Nini maana ya kuwa au kuitwa Baba?

Sipo

JF-Expert Member
Jul 25, 2008
2,139
91
Nimekuwa najiuliza nini maana ya kuitwa au kuwa Baba?
 
Nimekuwa najiuliza nini maana ya kuitwa au kuwa Baba
Je, ni kuzaa mtoto au watoto na kuingia mitini na kumuacha Mama akitaabika?
Je, ni kuzaa mtoto au watoto na kuwalea kwa pamoja na Mama (Mke)?
Je, ni kuzaa uko mtaani kwa wanawake tofauti na kujitangaza kidume kwa kuwa umeweza kuzaa na wanawake tofauti?

Nimeweka hii mada hapa kwani nina mshikaji wangu ambaye Baba yake baada ya kuzaa na Mama yake walitengana na mshikaji kukulia kwa ndugu wa Mama na Mungu saidia amesoma mpaka chuo. Sasa ndugu wa Baba wanaanza kumfuata na kumwambia mjali Baba yako, maisha yake sio mazuri kwa sasa vinginevyo utapata laana kutoka kwa Baba yako. Halafu kumbuka mshikaji toka chekechea hadi anamaliza chuo mwaka jana hajawahi kukutana na Baba yake. Ila msimamo wa mshikaji yeye ni kuwa kwa mateso aliyopata kwa kuishi kwa ndugu mara uku mara kule halafu uishi kwa uhuru kama nyumbani vile kumemfanya amchukie Baba yake na anasema kamwe hamfikirii hata kidogo kwenye maisha yake. Ameamua ni yeye na Mama yake na ndugu za Mama yake Kwani ndio wanajua uchungu na mateso ya kumlelea mpaka hapa alipo leo.

Ndugu yangu sipo;kabla sijachangia mada hii naomba msaada yafuatayo:

nini chanzo cha kutengana na kutelekezwa kati ya wazazi wake?
 
Kuzaa kunampa mzazi wajibu/majukumu ya kutimiza kwa mtoto. Yaani anapaswa kumlea mtoto hata kama wameachana na mama ya mtoto. Mtoto ana haki ya kupata malezi ya kimwili na pia ya kiutu. Kumbe uzazi (ubaba) ni wajibu: iwe ni katika ndoa au nje ya ndoa.

Kuhusu yule kijana aliyetelekezwa na babaye, bado ana wajibu wa kumheshimu baba yake na kumpenda hata kama mzee yule alikosea. Kijana hana sababu ya kulipa kisasi kwani yule ni baba yake tu hata kama hakuwajibika inavyotakiwa. Kamzaa kimwili, wana umoja wa damu. Ni tunda la baba yake.

Kwa sababu hiyo, mzee yule akiwa katika shida kubwa ya mahitaji ya maisha kijana bado anatakiwa kumsaidia. Msaada wa mtoto kwa mzazi si malipo ya yale wazazi wetu waliyotundea bali ni wajibu wetu kwao (hata vitabu vya dini vinahimiza). Kumbe kumtunza baba mzazi si lazima kutokane na yeye kukutunza mtoto. Si biashara ya kutendeana. Ni wajibu wa kila mmoja kwa wakati wake. Kumbe kijana amsaidie yule mzee katika uzee wake ikiwa yuko katika hali ya kutaka kusaidiwa.
 
Namshauri kijana hivi,kwanza hapo laana haipo ila ushirikina waweza kufanywa. kama huyo jamaa anaweza kumsaidia mtu ye yote hata asiyemjua basi hata baba yake amsaidie. La muhimu ni hili,amfuate baba yake kwa siri,ili azungumze naye kwa kirefu,pengine baba yake anaweza kumpa ukweli wa mambo na yeye akajua mwanzo mpaka mwisho.hapo atakuwa amejiongezea credit kwa jamii na baadae peponi( kama anaamini pepo).
 
Na mshauri huyo jamaa amsamehe Baba yake.ni kweli mzee wake alimtekeleza bila matunzo yoyote,kiubinadamu kama mshikaji anajiweza amsaidie baba yake asahau yote yalio tokea huko nyuma.na kwa kufanya hivyo Mungu atambariki sana,na hiyo ni fundisho kwa wanaume wanao wakataa watoto wao au kuwategeleza.nadhani huyu mzee hakuwahi kufikiria kama ipo siku atakuja kuomba msaada kwa huyu jamaa.Ya Mungu ni mengi jamani.
 
Nimeuchukua ushauri wenu wadau pamoja na kwamba mada haijachangiwa na wadau wengi. Na madhara ya michango michache ni kuwa ushauri huu ukiusoma kwa makini umeelemea upande wa baba wa mshikaji kusamehewa na kufaidi matunda ambayo hajui uchungu wake zaidi ya raha na utamu wa siku ile aliyopiga game na mama wa mshikaji ujauzito wake ukatungwa. Nway i will take it but as far as the post bado haijawaha closed please tuendelee kumpa mshikaji maushauri
 
Ndugu yangu sipo;kabla sijachangia mada hii naomba msaada yafuatayo:

nini chanzo cha kutengana na kutelekezwa kati ya wazazi wake?

Pointi!... wazazi wengi wakishaachana wanatabia ya kujivutia kamba upande wao... huenda mzazi mmoja (mama hapo) alifanya kila liwezekanalo kuhakikisha mtoto hana mawasiliano tena na babake. Matokeo yake mtoto anakua kwa akili baba hamjali, kumbe mama ndiye alikata mawasiliano yote!

Ugomvi wa wazazi mtoto haumhusu, la busara ni huyo Bw.mdogo kuwasiliana na baba yake, atimize majukumu machache atayojaaliwa kwa baba yake. Sio kwakuwa eti hakuwahi kuona 'huduma' toka kwa baba yake halafu naye akaamini ndivyo ilivyokuwa.

"Two wrongs doesnt make one right!"
 
Nilishawahi kuongea na mshikaji sababu ya mafarakano ya familia yao akasema nachofahamu yeye ni kuwa baada ya kuzaliwa yeye dingi yake aliamua kuoa mwanamke kwa sababu ambazo hata kwa mujibu wa ndygu zake wengine zilisababishwa na huyo dingi kuamia DSM na kumpata mwanamama mwingine ndio akatoa go ahead kwa mama wa mshikaji. Kinachomuuma mshikaji ni kuwa hiyo familia nyingine aliyokwenda kuilelea baba yake ilikula raha sana watoto wakasoma raha mustarehe yeye akitupwatupwa huku na kule pasipo msaada mahususi
 
Nilishawahi kuongea na mshikaji sababu ya mafarakano ya familia yao akasema nachofahamu yeye ni kuwa baada ya kuzaliwa yeye dingi yake aliamua kuoa mwanamke kwa sababu ambazo hata kwa mujibu wa ndygu zake wengine zilisababishwa na huyo dingi kuamia DSM na kumpata mwanamama mwingine ndio akatoa go ahead kwa mama wa mshikaji. Kinachomuuma mshikaji ni kuwa hiyo familia nyingine aliyokwenda kuilelea baba yake ilikula raha sana watoto wakasoma raha mustarehe yeye akitupwatupwa huku na kule pasipo msaada mahususi
Kibinadamu hali hiyo inaumiza moyo. Lakini hata hivyo ukweli unabaki palepale: kwamba mwingine kutotimiza wajibu kwako hakukuondolei wewe jukumu la kutimiza wajibu wako kwake. Baba alikuwa na wajibu wa kumtunza, lakini hakufanya hivyo. Akatunza wengine. Leo hii mtoto (kijana) amekuwa mtu mzima ana wajibu wa kumtunza (au kumsaidia) baba yake. Anapaswa kutimiza wajibu huo. Hawezi kusema kwa kuwa baba hakumtunza naye hatamsaidia. Ni makosa! Kwani wajibu wake kwa baba si malipo kwa mema alivyomfanyia. Ni wajibu wa kiutu na kimaadili. Tena kijana akifanya hivo atapata baraka tele kutoka kwa Mungu, na pia litakuwa somo chanya kwa wazazi wengine wanaotelekeza watoto wao
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom