri hii pamoja na dharau huambatana na vayolensi kama kutukana kupiga nk
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom