Nini madhara ya kumeza maji yenye dawa ya meno?

Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
4,314
5,982
Wadau salama?

Mimi naomba kuuliza kama kuna madhara yanayoweza kutokea kama mtu kwa makusudi au bahati mbaya atameza maji yaliyochanganyikana na dawa ya meno kwa muda mrefu kama mwaka mmoja hivi?

Nauliza hivyo kwa sababu nina mwanafamilia wangu ambae miaka miwili iliyopita aling'oa meno mawili ya nyuma. Baada ya kama miezi tisa hivi kila anapopiga mswaki kwa kutumia dawa ya meno anahisi kichefuchefu na hali hiyo kupelekea kutaka kama kutapika na hivyo sehemu ya maji yanayokuwa bado kinywani kushuka kooni huku yakiwa na sehemu ya hiyo dawa ya mswaki.

Hali hii imedumu kwa takribani mwaka mmoja na utokea pale tu anapopiga mswaki kwa kutumia dawa na asipotumia dawa tatizo linakuwa halipo.Tulimshauri abadili aina ya dawa na akafanya hivyo lakini tatizo bado liko palepale.

Kwa wenye uelewa je ni nini inaweza kuwa imesababisha hali hii na pia ni yapi madhara ya kumeza dawa hizi kwa kipindi kirefu kama hicho?

Je, umezaji wa dawa hizo hauwezi kuathiri mapafu na kuleta matatizo kama Pneumonia n.k?
 
Back
Top Bottom