Nini kinakurudisha kwa mkeo?

sina hakika kama wanandoa wa sasa yaani wanaozaliwa late seventeens na early eighties watakubali tena ujinga huo. ndoa unazozungumzia wewe ni zile wa wakongwe wa miaka ya sitini na sabini ya mwanzoni na kabla ya hapo. Kwa kifupi mama zetu. tatizo lilikua ni kukosa elimu ya kutosha na kudhani kua ukiwa kwenye ndoa huwezi kuondoka bila kupewa talaka. mume anapotea miaka kadhaa, anapata machungu huku aliko halafu anarudi kwa mkewe, na anapokelewa. kama ndoa yako ni ya karibuni, hebu ondoka japo mwezi tu bila taarifa, uone kama utapokelewa. Labda kama mkeo umemtoa kijijini.

Sal, una maana elimu imebadilisha mtazamo wa wanawake?
 
Last edited by a moderator:
Kongosho,
umehangaika na watoto zaidi ya miaka 12,
umeona rangi zote za maisha,
mwaka wa 12 jamaa anarudi (anakuja kwako hii ni kwa kuwa hata house ulimwachia hata mifugo na kila kitu ulikiacha) na bonge la kisukari na maradhi yote yamejimix humo humo,
mimi nasema hivi SIMPOKEI
Tena mimi ni mzee wa Kanisa ila simpokei.

hata akija kachakaa kwa ugonjwa anahitaji kupikiwa uji tu utamtimua? Ila wanaume hawana haya, nyumba mlojenga wote kakutimua ukaanza mwanzo leo anarudi mikono mitupu bila hata kandamnili..... Natamani kweli mwanaume aniambie vichwa vyao vinaingiwa na mdudu gani...
 
habari zenu wapendwa,

binafsi hili ni swala ambalo nimeliona likitokea ila sijalipatia jibu. Sijui kama lilishajadiliwa humu au la na kamchina kangu hakawezi kusearch.....

Ni hivi inakuwaje kwa wanandoa, hususan mwanaume anatelekeza familia yake miaka kadhaa, hata kumi..... Ila akishafika uzee/utu uzima anarudi kwa mkewe?

Na inaiuwaje mke, mume anaporudi miaka kumi-ishirini baadae unampokea? Na mnaendeleza gurudumu?

Saa nyingine mume akiumwa hoi hoi hurudi kwa mkewe na mke huyu humuuguza mkewe?

Wanaume nini kinawaondosha kwa wake zenu? Na ninu kinawarudisha?

Wanawake mnawaza nini mnapowapokea tena waume zenu? Nini kinawasukuma kuwapokea?

Je hili lina madhara gani kwa watoto? Haiwaadhiri? Huwajenga au huwabomoa?

Natarajia majibu toka kwenu........

Hapo kwenye blue hapo!! kama sijapaelewa hv?!.
 
Hii mada ni ngumu sana kwa upande wa wanaume...

Nimesoma michango ya Kongosho....Ni bonge la uzoefu.

Ni jambo gumu kulielewa hadi yakukute.

Ila pia naona kama si vizuri tujumuisha wote kwenye kapu la watu wachache wanaofanya mambo ya ajabu kama hayo!

Babu DC!!
 
Dark City .... Pole kwa kujumuishwa....
Ila hia nilitaka nijue ni nini haswa kinatokea kwenye kichwa cha mwanaume mpaka anatelekeza familia yake na nini kinamsibu anarudi.....

Na uzoefu kutoka kwa wanawake pia....... Kongosho ameelezea vyema nashukuru, bado nasubiria wengine wenye uzoefu tofauti...
 
Last edited by a moderator:
loh....
Nimeamini ndoa ngumu..... Na inahitaji haswa mkono wa Mungu.... Na nashukuru Kongosho umenifungua macho haswa....

Ila nashangaa Asprin ruttashobolwa Bishanga nitonye Judgement Erickb52 Dark City Mbu Mtambuzi na wengineo siwaoni hapa, waje kutueleza kinachowafanya kukimbia familia zao ni nini? Kwa nini wabadilika vichwa vyao vina nini humo ndani.......
Wanawake wana huruma nyie, acheni tu...
Kusema cha ukweli sina jibu la moja kwa moja kuhusu jambo hilo, lakini nitafamya udadisi na kuja kuweka hapa kile nilichokipata. Hata hivyo, Mzee mwenzangu Asprin, naamini ana uzoefu na jambo hili kwani yeye ni mmoja wa victim aliyerejea zizini baada ya makasheshe ya nyumba ndogo, ngoja aje hapa atupe uzoefu wake......

Salama leko Mzee Asprin...LOL
 
Last edited by a moderator:
nimeshakutana na hizi habari kutoka kwa wamama watatu ambao wananihusu sana!!!
wawili kati yao walijaribu kuniambia sababu za kuwapokea....kwamba "si ni mume wangu jamani saa nitafanyaje?!?!"
sikuridhishwa sana na hii sababu.
nahisi kuna kitu kingine kimejificha kwenye hii kauli!!!

mmoja nilikuja kujua kuwa aliombwa msamaha wa dhati ....lkn kumbe tayari alishajua amenasa kwenye gridi ya taifa!!! na nyumba ndogo ilimkimbia kabisa!!! huyu aliuguza mpk akazika na kujengea kaburi!!

mwingine alimpokea akamwambia umerudi baba, karibu chumba hicho apo, akipika chakula anapewa etc. lkn haulizwi kitu!!! jibaba likalia sana sasa hivi katulia! bahati huyu hajagusa gridi!!

mwingine alipigiwa simu na huyuo nyumba ndogo kuwa mumeo yupo hospitali wadi no...! baada ya siku akafariki! tukaandaa mazishi!! huyu niligundua alimpenda sana mumewe maana alimlilia sana akisema alikuwa anampenda mpenzi wake mume wake, kwa nini alimkimbia!! looh ilisikitisha!

bado sijaelewa huwa inakuwaje?
wanakubalije kuwapokea hawa wanaume waliowatenda?
wana mioyo gani hawa wamama?
ni upendo kweli ama..............??!? mhh sijui!!!
kizazi chetu kitaweza kweli kuwapokea hawa?

jamani msiache mbachao kwa msala upitao!!!
 
Wengi wa wawanaume wa aina hii ni wale wabinafsi wakupindukia.
Wanatafuta pesa na mkewe, likipata pesa linaanza anasa na kumnyanyasa mkewe na kama haitoshi linamtelekeza mke na watoto. Nalinawasahau kabisa kama halikuacha kitu. linastarehe huko wee.
Sasa likisha firisika na linarudi.

Ngoma nzito linaporudi na maradhi ya kimurder, kwasababu nilibinafsi linataka na huyu mama aliyenyanyasika miaka yote bado liondoke naye kwa kumuambukiza maradhi yake.

Wanaume makatiri sana .lol!

Nakubaliana na wewe100%.. Imewai kumtokea babaangu mkubwa. Yeye alikua ni dereva wa magari makubwa akisafiri nchi kadhaa kupeleka mizigo,bahati nzuri mwanzoni mwa ndoa yeke alikua ni mtu mwenye malengo ya maisha akabahatika kujenga nyumba mbili nzuri,Moja alijenga katikati ya mji na nyingine pembeni kidogo. ya mjini ndio alikua anaishi na familia yake yenye watoto wadogo wawili ambapo mkubwa alikua ni miaka takribani mitano..sijui shetani gani alimpitia ndoa yake ikaanza kusumbua,familia yake ilikua mbeya alikua akitoka dar anapitiliza hadi zambia au Congo hivyohivyo akitoka Congo mpaka dar bila kuijulia hali familia yake..ikaja kungundulika baadae kuwa tayari anabi-mdogo zambia ambae anaishi nae kama mkewe. Mkewe baada kusikia hizo habari suku moja akamhoji. ikawa balaa,ulizuka ugomvi mkubwa sana... Siku moja mke hana hili wala lile alijikuta anaambiwa nyumba wanayoishi imeuzwa hivyo wahamie nyumba ya pembeni ya mji ambayo aliipangisha,na kumwambia kuwa hiyo ndio itakua nyumba yake hivyo wasijuane, mama mkubwa alijua utani, akashangaa miaka inakatika mmewe hakanyagi nyumbani,kuulizia jamaa zake wanasema yupo na anafanya safari zake kama kawaida ila mke wa Zambia ndio kama mkewe rasmi....amekuja kurudi mwaka jana huku akiwa amepooza upande mmoja wa mwili na kumpigia magoti mkewe kwamba anaomba msamaha maana huko Zambia bi-mdogo wametibuana, ni baada ya kuona jamaa anaumwa na hana uwezo tena wa kufanya majukumu kama awali akaamua kumtelekeza...baba mkubwa alirudi na kabegi tu kenye nguo chache huku hata hele ya kujiuguza hana....mke alijaribu kumkataa lakini vikao vya familia vilisaidia kumrudisha kwe mstari akakubali kumpokea kwa masharti kuwa atapewa chumba chake binafsi kama msaada huku familia ikichangishana kuhusu matibabu yake..mtoto aliemwacha na miaka mitano anarudi mwaka jana yupo kidato cha kwanza.!!
 
So sad. Ndio maana nasema hao dawa yao ni kuwatimua wauguzwe na ndugu zao.

Kama mama yake yuko hai akamuuguze...si alijifanya mjanja. Je angemkuta mkewe kaolewa?

Mkiama muwege na plan B. Na plan B yenyewe isiwe wife ulomtelekeza.

Wanawake wameumbwa na roho ya huruma..na wanapenda kusikilizwa hivyo ukijinyenyekeza kwa mkeo ni rahisi sana kusamehewa hata kama unakosa kubwa kiasi gani, ilimradi yeye aonekane ni mwenye maamuzi na maisha yako.!!
 
wala si uongo,najaribu kuvaa viatu vya mwanamke aliyepita hapo nahisi vinanibana kusema ukweli BT,mtu akuache uhangaike na watoto,utukanwe kuwa hujui kumridhisha mume,udharaulike kiasi cha kujiona hufai,unyimwe haki yako ya msingi ya ndoa kwa miaka kadhaa,na kisha anarudi ukiwa umeshajimudu,umesomesha watoto,umeanzisha miradi yako,yeye anarudi na magonjwa yake na bado jamii inasahau yote hayo unalazimishwa to take him back!eti ndio maana ya ndoa katika shida na raha!ni ngumu zaidi ya tunavyofikiri,unachosema kuwa unatamani aje mwanamke aliyepita hapa atuambie alimeza hilo kaa la moto vipi!

uwiiii nikipita kwenye huu uzi nalia aisee, nakumbuka mbali sana maisha aliyoishi mume wangu, baba yao alifanya the same aliondoka mume wangu akiwa na miaka 14 amerudi akiwa na miaka 37 sasa. tena watotowalimfuata kwamba baba iangawa umetutesa sana lkin hatupendi udhalilike rudi nyumbani tuishi. mama mkwe alimkaribisha baba tena na mpaka leo ni mwaka wa 4 yuko nyumbani.
 
Kama wanawake wana huruma si aende kumwangukia aloponda nae maisha??? Au yeye si mwanamke?

Ndio maana tunapenda wanaume wafunguke...wanaona ugumu gani kuwaangukia hao nyumba ndogo zao? Ni kipi kinachowafanya wapate ujasiri wa kurudi kwa wake zao macho makavu after so many years?

Wanawake wameumbwa na roho ya huruma..na wanapenda kusikilizwa hivyo ukijinyenyekeza kwa mkeo ni rahisi sana kusamehewa hata kama unakosa kubwa kiasi gani, ilimradi yeye aonekane ni mwenye maamuzi na maisha yako.!!
 
Kama wanawake wana huruma si aende kumwangukia aloponda nae maisha??? Au yeye si mwanamke?

Ndio maana tunapenda wanaume wafunguke...wanaona ugumu gani kuwaangukia hao nyumba ndogo zao? Ni kipi kinachowafanya wapate ujasiri wa kurudi kwa wake zao macho makavu after so many years?

Familia nyingi za kiafrika tunaamini kuwa mke wa kwanza anaheshima na maamuzi ya busara.ndio maana hata ukikuta mwanaume mwenye wake wawili mara nyinyi mke mdogo ndio huwa mkorofi, sababu yeye anaamini hasikilizwi hathaminiwi eti kisa mke wa pili, hata kama bwanaake unampendelea kuliko bi mkubwa..mabi-mdogo hawajiamini na ndio wenye vitimbi kwenye mahusiano. Hivyo hapa nazungumzia mke wa kwanza.
 
Wanawake wana huruma nyie, acheni tu...
Kusema cha ukweli sina jibu la moja kwa moja kuhusu jambo hilo, lakini nitafamya udadisi na kuja kuweka hapa kile nilichokipata. Hata hivyo, Mzee mwenzangu Asprin, naamini ana uzoefu na jambo hili kwani yeye ni mmoja wa victim aliyerejea zizini baada ya makasheshe ya nyumba ndogo, ngoja aje hapa atupe uzoefu wake......

Salama leko Mzee Asprin...LOL

nasubiria udadisi wako, unaweza kuwasaidia wengi.....
 
Last edited by a moderator:
BADILI TABIA naomba nikupe jibu ambalo lilitoka kwa mtu ambaye ninamuheshimu sana maishan mwangu juu ya mkasa kama huu.

yeye alisema ingawa nimefwatwa na wanangu ili nirudi nasema wazi si kwasababu yenu nimerudi il nikwasababu sijawahi kuona upendo kama niliokuwa nauona hapa nyumbani kwangu, sijawah kuthaminiwa kama nilivyokuwa nathaminiwa hapa na istoshe sijawah kupata furaha toa niondoke nje ya hili geti.

alihitimisha hivi you might be the source of fire but the ignition comes from me. to me naamin hizi ndizo sababu ukiongeza na hayo alosem Kongosho hapo nyuma.
 
Last edited by a moderator:
nimeshakutana na hizi habari kutoka kwa wamama watatu ambao wananihusu sana!!!
wawili kati yao walijaribu kuniambia sababu za kuwapokea....kwamba "si ni mume wangu jamani saa nitafanyaje?!?!"
sikuridhishwa sana na hii sababu.
nahisi kuna kitu kingine kimejificha kwenye hii kauli!!!

mmoja nilikuja kujua kuwa aliombwa msamaha wa dhati ....lkn kumbe tayari alishajua amenasa kwenye gridi ya taifa!!! na nyumba ndogo ilimkimbia kabisa!!! huyu aliuguza mpk akazika na kujengea kaburi!!

mwingine alimpokea akamwambia umerudi baba, karibu chumba hicho apo, akipika chakula anapewa etc. lkn haulizwi kitu!!! jibaba likalia sana sasa hivi katulia! bahati huyu hajagusa gridi!!

mwingine alipigiwa simu na huyuo nyumba ndogo kuwa mumeo yupo hospitali wadi no...! baada ya siku akafariki! tukaandaa mazishi!! huyu niligundua alimpenda sana mumewe maana alimlilia sana akisema alikuwa anampenda mpenzi wake mume wake, kwa nini alimkimbia!! looh ilisikitisha!

bado sijaelewa huwa inakuwaje?
wanakubalije kuwapokea hawa wanaume waliowatenda?
wana mioyo gani hawa wamama?
ni upendo kweli ama..............??!? mhh sijui!!!
kizazi chetu kitaweza kweli kuwapokea hawa?

jamani msiache mbachao kwa msala upitao!!!

Paloma,
inasikitisha sana.....

Unamsamehe mtu, anakuja kukuambukiza maradhi!!!!!!!
Hapa unakua umeokoa nini? Ndoa? Na watoto kuwaachaje?

Hii inadhihirisha ubinafsi wa wanaume, hivi mwanaume ameathirika, anarudi kwa mkewe na anafurahia tendo la ndoa na kumuangamiza mkewe, ni mzima kweli upstairs?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom