Nini kinachofanya JK asiteuwe RC mpaka leo??

Uchaguzi umeisha toka nov 2010,raisi yupo na cabinet yake kashaiteua, na wabunge wapo tayari.Je kwa nini mpaka leo hajateua wakuu wa mikoa?? au ndo mpaka akapige ramli mlingotini??
ANAMSUBIRI LAWRENCE mASHA ARUDI KUTOKA US ALIKOENDA KUTIBU MAJERAHA YA UCHAGUZI
 
Bado anafikiria watu kama kibonde wa clouds atawaweka wapi,ana msululu mkubwa sana wa watu wake wa karibu pamoja na ndugu na mashemeji,kwa hiyo anashindwa kuamua kwa sababu awewzi kufanya maamuzi magumu.
 
Uchaguzi umeisha toka nov 2010,raisi yupo na cabinet yake kashaiteua, na wabunge wapo tayari.Je kwa nini mpaka leo hajateua wakuu wa mikoa?? au ndo mpaka akapige ramli mlingotini??

Hivi kutoteua kwake wakuu wa mikoa, imeathiri nini utendaji wa serikali kwani shughuli hazifanyiki ? Nawe sasa kweli utajiita GREAT THINKERS ?.
 
nadhani hawa wakuu wa mikoa hawana umuhimu wowote kwa taifa bali kwa chama tawala! Kwa hiyo hata asipowachagua nchi itaendelea vizuri tu.
 
in the meantime we on "autopilot" so we will wait until the pilot gets back otherwise we will crush somewhere safe!!!
 
Halazimiki kuwa ameshachagua by this time. Na sidhani kama anabanwa na hilo. So tusishangae hilo kutotendeka kwa "wakati" mnaotaka nyie. Tumpe muda afanye kazi zake.
 
Tusitake kukuza mambo hapa! Kwanza sheria haisemi kwamba kila baada ya uchaguzi wateuliwe wengine na wala sheria haisemi ukomo wa muda wa kuteua wakuu hao. Hakuna shughuli zinazolala kwa sababu Makatibu Tawala ambao ndiyo watekelezaji wakubwa wa maamuzi na masuala yote ya utawala wapo na wanachapa mzigo kama kawaida. Isije kuwa kuna watu wana maslahi na uteuzi huo ndiyo maana wanatia shinikizo hapa JF!

mkuu kuna mchangiaji ameeleza wazi kuwa kuna mikoa mingi ipo wazi kama mikoa mipya na pia dar,kilimanjaro,iringa nk.sio suala la maslahi bali ni gap ktk shughuli za kila siku za uendeshaji wa serikali za mikoa
 
Halazimiki kuwa ameshachagua by this time. Na sidhani kama anabanwa na hilo. So tusishangae hilo kutotendeka kwa "wakati" mnaotaka nyie. Tumpe muda afanye kazi zake.

ndio maana tunahitaji katiba iliyo wazi siyo mtu kuhodhi mamlaka ya kujiamulia atakavyo kama vile anaendesha familia yake

mkuu kuna mchangiaji ameeleza wazi kuwa kuna mikoa mingi ipo wazi kama mikoa mipya na pia dar,kilimanjaro,iringa nk.sio suala la maslahi bali ni gap ktk shughuli za kila siku za uendeshaji wa serikali za mikoa

kwa nini CDM wasifnye maandamano nchi nzima kumlazimisha rais achague ma rc, au CDM watangaze wakuu wao wa mikoa kama walivyo fanya kwa meya wa arusha.
 
wanadai hazina hakuna hela, lakini huenda mwezi ujao mtasomwa mnao tarajia kutajwa
 
Mimi sielewi kazi ya maRC nini zaidi yawanachofanya Makatibu tawala wa mikoa, nadhani hivi ni vyeo vya kishkaji tu hata wakuu wa wialaya nao kazi zao sielewei kama zina maana kwani kuna makatibu tawala wa mikoa.Hivi ni vyeo vya kufuta kabisa ni kuwabebesha mzigo mkubwa wa kodi wananchi ili kuwakirimu hawa jamaa.nani mwenye ushahid wa lipi la maana wanalofanya hawa jamaa kama si makatibu tawala ndo watendaji????kw ahivo hata asipochagua itakuwa faida nadhani kwneye katiba mpya haya ni ya kuangalia kabisa.hawafai,hawatakiwi ni mzigo kwa taifa maskini kama Tanzania
 
hizi shughuli za maafa ilitakiwa awepo mwenye cheo chake azisimamie ipasavyo sasa mtu anakaimu tu anakuwa hajiamini na walio chini yake wanamdharau
 
Uchaguzi umeisha toka nov 2010,raisi yupo na cabinet yake kashaiteua, na wabunge wapo tayari.Je kwa nini mpaka leo hajateua wakuu wa mikoa?? au ndo mpaka akapige ramli mlingotini??

Mie nadhani sasa kuna haja ya kuchuja Great Thinkers na Great Tankers, kwani kutoteua kwake amevunja katiba ? au unataka tu na we watu waone kuwa umeandika kitu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom