Nini mustakabali wa siasa za Tanzania na vikundi vya "Wanamgambo" wa Vyama?

Nilimsikia msemaji wa Polisi akihojiwa jana na BBC. Alilaani sana Chadema kuunda kikosi cha ulinzi na kuwa ni uvunjifu wa sheria. Lakini alipoulizwa mbona CCM ina GreenGuard alishindwa kujibu kabisa pia kuhusu sungusungu alikosa pia majibu.
Tatizo la polisi ni kuona kila kifanywacho na CCM ni sawa kwa mujibu wa Sheria ila wengine sio sawa. Nawapongeza sana Chadema kwa kuliona hilo.
Pengine kuna sheria za Bunge zinaruhusu kuunda jeshi la sungu sungu pengine na mashirika ya ulinzi bunafsi (wanasheria watatusaidia) Lakili hili la Ulinzi ndani ya vyama kwa nini watu wanagutuka saa hizi? Hata hivyo ni nini tusiimarishe jeshi la polisi lisifanywe kuwa imara na linalozingatia haki na usawa ili kuepuka haya mambo mengine? Hatuoni katika mazingira haya, kila kikosi usalama kitapawa kujiimarisha vilivyo ili kujilinda na hatimae kitakachokuwa na uwezo zaidi kitaogopwa na hivyo kutohujumiwa ila ili kipate uwezo huo ndani yake kutakuwa na mashindano ambayo ni hatari?
 
Kuanzisha haikatazwi, kosa ni kutangaza kuwa na jeshi baada ya kuanzisha. Mbona siku nyingi tu
 
Good analysis. Naunga mkono hoja!

Kuwa na vikundi vya kujihami ndani ya nchi huru ni dalili tosha za taifa lililoparaganyika. Hakuna anayemuamini mwenzake.
Hivyo basi ni vyema vikundi vyote (green guard, blue guard, red brigade n.k) vipigwe marufuku pronto kwa mustakabali wa taifa letu. Vyama vitapita, viongozi watapita lakini Taifa litabaki.

Chonde Mh Kikwete, haya ni mawingu na mvua i jirani. Hujachelewa, amua sasa! Fanya maamuzi magumu ulilinde Taifa kama ulivyoapa. Kukaa kimya hakujawahi kuondoa hatari na wala mzaha haujawahi kulifaidia Taifa kwa jambo lolote.
 
Good analysis. Naunga mkono hoja!

Kuwa na vikundi vya kujihami ndani ya nchi huru ni dalili tosha za taifa lililoparaganyika. Hakuna anayemuamini mwenzake.
Hivyo basi ni vyema vikundi vyote (green guard, blue guard, red brigade n.k) vipigwe marufuku pronto kwa mustakabali wa taifa letu. .
mkuu sio kuvipiga marufuku bali kutumia njia nyingine itakayo visababisha vyama vya siasa na hasa vya upinzani kujihakikishia kwamba watu wake watakuwa salama.Katika mazingira hayo automaticaly kutakuwa hamna haja ya vikundi hivyo. Zaidi ya hapo kusema vifutwe na wakati vyama vya upinzani vinalalamika vinadhuriwa kwa makusudi na hakuna wakuwatetea haviwezi kukubali.
 
Vyama vilisajiliwa kwa kuzingatia katiba za vyama hivyo zinasemaje na sheria za nchi zinavyoelekeza kuhusu uhalali wa vyama. Kama haya ya vikosi vya ulinzi hayamo katika katiba za vyama husika na sheria za nchi hazitoi ruhusa, tumuulize msajili wa vyama; kulikoni?
 
Lakini ukumbuke msajili wa vyama alishasema kuwa kuna vitu ambavyo chama kikikosea kama ni CCM, Itabidi akishauri na kama ni CHADEMA anaweza akaifuta.Sasa ukumbuke walioanza ni CCM? Upo!
 
Mkuu betlehem tatizo liko kwa rais ambaye ameamua kumkabidhi nchi Lowasa ili amfadhili Mwigulu
kulitumia jeshi la polisi kwa maslahi yake binafsi bila kujali madhara yanayoweza kutokea kwa watanzania'
 
Pengine kuna sheria za Bunge zinaruhusu kuunda jeshi la sungu sungu pengine na mashirika ya ulinzi bunafsi (wanasheria watatusaidia) Lakili hili la Ulinzi ndani ya vyama kwa nini watu wanagutuka saa hizi? Hata hivyo ni nini tusiimarishe jeshi la polisi lisifanywe kuwa imara na linalozingatia haki na usawa ili kuepuka haya mambo mengine? Hatuoni katika mazingira haya, kila kikosi usalama kitapawa kujiimarisha vilivyo ili kujilinda na hatimae kitakachokuwa na uwezo zaidi kitaogopwa na hivyo kutohujumiwa ila ili kipate uwezo huo ndani yake kutakuwa na mashindano ambayo ni hatari?

Sheria inayoruhusu sungusungu ni Police Force and Auxiliary services Act
 
Sheria inayoruhusu sungusungu ni Police Force and Auxiliary services Act hasa kipengele kinachoongelea armed na unarmed peoples militia
 
Sheria inayoruhusu sungusungu ni Police Force and Auxiliary services Act
Kweli kwa hilo uko sahihi mkuu.Ila kwa mengine majawabu yake naona ni magumu kwa kila mtu na ndio mana hakuna anayechangia kitu.Any way ujumbe umefika.
 
Lazima twende kwenye sheria ya nchi na sio kutazama katiba za vyama. Piga marufuku tu hakuna jingine.
 
Nafikiri na wakati muafaka kwa pande zote kukubali kuwa Green guards, Blue guards na Red Brigade hazina tofauti na zina malengo yanayofanana. Waanzilishi ni CCM na wengine wameiga tu. Vingine vyote tunavyobishana hapa ni siasa na propaganda. Kama nchi nyingine zifanyavyo, zaidi ya jeshi la police kutoa ulinzi ............ ulinzi wa ziada hutolewa na security companies.

Nafikiri ni muda muafaka Watanzania kuzikataa Green Guards, Blue Guards na Red Brigade na ulinzi badala yake ufanye na vyombo husika.

Nawasilisha!!
 
kama kufutwa vifutwe vyote mpaka chipukizi kwasababu ni ya kisiasa pia. Kama unataka kulinda nchi nenda JKT
 
Nafikiri na wakati muafaka kwa pande zote kukubali kuwa Green guards, Blue guards na Red Brigade hazina tofauti na zina malengo yanayofanana. Waanzilishi ni CCM na wengine wameiga tu. Vingine vyote tunavyobishana hapa ni siasa na propaganda. Kama nchi nyingine zifanyavyo, zaidi ya jeshi la police kutoa ulinzi ............ ulinzi wa ziada hutolewa na security companies.

Nafikiri ni muda muafaka Watanzania kuzikataa Green Guards, Blue Guards na Red Brigade na ulinzi badala yake ufanye na vyombo husika.

Nawasilisha!!

Inawezekana hoja yako ikapata mashiko. Ila umeiweka too general Zero.
 
Me nafikiri hapa kinachotakiwa ni kufuta vikundi vyote bila kujali green gards,red brigade and whatever. Maana inaonekana vitakuja kuleta maafa makubwa sana Kwa siku za usoni.
 
Nilimsikia msemaji wa Polisi akihojiwa jana na BBC. Alilaani sana Chadema kuunda kikosi cha ulinzi na kuwa ni uvunjifu wa sheria. Lakini alipoulizwa mbona CCM ina GreenGuard alishindwa kujibu kabisa pia kuhusu sungusungu alikosa pia majibu.
Tatizo la polisi ni kuona kila kifanywacho na CCM ni sawa kwa mujibu wa Sheria ila wengine sio sawa. Nawapongeza sana Chadema kwa kuliona hilo.

EBHANAE,right ccm na serikal yake watakapoamua kukir na kutambua udhaif wao,hakuna tena chokochoko! maneno ulosema hapa,nakupa big-up,keep it up!
 
Molemo,
Unakimbia hoja ya mleta uzi, yeye hajauliza mabaya green Guard wala Red guard bali tunahaja ya kuwa na vikundi hivi?
Nijuavyo mimi green guard ilikuwapo tangu hata uwepo wa vyama vya siasa havijaidhinishwa. Ni wazi malengo yake hayakuwa kuwa dhuru au kulinda viongozi wa chama kwani wao huwa wanaulinzi wa jeshi la polisi. Kinachoonekana eitha malengo ya green guard yamebadilika kama kweli inahusika na hayo wanayosemwa. Mimi nadhani tuliamini jeshi letu la polisi na tusiruhusu haya majeshi mbadala. Pia tujiulize ni yalikuwa hasa malengo ya green guard wakati kimeanzisha hata kabla ya uwepo wa vyama vingi vya siasa.
Kuna mdau hapo nyuma Massenberg anasema ccm ikiendelea kuwepo madarakani itapelekea vikundi hivi kuja kuleta vita, mimi nadhani ungesema kinyume chake.
 
Last edited by a moderator:
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom