Elections 2010 Nini kilitokea Ilemela?

Taifa_Kwanza

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
443
86
Mimi ni mzaliwa wa Mwanza, kutokana na mgawanyiko wa Majimbo ya uchaguzi, naweza kusema nimezaliwa katika Jimbo la Ilemela.

Wakati wa Kampeni za Uchaguzi habari nyingi kutoka Mwanza zilikuwa juu ya Jimbo la Nyamagana, sikusikia sana juu ya Ilemela, siku chache kabla ya uchaguzi nilipata bahati ya kukutana na rafiki yangu ambaye yeye anaishi Mwanza, tukazungumzia juu ya mchakato wa kampeni na matarajio ya matokeo.
Akaniambia Wenje anafanya kampeni nzuri, atatoa ushindani mzuri kwa Masha, lakini nilipomuuliza juu ya Ilemela, alisema Mbunge wa Kule ni Dialo, akadai Ilemela kumesinzia sana, bado hawajaamuka kabisa, nikamuuliza kwani Chadema hawajasimamisha Mgombea, akasema kuna mtu kamuambia kwamba wamesimamisha Mgombea lakini yeye hamjui hata kwa jina.

Hata mimi nilitegemea hilo, sababu hata nilipojaribu kupigapiga simu kwa ndugu jamaa na marafiki, sikuona mabadiliko yakitokea ILEMELA.

Hiyo ni TISA, Kumi ni kwamba Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ulikimbia Mwanza Kufanya utafiki wa maendeleo ya Kampeni, katika taarifa yao wakadai Dialo anamsaliti Masha Mwanza,sikumbuki kama walisema anafanya usaliti namna gani, pia hawakusema kama kumbe na Dialo kansa ya kushindwa ilikuwa ikimtafuna taratibu, Habari kuhusu Ilemela hazikusisikika kabisa.

Kauli ya kunistua niliipata siku moja kutoka kwa mama yangu mzazi, Kada wa CCM wa kuchanjiwa, Usiku wa jumamosi nilimpigia kumjulia hali, mwisho wa Maongezi nikamuuliza uchaguzi vipi, Akaniambia kesho Ilemela tutapaza sauti, nikamuuliza mtapaza vipi? akasema kura ni siri ya mtu, lakini kwa vile wewe ni Mtoto wangu nitakuambia, Kesho naipigia Kura VEMA.

Kilichobadilisha msimamo wa Mama yangu ni nini?
Hasa Kilichotokea Ilemela ni kitu gani jamani?
 
Wewe Majambazi wakimfuata mama yako! utawaeleza nini ndugu zako acha kutoa siri wewe
 
Kilichotokea Ilemela ni CDM kuchukua jimbo, ilikuwaje wakachukua sio muhimu kwa sasa!
 
Mimi si mkazi wa Mwanza ila najua kuwa watu wa Mwanza wameamka sana siku hizi; hawataki upuuzi tena. Wao walilinganisha wagombea wakagundua kuwa yule "Dr" pimbi wa CCM alikuwa anapwaya sana kuwawakilisha, hivyo wakamchagua mtu waliyeona kuwa atawawakilisha vizuri tena kwa kishindo.
 
Diallo alidhani kwa sababu Ilemela ina wasumkuma wengi wangemchagua kwa sababu ya usukuma wake. Alidhani pia kuwa vijana wengi hawatajitokeza kupiga kura hivyo kutegemea kuwa ni wale wale wazee wa siku zote ndiyo watakaopiga kura lakini mambo yakawa tofauti na matarajio yake.
Diallo anastahili heshima kwa kuwa mtu wa kwanza kukubali kushindwa na mapema kabisa alimwomba Returning Officer form ya kusaini kukubali kushindwa na kukubali matokeo. Returning Officer alipochelewesha ili apate maoni ya Chama kwanza, akamfokea kuwa aliyekuwa akishindana ni yeye na ni yeye aliyeona kuwa ameshindwa kihalali na hivyo hahitaji kupoteza muda mwingine!!!! Hii ni upande chanya sana kwa Diallo kuhusu mageuzi na mabadiliko. Tunahitaji akina Diallo wengi Africa!!!
 
Huyo Diallo aliwahi kuwatibua wananchi wa igombe ambako kunawapiga kura wengi zaidi kwa jimbo hilo.
Kuna siku alikuwa na kikao nao wakamuomba awatengenezee barabara akawaambia, 'mnataka barabara ya nini?mna magari ya kupitisha barabarani nyie?'Mara ' umeme ! umeme!, mna nyumba za kuweka umeme nyie?'
Poa wasukuma wakamsikiliza wakasema 'NAHENE'
 
Back
Top Bottom