Nini maana yake?

tbl

Senior Member
Mar 29, 2011
116
41
Habari WanaJF,
nina rafik yangu {wa kike} alikuwa na mpenziwe.kuna siku jamaa alimpigia simu binti akidai eti yupo nyumba ya kilokole kwa hiyo wasiwasiliane kwa njia yoyote asibip asimtumie message wala asimpigie mambo yakawa hivyo.Siku moja jamaa akampigia binti simu, sasa binti akawa ameweka wimbo wa lofa kama caller tune jamaa alipousikia akamwambia bibie "ina maana unanambia mie lofa,!basi mie nawe uhusiano mwisho leo"na kweli wakaachana hivyo.swali langu, inawezekana sababu kweli ilikuwa wimbo tu?
 
Hayo mazingira ya kukatazwa kupiga, kutuma sms afu siku anapiga anakutana na lofa sio mchezo.
 
Shida ni kuwa, tangu wanaanza mapenzi yao hawakuwekana wazi kuwa ni temporary relationship. Na hili ni tatizo letu kubwa sisi watanzani, hatupendi kuambiana ukweli. Ndiyo maana hata ifikapo wakati wa kuachana, badala ya kuambiana vizuri tu kuwa tayari tumechokana naomba tuishie hapa, utakuta mtu anategeshea kijisababu cha kijiinga!
 
Back
Top Bottom