Nini maana ya huu msemo?

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,711
12,067
Unakuta mtu anasema mfano:-

Serikali kama serikali,,,
Madactari kama madaktari?

Waziri kama waziri? nk

Mtu huyu huwa anakusudia kusema nini?
 
Ninavyoelewa mimi serikali kwa mamlaka iliyokuwa nayo inapaswa kufanya kadha kadha kadhaa! Na si vinginevyo! Waziri kwa mamlaka aliyokuwa nayo kisheria na si kama yeye binafsi! ('mfano; waislamu wamepokea sadaka ya bati za kujengea msikiti toka kwa waziri mkuu alipokuwa ziarani...., hapa waziri kama 'mizengo' katoa msaada kwa waislamu wa bati. Na si waziri kama wajibu wa uwaziri wake ni kuwapa waislamu sadaka ya bati.') sijui kama nimeeleweka!
 
Ni misemo tu ya kuwapumbaza wasikilizaji waache kuzingatia hoja ya msingi iliyo mezani, lakini haina umuhimu wala haileti maana yoyote. Ni sawa na mtu anayesema "kwa niaba yangu binafsi"
 
Mtu akisema: Waziri kama waziri hatakiwi kulala na Changudoa. Anamaanisha: Waziri(Mtu binafsi) kama waziri(Hadhi yake) hatakiwi kulala na changudoa. Huo ni mfano tu.
 
Mimi kama mimi, yeye kama yeye nk - yote ni misemo ambayo nadhani haina sababu ila imejiingiza tu katika lugha!
 
Back
Top Bottom