Kiraka Kikuu
JF-Expert Member
- Oct 3, 2011
- 5,904
- 1,976
Ni usiku wa manane.Namuona Job Lusinde akipanda jukwaani huku povu likimtoka puani,masikioni na nyoka wakali wakimtoka mdomoni...
Baada ya muda namuona BWM akirusha marungu huku na huko kuelekea pembe nne za nguo kuubwa yenye rangi ya kahawia.
Jambo linalo shangaza ni kwamba upepo mkali toka juu angani unavuma na kupeperusha marungu yale na yanakwenda kubonda nguo nyingine kubwa zaidi yenye rangi inayo fanana na majani mabichi!
Nikiwa usingizini bado,naona ghafla maji mekundu yakichuruzika toka kwenye nguo ile
ya kijani kuelekea kwenye nguo yenye rangi ya kahawia,lakini kwa mshangao mkubwa mabonge ya damu yanatoka ghafla toka kwenye nguo kahawia na kusukumia mbali maji yale kuelekea kusikojulikana!
Muda kidogo unapita na ndipo naona umati mkubwa wa watu walio vaa nguo zenye mistari ya rangi za manjano,kijani,nyeusi na bluu wakiwa na huzuni kubwa,wakiangalia watu waliopo jukwaani kwa matumaini makubwa!
Sehemu kubwa ya umati huo wanaonekana wamekonda,kudhoofu na wajinga na wote wamebeba mapanga,marungu na mitutu ya bunduki,lakini wanasubiri nguo ile ya kijani iwaokoe!
Baada ya hapo katika ardhi niliyo simama,nikaona udongo ule ukigeuka transparent,na chini yake nikaona sura ya mzee akilia!Mzee huyo alikufa akiwa na miaka 77,meno yake yamechongwa na ana mvi kichwa kizima!Hivyo nikajua huyu atakuwa mwalimu Julius K Nyerere.
Mzee huyu akapiga kelele,"Enyi watanzania msio na akili,acheni kulia!Tumieni silaha zenu kushambulia hilo vazi la kijani!"
ndipo watanzania wakaanza kurusha silaha zao kuelekea kwenye vazi la kijani,na vazi lile likapotea,huku vazi la rangi ya kahawia likianza kumea na kuchanua...
Watu wale umati wakaanza kunawiri na kufanya kazi kwa juhudi na kula matunda ya kazi yao!
Mzee yule chini ya ardhi akaanza kuchekelea na kufurahi.
Ghafla nikajikuta nimeamka asubuh,huku njaa kali ikiniuma!!