Nini maoni yako kuhusu Utendaji wa Spika wa kwanza mwanamke Tanzania

hana lolote mama huyu.....yani anaboa kweli kweli na anawapendelea ccm ndo maana mara nyingi anatoa mwongozo wa wabunge wa upinzani waandike utetezi kwa maandishi
 
Kwa maoni yangu binafsi na ninavyomfahamu huyu mama si mbaya kama wengi mnavyomjadili. Udhaifu unaojitokeza ni matatizo ya mfumo tulionao, kumbukeni bado mhimili wa Executive umelegea sana, na shughuli nyingi za Bunge zinaletwa na serikali. Pamoja na ukweli kwamba Spika bado ana jukumu la kuliendesha Bunge liweze kuisimamia na kuishauri serikali, tukumbuke Bunge hili ni tofauti sana na mabunge yaliyopita. Composition ya wabunge wa leo ukiongezea na uelewa wa wananchi walio nao leo hii si sawa na wakati mwingine wowote uliopita; bunge hili lina challenges nyingi na matatizo ya nchi hii yanazidi kuongezeka kila uchao. Kwa kuwa mfumo mzima umeoza, tumpe muda huyu mama badala ya kumponda, tumsaidie, tumshauri, tuonyeshe wapi anakosea naye ni binadamu anajifunza kutokana na makosa. Naamini ipo siku huyu mama atakuja kutu-prove wrong. Tusiwakatishe tamaa akina mama wanapokutana na challenges kama hizi. Jamani hayo ni maoni yangu.
 
Baada ya Tanzania kumpata spika mwanamke wa kwanza na kuandika historia mpya ya bunge la nchi hii unaweza kusema nini juu ya utendaji wake so far. Kuna matumaini yeyote ya kupata ufanisi wabunge letu kwa kuzingatia jinsi anavyo liendesha bunge mpaka sasa na uwezo wake au matumaini ya ufanisi wa bunge yana fifia.
Wakuu mi cna iman hata kiduchu na huyo mama, i see her as a puppet of ccm and she has proved it!
 
Back
Top Bottom