Nini Tofauti ya Jeneza na Sanduku la Maiti

IshaLubuva

JF-Expert Member
Dec 4, 2008
250
11
Wana JF nimekuwa nikipata ukakasi kuhusu matumizi ya maneno Jeneza na Sanduku la Maiti/Marehemu. Mara nyingi watu wamekuwa wakiyatumia maneno haya mawili kana kwamba yaanamaanisha kitu kimoja. Lakini mimi binafsi naamini kuwa yanamaanisha vitu wiwili tofauti:

Jeneza ni nyenzo ya kubebea mwili wa marehemu kutoka nyumbani/hospitali kwenda kwenye kaburi (kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine). Kwa kiingereza linaitwa Bier.

Sanduku la maiti ni boksi lililotengenezwa kwa ajili ya kumhifadhi marehemu ikiwa ni pamoja na kumsafirishia kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kwa kiingereza linaitwa coffin.

Tofauti kubwa kati ya Jeneza na Sanduku la Maiti ni kwamba Jeneza huwa halizikwi pamoja na marehemu wakati sanduku la maiti huzikwa pamoja na marehemu.

Waswahili karibuni kwa mjadala
 
Aise nimefungua hii thread nikajua nitakuta michango ya Wanajukwaa, zaidi ya mwaka na miezi 3 sasa naomba kuamsha huu uzi.
 
Wana JF nimekuwa nikipata ukakasi kuhusu matumizi ya maneno Jeneza na Sanduku la Maiti/Marehemu. Mara nyingi watu wamekuwa wakiyatumia maneno haya mawili kana kwamba yaanamaanisha kitu kimoja. Lakini mimi binafsi naamini kuwa yanamaanisha vitu wiwili tofauti:

Jeneza ni nyenzo ya kubebea mwili wa marehemu kutoka nyumbani/hospitali kwenda kwenye kaburi (kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine). Kwa kiingereza linaitwa Bier.

Sanduku la maiti ni boksi lililotengenezwa kwa ajili ya kumhifadhi marehemu ikiwa ni pamoja na kumsafirishia kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kwa kiingereza linaitwa coffin.

Tofauti kubwa kati ya Jeneza na Sanduku la Maiti ni kwamba Jeneza huwa halizikwi pamoja na marehemu wakati sanduku la maiti huzikwa pamoja na marehemu.

Waswahili karibuni kwa mjadala
Taelezea sana kama utanijibu kama unajua maana ya Lahaja (dialects), neno (word) na kishazi (phrase).

Maana bila kuelewa hayo maeneo hatutaelewana.
 
Vyote ni aina ya vyombo vya kubebea wafu...
Lakini vina tofauti, sasa hiyo tofauti ndio inayotafutwa hapa. Mfano ni sahihi kusema Sato na King fish wote ni Samaki lakini wana tofauti.
 
Taelezea sana kama utanijibu kama unajua maana ya Lahaja (dialects), neno (word) na kishazi (phrase).

Maana bila kuelewa hayo maeneo hatutaelewana.

Phrase ni kifungu cha maneno chenye kitenzi ambacho kina maana kamili au wakati mwingine kinahitaji kitenzi kisaidizi ili kuleta maana. Mfano;

1. Kalamu ya Juma ni nzuri sana
2. Fundi amekuja
(Yupi) anayetengeza Makomeo.

Neno: Ni mkusanyiko wa sauti zinazotamkwa au kuandikwa pamoja na kuleta maana. Mfano: Kalamu

Lahaja: Ni lugha ndogo ndogo ambazo hutumiwa na watu wa jamii fulani katika eneo la kijiografia wanaloishi.

Nadhani hoja yako inakuja kwa maana kwamba maeneo ya Pwani wakazi wake wengi wanaabudu dini ambayo taratibu zao za kuzika Marehemu anazikwa na sanda tu (Hawa wanaita kile kibebeo cha maiti kuwa ni Jeneza) na wale ambao Marehemu anazikwa kwenye box la mbao (whatever material) wanaita Sanduku.

Katika mazishi mengi ambayo nimehudhuria limezoeleka neno "Jeneza" hata pale ambapo Marehemu anazikwa akiwa ndani ya box.
 
zote ni nyezo za kubebea mfu ila jeneza hutumiwa xaana kutamkwa na waislam na sanduku hutumiwa na upande mwingne wa imani(wakristo)))
 
kwa ninavyofaham sanduku huzibwa kote ila jeneza huwa na uwazi, kwa mbao zilizopangiliwa kama kichanja na huwa kama machela
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom