Nini kinachomfanya Mzazi kufikia hatuwa hii?

Sonara

JF-Expert Member
Oct 2, 2008
726
68
Nimekuta habari hizi zimenisikitisha kiasi najiuliza maswali mengi bila ya kupata majibu, i lakini kuna swali moja bado limebaki najiuliza hadi hivi sasa Binafsi sijawahi kufika Bara nasikia tu kwa watu na mitandaoni lakini miongoni mwa sifa ambazo nazisikia ni hakuna ugumu wa kuchukuwa wanawake ukikohowa tu au kwa maana nyingi ukinyoosha mkono haurudishwi, sasa wakazi wa huko inakuwaje mtu kufikia hatuwa kama hiyo hapo chini?


Mahakamani kwa kumlawiti mwanawe
MKAZI wa Kata ya Nguvumali jijini hapa, Daniel Makundi (40), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tanga kwa tuhuma za kumlawiti mara sita mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 12.

Mtuhumumiwa Makundi alifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Ngasoma na kusomewa shitaka hilo.

Mwendesha Mashitaka, Wakili wa Serikali, Rebeca Mwongosso alidai kitendo alichofanya mtuhumiwa kinakwenda kinyume cha kifungu cha 154 cha Makosa ya Jinai.

Alidai kuwa Oktoba 22, mwaka huu saa moja usiku huko Nguvumali, mtuhumiwa alimwingilia kinyume cha maumbile mwanawe wa kiume (jina limehifadhiwa) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu.

Alidai mtuhumiwa amekuwa akimfanyia mwanawe kitendo hicho na amefanya hivyo zaidi ya mara ya sita hasa wakati anaporudi kutoka kilabuni kunywa pombe.

Hata hivyo, mtuhumiwa huyo alikana shitaka hilo ambapo shauri hilo limeahirishwa hadi Novemba 9, mwaka huu kwa kuwa uchunguzi haujakamilika.

Licha ya mahakama kuweka wazi masharti ya dhamana kwa mtuhumiwa, alikosa dhamana kwa kuwa hakuna jamaa yeyote aliyejitokeza kumdhamini na amerudishwa rumande.

Oktoba 24, mwaka huu, gazeti hili liliandika habari kuhusiana na kutiwa mbaroni kwa mtuhumiwa huyo baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Simon Sirro kuwaeleza wanahabari kuwa mtuhumiwa alikamatwa baada ya mtoto huyo kulalamika kwa polisi kuwa haridhishwi na vitendo anayofanyiwa na mzazi wake, hivyo kuiomba imsaidie
 
Back
Top Bottom