Nini Maana ya Ugonjwa Wa Autism?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,295
33,079
Autism



Autism ni tatizo la kiroho na kihisia linalotokea kwa watu tangu utotoni na kuathiri uwezo wao wa kuwasiliana na watu wengine. Watu wenye matatizo ya autism hawaonekani kama watu wa kawaida. Muda mwingine hawapendi kuwaangalia wengine pale wanapozungumza nao, au hawapendi kushirikiana mambo mengine na watu wengine. Pia, hawapo vizuri katika kimawasiliano. Muda mwingine wanakuwa

hawawezi kuongea, au kuzungumza na watu wengine. Mwishoni, hujijibu wao wenyewe. Wanaweza wakawa na shauku na kitu ambacho mtu mwingine ambaye hana matatizo ya autism asifikirie kama kina umuhimu. Mtu mwenye tatizo hili anaelekea mara nyingi kurudiarudia matendo kadhaa, na anaweza kuhofia vitu katika mazingira yake yasiyoelewka kama tatizo na wengine.

Dalili za autism


Kukaa peke yake
Mtoto wa kawaida asiye na autism huwaangalia watu wakizungumza, hutazama wengine usoni, hutabasamu, na huwa na shauku na watu wengine. Watoto wenye autism, wanaweza kupenda vituvitu zaidi kuliko sura au watu wengine. Wanaweza wakatazama usoni kwa

sekunde tu, halafu mara moja akageuka. Wanaweza wasitabasamu, au wanaweza wakatabasamu kwa kitu kile alichokipenda.

Watoto wenye matatizo ya autism huwa na kawaida ya kukaa wenyewe tu, bila kuwepo kwa wengine. Wanaweza wasiwe na shauku ya

kutaka urafiki na mtu yeyote. Pia, wanaweza wasiwe wanafanya kawaida kama kukumbatiana na alama nyingine za upendo kwa wazazi wao. Hii haimanishi kama hawa wapendi wazazi wao, ni kwamba hawajui namna ya kusema hivyo vitu.

Wanaweza wasione hisia za watu wengine; kwa mfano, wanaweza wasione tofauti kubwa sana kati ya labda mzazi ana furaha ma ana uzuni. Wanaweza wakacheka na kulia kwa mara zisizoeleweka.


Kutozungumza
Mtoto mweye autism anaweza asithubutu kuongea, maana, au kujaribu kuelewa maongezi kati ya mwenzie mwenye umri sawa. Kuna baadhi yao huwa hawaongei kabisa. Wengi wao hawawezi kuongea vizuri na watu wengine.

Kufanya vitu tena na tena zaidi
Kuna baadhi ya maautistic hutumia muda mwingi kufanya vitu vimoja kwa mara nyingi na nyingi zaidi, au kuwa na shauku na vitu ambavyo si vya kawaida; kuna baadhi yao wanaweza kutumia muda mwingi kwa kujizungushia mkono wake, kutembea na visanamu vyao, au

kuvipnga vitu kwa mpangilio mmoja. Watu wenye matatizo ya autism wanaweza wakatumia muda mkubwa kwa kupanga visanamu vyake kwa mstari mmoja au vyumbavyumba na wanaweza kusikia jazba pindi mtu akavivuruga pale katika eneo lake.

Baadhi yao hawataki badiliko lolote lile, na wanaweza wakafanya mambo yaleyale kila siku bila kubadilishakama vile kuto kula, wanapokula, wanavaa, wanapiga mswaki, au pale wanapokwenda shulehuwa na uzuni kama kuna badiliko lolote katika vitu hivyo. Pia, wanaweza wakawa na shauku na vitu vya ajabu na kutumia muda wao mwingi kujifunza vitu hivyo.


Historia
Autism lilipewa jina kwa mara ya kwanza mnamo 1943. Leo Kanner alifanya utafiti huu kwa watoto wapatao 11 na akagundua vitu ambavyo si vya kawaida kuhusu wao. Aliita early infantile autism. Muda huohuo, daktari mwingine, Hans Asperger, akafanya utafiti mwingine karibuni kitu sawa. Alichogunda sasa kinaitwa Asperger syndrome, wakati alichogundua Leo Kanner kinaitwa autistic disorder, childhood autism, infantile autism, au tu autism.
 
Hakuna dawa zaidi ni kumpeleka mtoto mwenye autisim kwa occupation therapist afundishe kazi za kufanya ili kumjenga kiakilu
 
Kuna jamaa mmoja alichemka kazi sehemu kaamua kuwa balozi wa huu ugonjwa ,nahisi at a yy anaumwa hii kitu
 
tufanyeje wenye watoto wa aina him?
Kama nimechelewa kukujibu kama mdau alivyokujibu hapo juu. Yakupasa kumpeleka mtoto kwa watu wa occupational and physical therapists watamsaidia sehemu kubwa sana hata kama hataweza kurudi kwenye normal kabisa lakini angalau atakuwa mtu miongoni mwa watu. Tatizo la language pia linatibika japo si kwa dawa ila na mtu anayeitwa language therapist.
 
nahitaji unielekeze nifanyeje maana nina mtoto ana tatizo hilo na ana umri wa miaka mitano sasa na haongei ni kama bubu
Kama nitakuwa nimechelewa sana kukujibu nenda /mpeleke mtoto kwenye Kituo cha watoto /watu wenye mtindio wa akili hao wengi wanakuwa na huduma za occupational and physical therapy. Kwa umri wa miaka mitano bado haujachelewa sana atakuwa okay kabisa. Kwa ifakara kuna Kituo kinaitwa Bethlehem ni cha kanisa katoliki kipo vizur sana. Kuna wanafunzi waliolelewa hapo then badaye tukaungana pamoja shule ya msingi tukamaliza walikuwa okay japo wengi wao walikuwa na mental retardation.
 
Wataalam wanasema kwamba, tusiseme ugonjwa. Hii ni hali inayompata mtoto eitha akiwa tumboni au akiwa anakua na huja kuonekana mtt akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu.

So kiufupi nasema si ugonjwa kwakuwa utaratibu wa kuwasaidia huwa hauinvolve dawa. Ni kumfundisha tu.

Na wengine huwa vizur kuliko binadamu ambaye hajawah pata hali hiyo..

Kwahiyo kama una mtt wa aina hiyo Mshukuru Mungu tu. Si jambo baya iq zao pia huwa juu zaidi na wanaweza kuperfom katika viwango vya juu kuliko unavyotegemea katika fani flan atakayoichagua kwakuwa akikipenda kitu hukipenda hasa na asichokipenda hawez kukipa umuhimu hivyo humsaidia kuwa makini na vitu vichache na kuvifuatilia sana
 
Asante sana mtaalam nilipata kuona kwenye youtube mngonjwa mmoja wa hiyo autism alikuja kuwa na kipaji cua kuchora hatari tupu, yaani anatisha. Mjengo kama ile Ikulu yetu anaangalia dk 10 halafu anaomba karatasi,baada ya masaa anakuwa amemaliza. Ila wanasema hajapona bado. Mtafute youtube stephen Wiltshire. Kama ana tatizo kama hilo basi Mungu ni wa ajabu sana
 
Back
Top Bottom