Nini kimesababisha nchi kukosa maendeleo miaka 54 baada ya Uhuru

aliisaac1000

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
407
272
Nimekua nikijiuliza maswali mengi juu ya umaskini wetu lakini nimeshindwa kupata jibu, nimeshawishika kuleta mada hii niki linganisha na baadhi ya nchi ambazo zimepiga hatua ya kimaendeleo huku hazina raslimali kama zetu, nchi hizi karibu zote tumepata uhuru pamoja miaka ya sitini, mfano Thailand ambayo haina raslimali zozote lakini inatumia fukwe zake za bahari pekee kuvutia na kuingiza watalii. Kwa mwaka huingiza watalii milioni 32 huku kipato cha raia kwa mwaka ni $5,938.
Dubai nchi ndogo inayoongozwa na mfalme yenye idadi ya watu milioni 2.6 tu kipato cha raia kwa mwaka ni dola 24,866/=
Falme hii hutegemea utalii, na imewekeza kwenye 'real estate' na biashara za kifedha na bandari ya jebel ali ambayo ni ya 7 duniani kwa kupokea makasha. ( busiest port in the world) na huiingizia nchi kipato kikubwa.
Jamhuri ya kisoshalist ya Vietnam ambayo ilipigana vita kubwa kutokana na mgawanyiko wa kiitikadi hadi mwaka 1967 ilipoungana , Vietnam ya kusini na kaskazini. Nchi hii bado ni ya kiitikadi ya ki mrxist na leninist na ya chama kimoja. Lakini punde tu baada ya vita kuisha na kuungana ilianza mapinduzi makubwa ya kiuchumi, hadi kufikia sasa ina uchumi unaokua kwa kasi duniani wa asilimia 10 kwa mwaka huku ikiongoza duniani kwa kulima na kuuza mchele na korosho.
Nchi nyingine ni singapore ambayo ilipata uhuru wake mwaka 1963 kutoka kwa waingereza kama sisi. Hii leo baada ya miaka 52, kipato cha raia wa singapore kwa mwaka ni dola 56,319, nchi hii haina raslimali zozote na uchumu wake unategemea biashara ya bandari ambayo ni kubwa na kiungo cha biashara za shehena duniani, huku pia ikinufaika kwa kuwa na watu wenye ujuzi mkubwa kutokana na mpango kabambe wa kuelimisha raia wake.

Nimeona kwanza nitoe takwimu hizi ili muweze kuzilinganisha na Tanzania na hapo ndio sote tujiulize tumefikwa na maswshibu gani na tufanye nini ili tufike walikofika wenzetu au zaidi
Tanzania nchi tajiri na yenye raslimali nyingi za madini ya aina zote ikiwemo ardhi nzuri yenye rutuba kubwa katika ukanda huu. Ina ukanda mrefu na mzuri wa bahari kwa shughuli za kiutalii, ni nchi pekee Afrika iliyozungukwa na mito mikubwa
lakini kufikia mwaka 2016, ni asilimia 20 ya wananchi wake wanapata maji ya bomba ikilinganishwa na Nchi Ya Misri ambayo wananchi wake wafikao asilimia 98 wanapata maji ya bomba na la kushangaza maji hayo chanzo chake ni mto Nile ambao huanzia Afrika mashariki!
Tanzania ina ardhi kubwa na yenye rutuba kubwa ambayo yenyewe pekee ingeweza kutupatia fedha nyingi za kigeni kwa kilimo kikubwa cha biashara kama ilivyo kwa Vietnam. Kipato cha Mtanzania kwa mwaka ni dola 963 ambacho kwa nchi zilizo kusini mwa sahara ni cha 32 na cha chini zaidi ya kiwango cha chini kilichowekwa na UNDP cha dola 2,673.
Tuna mbuga na vivutio vya utalii kuliko nchi nyingine yoyote duniani lakini tunapokea watalii milion 1.5 kwa mwaka kuliko Thailand ambayo inaingiza watalii milioni 32 kwa mwaka kwa fukwe tuu!! za bahari na mahoteli!!, Sisi fukwe zetu hatupati chochote hata samaki.
Tunahitaji mjadala wa kitaifa tujue wapi tuliko jikwaa. Hapa sio suala la mfumo gani ni bora, ukiangalia mafanikio ya nchi nilizozitaja ambazo zimepiga hatua kubwa, zina mifumo yote ya kiutawala, kuanzia ufalme,ukomunisti (bila kusahau China) na hata utawala wa chama kimoja na vyama vingi. Ni jinamizi gani hili linalotumaliza tushidwe kusonga mbele ilhali tuna kila kitu ??
 
Africa haiwezi kuwa na maendeleo hadi tuachane na tabia za kimaskini,tungesonga mbele zaid kama tusingedai Uhuru, baada Uhuru kila kitu kitoka nje ya mstari sababu ya nature tuliumbwa tuongozwe au tusimamiwe ndo maana Africa mzima Mifumo ya maisha yafanana.Tulifanya makosa kudai Uhuru, yanathibitika maneno ya mkoloni mmoja aliwaambia wenzake waliokuwa wakipinga Uhuru kuwa waache wajitawale lkn hawatawezasonga popote,ni nadharia zenye ukweli mchungu.
 
Back
Top Bottom