Nini matumizi ya hazard light kwenye gari?

WA MAMNDENII

JF-Expert Member
Jun 5, 2010
344
57
madereva wa kibongo wananishangaza kama sio kunisikitisha na matumizi ya taa za hazard wanapoendesha magari yao, utamkuta dereva anasimamisha gari katikati ya barabara anawasha hazard halafu unaona abiria anashuka kutoka kwenye gari kisha dereva anazima taa zake za hazard anaendelea na safari, kwa uelewa wangu mi najua hizo taa zinawashwa wakati gari linapopata hitilafu likiwa katikati ya road ndio ziwashwe kwa ajili ya kumtahadhirisha dereva wa gari linalokuja nyuma au wadau munijuze matumizi zaidi ya ninavyojua.
 
Kazi ni moja tu na umeshaitaja. Ni kuwapa taarifa watumiaji wengine wa barabara kuwa gari yako ina hitirafu hivyo huwezi kufuata taratibu husika katika eneo husika. Kuna wengine huwa wanawasha hazard mahala penye pacha nne wakimaanisha wananyoosha. Kumbe wanasahau aliyeko kulia atadhani unakata kulia na huyu wa kushoto atajuwa unakata kushoto.
 
Ukiona wanafanya hivyo jua sehemu hiyo hairuhusiwi kushusha abiria. Wanawasha ili kuzuga tu.
 
Kazi ni moja tu na umeshaitaja. Ni kuwapa taarifa watumiaji wengine wa barabara kuwa gari yako ina hitirafu hivyo huwezi kufuata taratibu husika katika eneo husika. Kuna wengine huwa wanawasha hazard mahala penye pacha nne wakimaanisha wananyoosha. Kumbe wanasahau aliyeko kulia atadhani unakata kulia na huyu wa kushoto atajuwa unakata kushoto.
Eh, mimi pia nimezoea kufanya hivyo. Hebu tupeane akili kidogo, kwenye pacha tunatakiwa tufanyeje?
 
Eh, mimi pia nimezoea kufanya hivyo. Hebu tupeane akili kidogo, kwenye pacha tunatakiwa tufanyeje?

Kama hiyo pacha haina traffic lights basi michoro itaonyesha na lazima barabara moja itakuwa ni main road au zote zikiwa main basi utapigwa mzunguko! Traffic rules zinafafanua zaidi, kasome!!
 
Eh, mimi pia nimezoea kufanya hivyo. Hebu tupeane akili kidogo, kwenye pacha tunatakiwa tufanyeje?

Kama unapinda kushoto washa indicator ya kushoto kama ni kulia washa ya kulia, kama unakatiza usiwashe hazard katiza tu
 
Barabara nyingi za Tz hazina traffic light na mie mara nyingi nikifika kwenye barabara kama hizo huwa nawasha hazard. Naomba elimu zaidi
 
Barabara nyingi za Tz hazina traffic light na mie mara nyingi nikifika kwenye barabara kama hizo huwa nawasha hazard. Naomba elimu zaidi
Hutakiwi kuwasha taa za hazard. Hii inamaanisha unanyosha. Kuna wengine huwa wanawashiana mitaa mikubwa kwa kumuliika mulika kuonyesha kuwa amekuruhusu kufanya unachoomba. WANAKOSEA. Maana ya kufanya hivyo ni kuwa anayewasha anamuonya anayewashiwa kuwa anachokifanya si sahihi
 
Wengine wanawasha wakati wakiwa wanafanya mbwembwe kwenye msafara wa harusi kuonyesha mwendo anakwenda nao ni taratibu na mbwembwe kiasi!
 
[h=4]Hazard flashers[/h]Also called "hazards", "hazard warning flashers", "hazard warning lights", "4-way flashers", or simply "flashers". International regulations require vehicles to be equipped with a control which, when activated, flashes the left and right directional signals, front and rear, all at the same time and in phase.[SUP][5][/SUP][SUP][15][/SUP] This function is meant to indicate a hazard such as a vehicle stopped in or near moving traffic, a disabled vehicle, a vehicle moving substantially slower than the flow of traffic such as a truck climbing a steep grade, or the presence of stopped or slow traffic ahead on a high speed road. Sometimes, they are used in severe fog conditions.[SUP][citation needed][/SUP] Operation of the hazard flashers must be from a control independent of the turn signal control, and an audiovisual tell-tale must be provided to the driver. In vehicles with a separate left and right green turn signal tell-tale on the dashboard, both left and right indicators may flash to provide visual indication of the hazard flashers' operation. In vehicles with a single green turn signal tell-tale on the dashboard, a separate red tell-tale must be provided for hazard flasher indication.[SUP][5][/SUP][SUP][15][/SUP][SUP][76][/SUP][SUP][77][/SUP] Because the hazard flasher function operates the vehicle's left and right turn signals, a left or a right turn signal function cannot be provided while the hazard flashers are operating.
 
mliosema hapo juu mpo sahihi, ni makosa kuwasha hazard kumaanisha haupindi kulia wala kushoto. Jambo sahihi unalotakiwa kufanya ni kupita bila kuwasha taa zozote za alama. Hazard inatumika kumaanisha hatari. Unaweza ukawa umepata hitilafu katikati ya barabara, au kumjulisha dereva aliye nyuma yako kwamba mbele kuna hatari. Pia unaweza kuwa umebeba mgojwa kwa dharura hivyo kuwataarifu wenzako wakupe nafasi.
 
Wengine wanawasha wakati wakiwa wanafanya mbwembwe kwenye msafara wa harusi kuonyesha mwendo anakwenda nao ni taratibu na mbwembwe kiasi!
mkuu sio kwa sababu ya mbwembwe tu pia ni kwa sababu wanakuwa wanaenda mwendo mdogo kuliko kawaida kwa hiyo wanakuwa wanatoa ishara kwa watumiaji wengine wa barabara.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom