Nini kimemsibu RENATUS MKINGA?

Huo ndio ukweli wenyewe!. CCM ndicho chama pekee kitakacho ulinda muungano!. Asili ya CCM ni kama asili ya Muungano, muungano wa TANU na ASP. Wale CCM wanaopinga muungano kule Zanzibar, sio CCM kweli, wale ni CCM kadi na sare tuu ila ndani yao bado ni ASP!. Wale wengine wote ambao ni CUF, wale ni ZPP, ZNP na Hizbu, wao ni wahanga wa mapinduzi, kwa vile muungano ndio umeyalinda mapinduzi daima, hawawezi kupenda aslan!.

Tuna tatizo kubwa humu jukwaani, mtu akiwa CCM, kila kitu asemacho mnakiona kama sicho!, alichosema Mkinga ndio ukweli wenyewe!. Kwa vile mpaka sasa hatujajua katiba mpya itasemaje kuhusu asilimia ya kura za Zanzibar, ili chama chochote kiweze kushinda urais wa JMT!

CCM na CUF wana uhakika wa kura za Zanzibar, Chadema haina uhakika wowote wa kura za Zanzibar, katiba mpya itatamka wazi kuwa ili chama chochote kitangazwe mshindi wa urais wa Muungano, lazima kishinde kwa theluthi moja ya kura za pande zote za muungano!

Wengine wanakalia maandamano huku siku zinakwenda!, wakiambiwa hawajipanga wanakuwa mbogo!, sasa wewe unaambiwa CCM ndicho chama pekee kinachotetea muungano, unashangaa nini?!, mkiambiwa 2015 ni CCM tena!, mapovu yanawatoka!.
P.
Huu nao ukweli CCM ndo waumini wa muungano hili huitaji kwenda shule kujua. Mkinga kavaa nguo ya CCM akimaanisha lile aliloliamini kuhusu muungano. Mkinga mtu wa misimamo na hapa anasimamia muungano ila ukimwambia richmondi. meremeta, deep green utajua huyo ni nani.
 
Huo ndio ukweli wenyewe!. CCM ndicho chama pekee kitakacho ulinda muungano!. Asili ya CCM ni kama asili ya Muungano, muungano wa TANU na ASP. Wale CCM wanaopinga muungano kule Zanzibar, sio CCM kweli, wale ni CCM kadi na sare tuu ila ndani yao bado ni ASP!. Wale wengine wote ambao ni CUF, wale ni ZPP, ZNP na Hizbu, wao ni wahanga wa mapinduzi, kwa vile muungano ndio umeyalinda mapinduzi daima, hawawezi kupenda aslan!.

Tuna tatizo kubwa humu jukwaani, mtu akiwa CCM, kila kitu asemacho mnakiona kama sicho!, alichosema Mkinga ndio ukweli wenyewe!. Kwa vile mpaka sasa hatujajua katiba mpya itasemaje kuhusu asilimia ya kura za Zanzibar, ili chama chochote kiweze kushinda urais wa JMT!

CCM na CUF wana uhakika wa kura za Zanzibar, Chadema haina uhakika wowote wa kura za Zanzibar, katiba mpya itatamka wazi kuwa ili chama chochote kitangazwe mshindi wa urais wa Muungano, lazima kishinde kwa theluthi moja ya kura za pande zote za muungano!

Wengine wanakalia maandamano huku siku zinakwenda!, wakiambiwa hawajipanga wanakuwa mbogo!, sasa wewe unaambiwa CCM ndicho chama pekee kinachotetea muungano, unashangaa nini?!, mkiambiwa 2015 ni CCM tena!, mapovu yanawatoka!.
P.

Njaa Inabadilisha Fikra hata za vijana Makini.PASCO BADO UNA HAMU NA CCM?
 
Kuna watu wanaamini katiba mpya imekuja tuu kama "manna"!. CCM ndio waliokuwa hawataki kabisa kuisikia katiba mpya!, mara all over a sudden change of heart sasa serikali ya CCM imekubali katiba mpya kwa moyo mkunjufu!

Ndio maana natumia msemo huu "I fear the Greeks, especially when they bring gifts", kipengele gani kitaingizwa kwenye katiba mpya na kipi hakitaingizwa, watatumia principle of "concensus" ya wengi wape!. Composition ya constituent assembly itasukwa kwa utaalamu wa hali ya juu kuhakikisha katiba hiyo inalinda "status quo" ya waliopo!

Kura ya maoni ni kuikubali tuu au kuikataa in its totality!, yaani itakuwa na swali moja tuu la "Jee Unaikubali Katiba Mpya?. Jibu ni "YES" or "NO". Yes zikishinda, katiba mpya imepita, no zikishinda, katiba ya zamani inaendelea!.
P.

Wewe sema mambo meeengi kadri utakavyo ila mimi nitakupima kwa jambo moja tu nalo ni kuhusu lowassa na nec, unajua ni nini ulichokisema na nini kimetokea mpaka sasa! assumptions and speculations arise from plausible basis not from absurd remarks!
 
Njaa Inabadilisha Fikra hata za vijana Makini.PASCO BADO UNA HAMU NA CCM?
Baba Matatizo, hili la kuhusu CCM sio suala la hamu!, so far ndicho chama pekee kilichopo very organized!, kinakabiliwa na matatizo makubwa ya kuhodhiwa na mafisadi, na kimeoza na kunuka rushwa from top to bottom!. Sasa hivi vyama vingine visipojipanga na kujionyesha ni vyama mbadala, amini nakuambia, 2015 ni CCM tena, pamoja na uozo wake, pamoja na mafisadi yake, tena sasa ndio mafisadi papa, watatinga rasmi Ikulu, kwa ridhaa yetu!.
P.
 
huo ndio ukweli wenyewe!. Ccm ndicho chama pekee kitakacho ulinda muungano!. Asili ya ccm ni kama asili ya muungano, muungano wa tanu na asp. Wale ccm wanaopinga muungano kule zanzibar, sio ccm kweli, wale ni ccm kadi na sare tuu ila ndani yao bado ni asp!. Wale wengine wote ambao ni cuf, wale ni zpp, znp na hizbu, wao ni wahanga wa mapinduzi, kwa vile muungano ndio umeyalinda mapinduzi daima, hawawezi kupenda aslan!.

Tuna tatizo kubwa humu jukwaani, mtu akiwa ccm, kila kitu asemacho mnakiona kama sicho!, alichosema mkinga ndio ukweli wenyewe!. Kwa vile mpaka sasa hatujajua katiba mpya itasemaje kuhusu asilimia ya kura za zanzibar, ili chama chochote kiweze kushinda urais wa jmt!

Ccm na cuf wana uhakika wa kura za zanzibar, chadema haina uhakika wowote wa kura za zanzibar, katiba mpya itatamka wazi kuwa ili chama chochote kitangazwe mshindi wa urais wa muungano, lazima kishinde kwa theluthi moja ya kura za pande zote za muungano!

Wengine wanakalia maandamano huku siku zinakwenda!, wakiambiwa hawajipanga wanakuwa mbogo!, sasa wewe unaambiwa ccm ndicho chama pekee kinachotetea muungano, unashangaa nini?!, mkiambiwa 2015 ni ccm tena!, mapovu yanawatoka!.
P.

ni kweli ccm kinalinda muungano dhidi ya raia wema wasio wezi, mafisadi wanaotaka kuufanyia mabadiliko yenye kunufaisha wengi
 
Katika hali isiyo ya kawaida mchambuzi mashuhuri wa siasa bwana RENATUS MKINGA amekuja kwenye kipindi cha marumbano ya hoja kinachoendeshwa na kituo cha TV cha ITV akiwa amevalia nguo ya CCM. Kitendo cha kuvaa nguo hiyo wakati yeye anafahamu kwa undani madhambi yaliyotendwa na chama hicho kama alivyokuwa akiainisha kipindi cha nyuma kimeniogopesha mimi binafsi. Moja kati ya dhambi kubwa ni kuunga mkono jambo fulani wakati ukijua kuwa ni jambo la hatari.

Eti anasema chama pekee kinachounga mkono muungano ni CCM wakati kwa sasa Wazanzibari wanataka kujitenga wakiwa chini ya utawala wa CCM tangu muungano. Mkinga anafikiri kuunga mkono muungano ni maneno tu, kwanini CCM hawajatatua kero za muungano wakati wao muda wote ndiyo watawala, na wana uwezo wa kufanya hivyo?.

Mkinga ambaye jamii masikini ilimuheshimu sasa anaanza kupotea, kitendo cha kuvaa nguo ya CCM ni dalili za kufa kiakiri. Shujaa ufa akisema ukweli, mkinga umeanza kupotea na ndiyo maana mwendesha mada bwana DEOGRATIUS RWEYUNGA alikuponda hapohapo kuwa jadili maswala ya kauli ya nyerere kuhusu muungano na siyo jezi ya CCM

Ulitaka aunge mkono chama gani ili moyo wako ufurahi?,pili.hivi shati alilovaa ndio kimetenda hayo unayosema,chama au baadhi ya watu walioko ndani ya chama hicho wasiokuwa na uadilifu kama ambavyo wapo katika vyama vingine?.

Jaribu kuwa na fikra pevu,halafu kajifunze kiswahili ndio uje uweke Thread humu JF.
 
Back
Top Bottom