Nini maama ya vidole viwili (The 'V' sign)?

Vidole viwili vina ashiria alama ya V ikimaanisha Victory kwa kiswazi ni Ushindi
 
Bunge letu likipata nusu ya wabunge kutoka upinzani, uendeshaji wa nchi utabadilika kwa manufaa ya kila mwananchi, kwani ongezeko la wabunge wa upinzani katika uchaguzi uliopita imewafanya wabunge wa ccm waamke kutoka usingizini na kufanya kazi iliyowapeleka bungeni, mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio haambiwi sikiliza. Kazi kwenu wapiga kura wa Arumeru mashariki.
 
Juzi hapa nilisoma gazeti fulani hivi lenye madai kwamba alama ya vidole ya "V" inayotumiwa na CDM ni alama ya Freemasons na kwamba Freemansonry ni dini ya kumuabudu Shetani. Binafsi nadhani huu ni upotoshaji wa mambo. Isipokuwa, kabla ya kuhitimisha, naomba michango yenu juu ya hadidu zifuatazo: -

a) Je, ni kweli kwamba alama hiyo ya "V" ni ya Freemasons?

b) Je, ni kweli kwamba Freemasons wanamuabudu shetani?

c) Endapo jibu la hadidu (b) ni "Ndiyo", je, kuna ushahidi wowote?

Ahsanteni wadau.

Watababu,

Mwonambali
 
Siyo kweli,alama ya v ilitumiwa na waziri mkuu wa uingereza winston churchill akimaanisha victory katika vita vya pili vya dunia.
Nawasilisha
 
(a) si kweli kuwa alama ya V ya chadema ni ya kifreemarsons (b) ni kweli freemarson wanahusishwa na dini za mashetani,
 
sa hivi kila kitu kizuri kimehusishwa na free masson. wanadamu temegeuka kuamini kuwa, hakuna mafanikio bila kuwa member wa free masson. hii ni hatari.

lakini kama ni ya kweli, kuwa free massoni ndo ma in charge wa teknohama, hakuna kifanyikacho bila idhini yao katika tasnia ya habari na mawasiliano. nani siyo mwanachama wa free mason?
 
Habari za freemason ni deep and complecated,zinahitaji utafiti na zipo tafiti nyingi zimefichua in and out,purely freemason ni devil worshippers,kwa nje ni kama taasisi ya watalaamu na watu mashuhuri lakini inside wana ibada za makafara za ajabu sana,kama alama V ni yao,no way tunaweza kuikataa hata kama tunaipenda chadema namna gani,mwenye katiba ya chadema atuwekee sehemu inayoelezea maana ya nembo yao,then tutajadili critically zaidi
 
Siku hizi kuna 'society' ambayo inadhani inajua kila kitu, kwa hio kila kitu kinachowachanganya kimetokana na freemasons, kujifunza ukweli chimbuko, maana, sababu hawataki wanapenda stori nyepesinyepesi. Ndio kizazi kilichorithi uchawi, enzi za huko nyuma, hii 'society' kila tajiri, kila aliekufa, alkuwa 'amelogwa'. Sasa kwa hii wamehamia kwa freemasons, ni namna ya kujiliwaza na uvivu wa kufikiri.
 
Sasa mkuu unataka kuniambia kuwa chama hiki kimejikita kwa hao devil worshippers?

Na je ndiyo sababu wanamvuto sana machoni pa watu?

Na je sera zao ambazo nakumbuka kabisa mwaka 1992 Mwl Nyerere alipoulizwa juu ya vyama vingi alisema wakati huo vilikuwa kama 13 hivi (sina hakika sana na idadi) ' kama ningekuwa nataka kujiunga na chama pinzani basi ningejiunga na Chama cha demokrasia na maendeleo' na alitoa sababu kwamba sera zake ndizo zilizo mvutia kwani ni nzuri. sasa mm nakuuliza au niulize wana jamvi je ni hao freemanson walikuwa wamempatia Edwin mtei hizi sera?

kwakweli nisaidieni manake sijui nielewe nini.
 
Ninachoamini Freemasonry wapo na wanaendesha ibada zao za kishetani kwa siri ya hali ya juu sana, cha msingi ni kueleweshwa hii alama V ambayo niliitafsiri kama alama ya ushindi, itakuwa njema kama CHADEMA watatusaidia kujua V inawakilisha nini?

Kwanini kumsifu shetani ndiye mwenye kufanya mazuri na si MUNGU WA MBINGUNI kwani alishasema nitawafanya kichwa na si mkia kwanini iwe hivi kwa CDM kuwa hakuzwi na MWENYEZI MUNGU.
 
Alama ya V ni alama ya ushindi,amkuona ata makamanda wa Libya walikuwa wanaitumia,sasa hiv ukiwa na pesa au maendeleo tanzania,waliopigika na maisha watakuita freemason,acheni majungu tanzania fanyeni kazi usitegemee ukae kijiweni harafu upate maendeleo,tuache uvivu wa kufikiri na majungu
 
Back
Top Bottom