Nini Maana Halisi ya Kauli ya Mh. S. SITTA ya SISI tunatumia AKILI siyo TUMBO ?

Kikarara78

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
1,495
901
Habari zenu Great Thinker,
Naomba kujua hasa nini maana ya hii kauli ya Mheshimiwa Sitta aliyoitoa Mbeya kuwa wao waliokuwa kwenye Mkutano, Kongamano wanatumia Akili na siyo tumbo ?? Ana maana kwenye Chama chao cha CCM na Serikali wengine wote wanatumia tumbo kufikiri na kutoa maamuzi ?? Hata Kiongozi wetu wa Nchi nae anatumia tumbo ???? Maana Rais wetu akuwepo Mbeya.

"Nawapa matumaini katika chama chetu kuwa sisi mnaotuona hapa ndio tunaotumia akili siyo tumbo katika kufikiri, hivyo chama chetu kitakwenda vizuri,"aliongeza Sitta.

Tuzidi kuombea Nchi yetu maana Viongozi wetu na kauli zao zinatutatiza sisi Wananchi
Nawakilisha

Source: Mwananchi - Sitta amkaba koo Ngeleja , ATAKA WALIOSABISHA MGAWO WAWAJIBISHWE
 
Du simple tu wanayotumia matumbo ni wale waliyotufikisha hapa tulipo kwenye mikataba mibovu ya ten % richmond then dowans then symbion wapo viongozi ccm wazuri sana ila chama kina misingi yange ukiwa nje utaona uozo mwingi sana ukishaingia kila utakachotaka kiwekwe sawa ni cha mkubwa fulani na ukitaka kukiona cha moto ifwatilie vizuri utapata hata ajali ya kugongwa na bajaji
 
Sijakataa hilo wala kubisha, hoja yangu ni kuwa ni sawa kusema ni wao tu ndio wanaotumia AKILI ??? Alikuwa au walikuwa wapi miaka, muda wote huo mpaka waone mambo yanakwenda kombo, hovyo ndio waje na Kauli hii ???
 
Kwamba wao ni wasafi kama maji ya Zamzam!!! Hawajawahi hata kuionja raha ya rushwa!!! Sita aliuwa pale TEC... hawa wawekezaji wengi tunaowapigia kelele ryt now waliingia kipindi chake!! anataka kutuaminisha kuwa yeye (wao) wanaishi maisha tunayoishi sisi!! La hasha... Masaki sio kama kwa MTOGORE....wala hakuna kiongozi ambae anaishi kama tunavyoishi sisi!!! All these are 2015 visions and Missions!!!
 
Sijakataa hilo wala kubisha, hoja yangu ni kuwa ni sawa kusema ni wao tu ndio wanaotumia AKILI ??? Alikuwa au walikuwa wapi miaka, muda wote huo mpaka waone mambo yanakwenda kombo, hovyo ndio waje na Kauli hii ???

Hizo ni lugha za kisiasa,wanajaribu kuwashawishi wananchi kuwa CCM bado inawatu wanaofikilia kwa kutumia AKILI.Na hivyo wanawaambia umma kuwa kuna viongozi waliotanguliza kuendesha maisha yao ya kutawala kwa kuendesha NJAA zao hivyo kuzingatia zaidi katika kuchuma kwa ajili ya matumbo yao.
 
Jamani kampeni za urais 2015 zimeshaanza, Sitta alishasema yeye ni "presidential material" hivyo kazi imeshaanza, kama siyo kupitia CCM basi wanafufua CCJ yao, si mmeona wenyewe line up yao, typical CCJ.
 
Yes alimaanisha hivyo kuwa hata rais wake anatumia tumbo kufikiri na ni kweli.Lakin hata yeye mwenyewe ameshaambukiza hicho kirusi.
1.Alikuwemo kwenye baraza la mawaziri ambalo lilituletea rasimu ya katiba ambayo inaonyesha waliyoiandaa walitumia matumbo na si akili.
2.Baraza la mawaziri akiwemo Sitta wanatumia matumbo kutatua mgogoro wa umeme. Sasa yeye ametumia akili kwenye lipi hasa?Naishìa hapo kwa sasa.
 
Daima binadamu(mwanaume) hasahasa tunavchwa viwili cha juu na chini sasa hawa wenzetu magamba wanafikiria kwa kichwa cha chini.
 
Kinyume chake yaani! kwamba wanafikiria matumbo tu. Ukitaka kujua nguvu ya mlevi mwaga pombe yake! Ukitaka kujua nguvu ya 6 pinga posho bungeni, atakuambia na wewe rudisha posho ZOoote ulizowahi kupokea hapa bungeni miaka iliyopita.
 
Habari zenu Great Thinker,Naomba kujua hasa nini maana ya hii kauli ya Mheshimiwa Sitta aliyoitoa Mbeya kuwa wao waliokuwa kwenye Mkutano, Kongamano wanatumia Akili na siyo tumbo ?? Ana maana kwenye Chama chao cha CCM na Serikali wengine wote wanatumia tumbo kufikiri na kutoa maamuzi ?? Hata Kiongozi wetu wa Nchi nae anatumia tumbo ???? Maana Rais wetu akuwepo Mbeya."Nawapa matumaini katika chama chetu kuwa sisi mnaotuona hapa ndio tunaotumia akili siyo tumbo katika kufikiri, hivyo chama chetu kitakwenda vizuri,"aliongeza Sitta.Tuzidi kuombea Nchi yetu maana Viongozi wetu na kauli zao zinatutatiza sisi WananchiNawakilishaSource: Mwananchi - Sitta amkaba koo Ngeleja , ATAKA WALIOSABISHA MGAWO WAWAJIBISHWE
Yeye mwenyewe huyo Sitta anafikiri kwa kutumia tumbo. Wanaofikiri kwa kutumia akili wapo Cdm kasoro Shibuda.
 
Yeye Sitta na Mwakyembe ndiyo wanastahili kuwajibishwa, Sitta alilizima sakata la Richmond kihuni habla Serikali haijatekeleza maazimio ya bunge kuwawajibisha wote waliohusika, na Mwakyembe kwa kinywa chake alikiri kuwa kamati yake ilificha taarifa muhimu kwa kile alichoita kulinda heshima ya serikali.Hawa ni wanafiki wakubwa walifanya waliyofanya kwa kushirikisha matumbo yao badala ya akili zao, magamba ni magamba tu kamwe hayawezi kuwa ngozi.
 
Haya yote yanaambatana na matukio yake ya kuumwa kwa Dr. Mwakyembe ??? wabaya wake ???
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom