Nini madhara ya kunywa maji lita 6 kwa siku?

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
Wanajamvi,

Nina mdogo wangu yupo 45 yrs anakunywa maji lita kwa siku; asubuhi, mchana na usiku. Jumla, anakuwa amemaliza lita 6. Kwasababu ya kunywa kiasi hicho cha maji, huwa anaenda sana haja ndogo.

Je, kuna madhara yoyote?
 
Kama anakunywa kwa kuhisi kiu, basi aende hospital akapime blood sugar. Kama anakunywa coz amesoma au ameshauriwa na Dr. Ndodi kunywa lita 6 kwa siku, mwache aendelee kwani ni afya kwake.
 
Kama kashauriwa na ndodi tutarajie kumpoteza soon. Kama sivyo apime sukari au afike wilolesi dispensary mafinga nitamtibu
 
Unatakiwa Kunywa Maji kulingana Na Uzito wako si Kubugia Maji Tu.. Utakuwa Unakojoa Na Madini ya Mwili Sasa

Mfano Mwenye Uzito wa 60kg Anatakiwa Kunywa Maji lita 2.5 asizidi hapo..
 
Inatengemea na kazi anayofanya kama ni kupasua mbao au kupasua mawe hyo n sawa
 
Anachoma tanuri la mkaa au anafanya kazi katika kiwanda cha kutengeneza nondo huyo nahisi
 
RGforever na Barca naomba mnisaidie kwa pamoja.
Kwanza, kisukari kinasababishaje kiu ya Mara kwa Mara?
Pili, ukiwa na uzito mkubwa kuanzia let say 80-90 ukawa unakunywa lita zaidi ya nne kwa siku, utapata madhara gani kiafya?
Naomba kuelimishwa.
MziziMkavu pita pande hii pia tafadhali

Cc: Fadhili Paulo
 
Last edited by a moderator:
Mmawia

Basi huyo mdogo wako anakunywa kwa siku maji Lita 6 pasipo na kula chakula? Hebu mpeleke hospitali ukampime huyo mdogo wako. Huenda ana Maradhi Tumboni.
 
Last edited by a moderator:
Unatakiwa Kunywa Maji kulingana Na Uzito wako si Kubugia Maji Tu.. Utakuwa Unakojoa Na Madini ya Mwili Sasa

Mfano Mwenye Uzito wa 60kg Anatakiwa Kunywa Maji lita 2.5 asizidi hapo..

Mkuu huyu alisikia ushauri kupitia tv,ana uzitito wa kilo 106.
 
Basi huyo mdogo wako anakunywa kwa siku maji Lita 6 pasipo na kula chakula? Hebu mpeleke hospitali ukampime huyo mdogo wako. Huenda ana Maradhi Tumboni.

Alishakwenda hospitali ya mulago Uganda wakamcheki na kumwambia kuwa hana tatizo,na wakamwambia kuwa maji ni kinywaji kisicho na madhara mwilini kabisa
 
RGforever na Barca naomba mnisaidie kwa pamoja.
Kwanza, kisukari kinasababishaje kiu ya Mara kwa Mara?

Yes Ni dalili Maana Solute(glucose) ikizidi mwilini unahitaji Solvent(maji) ku neutralize Ndo maana anakunywa Maji mengi...

Pili, ukiwa na uzito mkubwa kuanzia let say 80-90 ukawa unakunywa lita zaidi ya nne kwa siku, utapata madhara gani kiafya?
Naomba kuelimishwa.
MziziMkavu pita pande hii pia tafadhali

Cc: Fadhili Paulo

Kunywa Maji kiasi Hata Wataalam wanashauri Kwa Uzito Kama Huo Usipitishe Lita 3.5 kwa Siku ..

Kwahiyo ni vyema Ukanywa Maji si zaidi ya Hapo pia Maji yasiwe Tupu.. Yaan maji kama Maji Changanya Kidogo na Chumvi yawe kama Oral ili kubalance Ions za Mwili..

Wengine Wataongeza
 
Last edited by a moderator:
Basi huyo mdogo wako anakunywa kwa siku maji Lita 6 pasipo na kula chakula? Hebu mpeleke hospitali ukampime huyo mdogo wako. Huenda ana Maradhi Tumboni.

Ampeleke hospitali au amshauri kwenda hospitali? mwanaume/mwanamke wa miaka 45 ambaye hayuko hoi kwa ugonjwa anapelekwa hospitali?
 
Alishakwenda hospitali ya mulago Uganda wakamcheki na kumwambia kuwa hana tatizo,na wakamwambia kuwa maji ni kinywaji kisicho na madhara mwilini kabisa

Sasa ndugu, lengo hasa la kuuliza ni nini kama ameshahakikishiwa kuwa maji anayokunywa hayatamdhuru...
 
Sasa ndugu, lengo hasa la kuuliza ni nini kama ameshahakikishiwa kuwa maji anayokunywa hayatamdhuru...

No mkuu hapa ni jukwaa huru na ujue utaalam unazidiana,ndio maana nikaomba kupata ushauri wa ziada.
 
No mkuu hapa ni jukwaa huru na ujue utaalam unazidiana,ndio maana nikaomba kupata ushauri wa ziada.

Nimesema hivyo kwa sababu asilimia kubwa watashauri aende hospitali akacheki sukari... na kama alishaenda kucheki akaambiwa hakuna tatizo, then the solution must come from a different angle (like personal experience) if there is any solution out there. I wish you all the best.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom