Nini kinachofanya JK asiteuwe RC mpaka leo??

Uchaguzi umeisha toka nov 2010,raisi yupo na cabinet yake kashaiteua, na wabunge wapo tayari.Je kwa nini mpaka leo hajateua wakuu wa mikoa?? au ndo mpaka akapige ramli mlingotini??

Wakuu wa mikoa wa nini wakati hawafai na hata wakuu wa wilaya hawa tija zaidi ya kuongeza gharama kwa serikali so let him delay.
 
Wadau kwani katiba,sheria inatamka baada ya muda gani toka uchaguzi awe ametangaza wakuu wa mikoa na wilaya!Je kuna ulazima wa kuwabadirisha kila baada ya uchaguzi?
 
Alikuwa kesha teua "wachumba" sasa aliposema Jenerali pale Nkurumah hall jamaa akachomoa bado anafikiri sasa hao wachumba waende wapi
 
Uchaguzi umeisha toka nov 2010,raisi yupo na cabinet yake kashaiteua, na wabunge wapo tayari.Je kwa nini mpaka leo hajateua wakuu wa mikoa?? au ndo mpaka akapige ramli mlingotini??

Hivi ni lazima kubadilisha wakuu wa mikoa wakati serikali ni ile ile? Angekuwa raisi mpya sawa, ila kwake ni yeye aliyewateua awali na walikuwa hawagombei ubunge.
 
Hivi ni lazima kubadilisha wakuu wa mikoa wakati serikali ni ile ile? Angekuwa raisi mpya sawa, ila kwake ni yeye aliyewateua awali na walikuwa hawagombei ubunge.
sio lazima ....sasa mikoa ambayo hawapo inakuwaje?
 
kuna uwezekano wa kuwa bado anaangalia ni akina nani walioboronga kwenye uchaguz ulopta ili awabebe.... miaka mitano ilopta alijaribu kumbeba henry shekifu (aliyekuwa rc wa manyara) na ameshafanikiwa kuwa m bunge........ akajaribu tena kum beba na mwakipesile wa mbeya but mwaki amedondokea pua.......... wengne nimewasahau......... hyo ndo system ya chama chao mambumbumbu.(CCM)
 
Uchaguzi umeisha toka nov 2010,raisi yupo na cabinet yake kashaiteua, na wabunge wapo tayari.Je kwa nini mpaka leo hajateua wakuu wa mikoa?? au ndo mpaka akapige ramli mlingotini??

Katiba inasema nini juu ya uteuzi wao?.Nao wako ndani ya appointment ya miaka 5?kama iko silent bila shaka ndo jibu.
 
Mkuu wa mkoa ana faida gani kwako? Kama una meya, mkurugenzi, katibu tawala na wengine kibao wasio na majina unakosa lipi?
 
Ameshindwa kuamini kuwa 2 + 2 = 4, kumbe wakati mwingine huweza kuwa 3 + 1 = 4, Kuna namna hapa!!!
 
Hii ina maanisha kuwa RC are useless items na source ya umaskini wetu!!
 
Uchaguzi umeisha toka nov 2010,raisi yupo na cabinet yake kashaiteua, na wabunge wapo tayari.Je kwa nini mpaka leo hajateua wakuu wa mikoa?? au ndo mpaka akapige ramli mlingotini??

Kutokana na hali halisi ya kazi yao, kwa ujumla hawana kazi yoyote wako kimaslahi ya chama zaidi, wanawakilisha chama. Ni afadhali tu ingefutwa kabisa manake wanatumia hela zetu bure tu na kuongeza bajeti ya bure,
 
Nafikiri anasubiri msahau Masahibu yaliyowapata marafiki zake walioangushwa ili akiwateua presha zenu zitakuwa zimeshashuka na mmesahu.
 
Wakuu wote wa mikoa ambao waliomba likizo ya kugombea ubunge wako kijiwenii....hadi sasa...mbega,abdul aziz na lukuvi nafasi zao hazijazibwa hata....alikuwa anasubiria ma meya wapatikane....kwanza ndio apachike hao wachumba zake ukuu wilaya na ukuu mikoa!!

Niunge mkono hoja ya mdau aliyetangulia kwa kusema, nafikiri Fadhira ndiyo inayoleta tabu. Jamani simnajua uchakachuaji ulisababisha wakurugenzi wngine wa Halmashauri kuruka ukuta na wengine kupitia madirishani kukimbia wananchi baada ya zoezi la kuchakachua? Nafikiri hilo linamuumiza kichwa JK. Pengine tuvute subira kido, natabiri kuwa pengine lolote laweza kutokea katika uteuzi huo.
 
Jamani tumvumilia bado muda kidogo tu atukabidhi nchi yetu tuamue wenyewe kwani akiwateua kwa sasa itakuwa ni gharama mara mbili
 
Uchaguzi umeisha toka nov 2010,raisi yupo na cabinet yake kashaiteua, na wabunge wapo tayari.Je kwa nini mpaka leo hajateua wakuu wa mikoa?? au ndo mpaka akapige ramli mlingotini??
Kwani kuna mkoa ambao hauna RC kwa sasa?
 
Back
Top Bottom