Nini kilisababisha Prof Mwakyusa kumpuuza Baba wa Taifa?

bahati nzuri vincent nyerere hayuko ccm, na hii ilitokea tu mtu akapayuka na matokeo yake ndio haya

Hio kwa mtazamo wa kuangalia "mantik" naona tuite bahati mbaya.... Angekua yupo CCM akaongea hayo walau it would have held more water. Hata kama kweli alikua wapi siku zote? Mwalimj ana mda gani toka kafariki? Ina maana ilikua haimuumi hadi pale alipoona anaweza itumia kwa advantage ya media na kujipaisha na kuchafua papo hapo?

Alafu Raia usiniambie kua you don't know kuna viongozi wengine wana majina makubwa na wajulikana chama fulani lakini wapo hapo kama chambo....
 
Nilicho na uhakika nalo ni kwamba popote pale alipo Prof. Mwakyusa, hana raha kabisa na anasononeka ile mbaya moyoni mwake. Atakuja tu kupata amani siku atakapopata ujasiri wa kuusema ukweli na ni ukweli tu utakaomfungulia minyororo na kuwa huru. Mimi namwomba kitu kimoja tu, nacho ni kwamba ana deni kubwa sana kwa Watanzania wote na sasa ndio muda muafaka wa kusema yote. Come on, Prof., the time to do the right thing is NOW!
 
tunaanza kuwa wadaku.

Mlitaka afanyaje? Tuelezeeni kile alichokifanya na alitakiwa afanyeje!

Rafiki yangu Fair Player,

Hapa hakuna udaku, nadhani watu wanataka kupata ukweli wa hili swala na ndio maana akina Balile wamelivalia njuga, whether ni kwa manufaa ya Boss wao [mmiliki wa gazeti la Jamhuri] au ku-divert attention.

Kwenye habari za gazeti la Jamhuri, Mwalimu wa Nyerere amekiri kwamba alipinga mwanafunzi wake kupelekwa UK kutibiwa. Huyu mzee bado yuko hai.

Gachuma yuko hai na yeye alikuwa ni shahidi kwamba baada ya kusikia Mwalimu ni mgonjwa ilibidi ajitolee kumpeleka Nairobi akatibiwe na yeye amehojiwa akakubali.

Sasa hapo udaku uko wapi?

Swala la kujiuliza ni kwamba mpaka Gachuma anaamua kupendekeza Mwalimu akatibiwe Nairobi [kwa gharama za Gachuma], je Prof. Mwakyusa alikuwa wapi? Ilikuwaje mgonjwa awe anaugulia Butiama nyumbani kwake wakashindwa hata kumsogeza japo Bugando au Muhimbili, kama walikuwa wanaona ni ghali kwenda kumtibu nje?

Watu wakimtuhumu Prof. Mwakyusa kwamba alimtelekeza Mwalimu, watakuwa wanafanya makosa? Hivi kweli mgonjwa aliye serious unaweza kumwacha Butiama na ukawa uko Dar na bado ukaendelea ku-claim kwamba wewe ni Daktari unayemhudumia mgonjwa?

Nini maana ya kuitwa Daktari wa Mwalimu? Hivi leo hii JK akiugua mafua/malaria unadhani yule Daktari wake anaweza kwenda kulala nyumbani kwake akamwacha au akakaa siku 2 bila kujua JK anaendeleaje?

Hapo kwenye udaku, naomba kupingana na wewe. Tayari kuna leading clues ambazo zina point fingers kwamba kuna uzembe ulifanywa japo siwezi kujua kama ni wa makusudi au la.

Naomba nikuhakikishie kwamba hii issue ya Mwalimu haitaisha na ni mtaji wa kuelekea 2015 na atakayekuja kuitumia ni White Hair [utakuja kunikumbusha wakati ukifika maana najua uko kambi ya Lowassa].

Jamii imeaminishwa kwamba EL alikuwa na bifu na Mwalimu, na hivyo inawezekana kabisa kifo cha mwalimu kilileta faraja kwa EL. Lakini baada ya hizi tuhuma za juzi, nina uhakika EL atakuja na nguvu zote kuichimba hii issue mpaka kwenye mizizi ili kubadilisha mtazamo wa jamii kwamba kuna watu wabaya zaidi ambao walisababisha/harakisha kifo cha Mwalimu kwa uzembe au makusudi kwa manufaa yao.

Tuhuma hizi zikichimbwa vizuri sana na kuwekwa sawa, EL anaweza kuzitumia kujisafisha na kuionyesha jamii kwamba wapo watu wabaya zaidi ambao wako tayari kuharakisha vifo vya wenzao kwa manufaa yao. Kwa hiyo zile tuhuma kwamba mafisadi wa CCM wanataka kuwaua wapiganaji, zitaonekana si mali kitu ni cha mtoto ukilinganisha na watu walioharakisha kifo cha Mwalimu. Balile hawezi kukurupuka hivi hivi, lazima kuna kitu kinatengenezwa na huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya CCM na kampeni ndo zimeanza hivyo.

Hili swala litatumia kuua so ya Barua ya Mzee wangu Hamis Kassori [na nilitamani sana nisikie kauli yake kwenye hili sakata maana najua ana mengi sana]. Subiri hili swala litakapoanza kutumiwa na EL ndo utasema sio udaku, ila kwa sasa kwa kuwa bado ni mapema ndo maana unasema ni udaku!
 
Hio kwa mtazamo wa kuangalia "mantik" naona tuite bahati mbaya.... Angekua yupo CCM akaongea hayo walau it would have held more water. Hata kama kweli alikua wapi siku zote? Mwalimj ana mda gani toka kafariki? Ina maana ilikua haimuumi hadi pale alipoona anaweza itumia kwa advantage ya media na kujipaisha na kuchafua papo hapo?

Alafu Raia usiniambie kua you don't know kuna viongozi wengine wana majina makubwa na wajulikana chama fulani lakini wapo hapo kama chambo....

hili la viongozi kuwa kama chambo silipingi, ila katika hili sakata la sasa sioni suala la chambo bali kuzidiana kete na kuteleza na kumalizana kabisa
 
Hio kwa mtazamo wa kuangalia "mantik" naona tuite bahati mbaya.... Angekua yupo CCM akaongea hayo walau it would have held more water. Hata kama kweli alikua wapi siku zote? Mwalimj ana mda gani toka kafariki? Ina maana ilikua haimuumi hadi pale alipoona anaweza itumia kwa advantage ya media na kujipaisha na kuchafua papo hapo?

Alafu Raia usiniambie kua you don't know kuna viongozi wengine wana majina makubwa na wajulikana chama fulani lakini wapo hapo kama chambo....

Dada yangu AshaDii,

Vicent hakuwa na sababu yoyote ya kumfanya aongelee swala kutelekezwa kwa Mwalimu na pia tofauti zilizojitokeza kwamba asiende kutibiwa Uingereza. Linapokuja swala sensitive kama hilo wenye haki ya kuliongelea ni biological chiildren wa Mwalimu.

Kitendo cha Vicent kuchokozwa na kuambiwa anatumia jina la Mwalimu kwa maslahi ya kisiasa, ndicho kilichopelekea kuropoka hayo maneno ili kumwonyesha Mkapa kwamba Vicent ni insider wa ukoo wa Nyerere na anayajua mengi sana ya ukoo huo. Sina hakika kama alitumia hilo kama mtaji wa kisiasa, bali alikuwa akijibu mapigo kwa lengo kujitetea asije akaonekana ni tapeli na anatumia jina la Mwalimu kwa maslahi/manufaa ya kisiasa.

Mwaka 2010 kwenye Kampeni, baada ya CCM kuona Leticia Nyerere anawapelekesha puta, walikuja na kauli hii hii ya Mkapa kwamba Leticia hahusiki na ukoo wa Nyerere. Leticia aliwajibu kwamba yeye ni mtalaka wa mtoto wa Nyerere na tangu alipoolewa alibadilisha jina na hawezi kubadilisha tena baada ya kutalikiwa na mtoto wa Nyerere.

Kwa kifupi ni kwamba CCM inaona kwamba jina la Mwalimu ni deal kubwa, na kumbe ni wananchi tu ndio waliowachoka.
 
Rafiki yangu Fair Player,

Hapa hakuna udaku, nadhani watu wanataka kupata ukweli wa hili swala na ndio maana akina Balile wamelivalia njuga, whether ni kwa manufaa ya Boss wao [mmiliki wa gazeti la Jamhuri] au ku-divert attention.

Kwenye habari za gazeti la Jamhuri, Mwalimu wa Nyerere amekiri kwamba alipinga mwanafunzi wake kupelekwa UK kutibiwa. Huyu mzee bado yuko hai.

Gachuma yuko hai na yeye alikuwa ni shahidi kwamba baada ya kusikia Mwalimu ni mgonjwa ilibidi ajitolee kumpeleka Nairobi akatibiwe na yeye amehojiwa akakubali.

Sasa hapo udaku uko wapi?

Swala la kujiuliza ni kwamba mpaka Gachuma anaamua kupendekeza Mwalimu akatibiwe Nairobi [kwa gharama za Gachuma], je Prof. Mwakyusa alikuwa wapi? Ilikuwaje mgonjwa awe anaugulia Butiama nyumbani kwake wakashindwa hata kumsogeza japo Bugando au Muhimbili, kama walikuwa wanaona ni ghali kwenda kumtibu nje?

Watu wakimtuhumu Prof. Mwakyusa kwamba alimtelekeza Mwalimu, watakuwa wanafanya makosa? Hivi kweli mgonjwa aliye serious unaweza kumwacha Butiama na ukawa uko Dar na bado ukaendelea ku-claim kwamba wewe ni Daktari unayemhudumia mgonjwa?

Nini maana ya kuitwa Daktari wa Mwalimu? Hivi leo hii JK akiugua mafua/malaria unadhani yule Daktari wake anaweza kwenda kulala nyumbani kwake akamwacha au akakaa siku 2 bila kujua JK anaendeleaje?

Hapo kwenye udaku, naomba kupingana na wewe. Tayari kuna leading clues ambazo zina point fingers kwamba kuna uzembe ulifanywa japo siwezi kujua kama ni wa makusudi au la.

Naomba nikuhakikishie kwamba hii issue ya Mwalimu haitaisha na ni mtaji wa kuelekea 2015 na atakayekuja kuitumia ni White Hair [utakuja kunikumbusha wakati ukifika maana najua uko kambi ya Lowassa].

Jamii imeaminishwa kwamba EL alikuwa na bifu na Mwalimu, na hivyo inawezekana kabisa kifo cha mwalimu kilileta faraja kwa EL. Lakini baada ya hizi tuhuma za juzi, nina uhakika EL atakuja na nguvu zote kuichimba hii issue mpaka kwenye mizizi ili kubadilisha mtazamo wa jamii kwamba kuna watu wabaya zaidi ambao walisababisha/harakisha kifo cha Mwalimu kwa uzembe au makusudi kwa manufaa yao.

Tuhuma hizi zikichimbwa vizuri sana na kuwekwa sawa, EL anaweza kuzitumia kujisafisha na kuionyesha jamii kwamba wapo watu wabaya zaidi ambao wako tayari kuharakisha vifo vya wenzao kwa manufaa yao. Kwa hiyo zile tuhuma kwamba mafisadi wa CCM wanataka kuwaua wapiganaji, zitaonekana si mali kitu ni cha mtoto ukilinganisha na watu walioharakisha kifo cha Mwalimu. Balile hawezi kukurupuka hivi hivi, lazima kuna kitu kinatengenezwa na huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya CCM na kampeni ndo zimeanza hivyo.

Hili swala litatumia kuua so ya Barua ya Mzee wangu Hamis Kassori [na nilitamani sana nisikie kauli yake kwenye hili sakata maana najua ana mengi sana]. Subiri hili swala litakapoanza kutumiwa na EL ndo utasema sio udaku, ila kwa sasa kwa kuwa bado ni mapema ndo maana unasema ni udaku!
Keil,
Hapo hapo tutamkumbusha Lowassa kwamba yeye alichinja ng'ombe kusherehekea kifo cha Mwalimu. Hatujasahau na hatutasahau!
P.S. Mwambie Fairplayer kwamba tunajua.
 
Posti nyingine ni za kipuuzi.
Mtoa mada hebu tupe historia ya matibabu ya Mwalimu kabla na BAADA ya kustaafu, na kama Prof Mwakyusa naye alihamia kabisa Butiama kwa kazi hiyo.
Mwalimu Kama binadamu mwingine alikufa kwa ugonjwa ambao hata mabingwa huko Uingeteza walishindwa kuudhibiti.

Walikwambia kuwa walishindwa? Au waliandaliwa washindwe?
 
Dada yangu AshaDii,

Vicent hakuwa na sababu yoyote ya kumfanya aongelee swala kutelekezwa kwa Mwalimu na pia tofauti zilizojitokeza kwamba asiende kutibiwa Uingereza. Linapokuja swala sensitive kama hilo wenye haki ya kuliongelea ni biological chiildren wa Mwalimu.

Kitendo cha Vicent kuchokozwa na kuambiwa anatumia jina la Mwalimu kwa maslahi ya kisiasa, ndicho kilichopelekea kuropoka hayo maneno ili kumwonyesha Mkapa kwamba Vicent ni insider wa ukoo wa Nyerere na anayajua mengi sana ya ukoo huo. Sina hakika kama alitumia hilo kama mtaji wa kisiasa, bali alikuwa akijibu mapigo kwa lengo kujitetea asije akaonekana ni tapeli na anatumia jina la Mwalimu kwa maslahi/manufaa ya kisiasa.

Mwaka 2010 kwenye Kampeni, baada ya CCM kuona Leticia Nyerere anawapelekesha puta, walikuja na kauli hii hii ya Mkapa kwamba Leticia hahusiki na ukoo wa Nyerere. Leticia aliwajibu kwamba yeye ni mtalaka wa mtoto wa Nyerere na tangu alipoolewa alibadilisha jina na hawezi kubadilisha tena baada ya kutalikiwa na mtoto wa Nyerere.

Kwa kifupi ni kwamba CCM inaona kwamba jina la Mwalimu ni deal kubwa, na kumbe ni wananchi tu ndio waliowachoka.

Maneno aloongea Vicent ni makali na mazito mno... Very very unsettling, Siasa ni mchezo mchfu hio ni wazi, na kwa mwanasiasa kuweza hasa himili vishindo vya walo mzunguka ni lazima nae achafue mikono yake ama hali ya hewa. Nakubaliana na maneno na maelezo yako ambayo yanaeleweka na yako clear.... Hata hivo naona tu kama hio ni "Gutter politics" na Vincent knew what he was doing. Ok unasema kua he was mad at Kipara kwamba anatumia jina la Nyerere... Kwa muktadha huu na flow of events inaonesha kua Mkapa was right after all... Umeona the way imemuongeze popularity? The way sasa jina lake twataja mara kwa mara?

Bahati mbaya ama nzuri atapata wafuasi wengi sana basing on the issue at hand... Just because katoa habari ambazo zinakua assumed kua ni kweli na kana kwamba kusema hayo maneno yanam qualify yeye kushika position. For believe me you ndio kigezo kikuu kitatumika ila sio anaweza fanya nini! Angetaka kumkomoa BM Angefukua ya BM mbona mengi tu ambayo wengine hawana guts ya kuyafufua? Hivo tayari hata mimi nakubali na kuunga mkono anatumia jina la Mwalim...

BTW Huyo Leticia kama ni mtalaka wa Mtoto wa malimu na akaamua kuingia katika politics... Lazima alichukulia hio advantage bana. Jina holds a lot of water... hio ni kitu ambayo haikwepeki hata katika maisha ya kawaida ya katika jamii... Angekua kweli hana nia ya kutumia ukaribu ama kuonesha uhusiano na anajiamini angekubali tu kua YES sina mahusiano (for at the end of the day ni kweli hayupo kwenye hio familia)
 
Keil,
Hapo hapo tutamkumbusha Lowassa kwamba yeye alichinja ng'ombe kusherehekea kifo cha Mwalimu. Hatujasahau na hatutasahau!

Ha ha ha ha ha ha ... nilikuwa najaribu kulinganisha thamani ya champagne na ng'ombe ili nione nani alifanya sherehe kubwa!

Ila hapo kwenye ng'ombe lazima kuwe na kishushio ambacho ni beer/wine/champagne ambayo inamaanisha kwamba kwenye kuchinja ng'ombe ndo sherehe ilikuwa kubwa sana!

Ngoja tuone akina Balile wanaelekea wapi na wataishia wapi.
 
Maneno aloongea Vicent ni makali na mazito mno... Very very unsettling, Siasa ni mchezo mchfu hio ni wazi, na kwa mwanasiasa kuweza hasa himili vishindo vya walo mzunguka ni lazima nae achafue mikono yake ama hali ya hewa. Nakubaliana na maneno na maelezo yako ambayo yanaeleweka na yako clear.... Hata hivo naona tu kama hio ni "Gutter politics" na Vincent knew what he was doing. Ok unasema kua he was mad at Kipara kwamba anatumia jina la Nyerere... Kwa muktadha huu na flow of events inaonesha kua Mkapa was right after all... Umeona the way imemuongeze popularity? The way sasa jina lake twataja mara kwa mara?

Bahati mbaya ama nzuri atapata wafuasi wengi sana basing on the issue at hand... Just because katoa habari ambazo zinakua assumed kua ni kweli na kana kwamba kusema hayo maneno yanam qualify yeye kushika position. For believe me you ndio kigezo kikuu kitatumika ila sio anaweza fanya nini! Angetaka kumkomoa BM Angefukua ya BM mbona mengi tu ambayo wengine hawana guts ya kuyafufua? Hivo tayari hata mimi nakubali na kuunga mkono anatumia jina la Mwalim...

BTW Huyo Leticia kama ni mtalaka wa Mtoto wa malimu na akaamua kuingia katika politics... Lazima alichukulia hio advantage bana. Jina holds a lot of water... hio ni kitu ambayo haikwepeki hata katika maisha ya kawaida ya katika jamii... Angekua kweli hana nia ya kutumia ukaribu ama kuonesha uhusiano na anajiamini angekubali tu kua YES sina mahusiano (for at the end of the day ni kweli hayupo kwenye hio familia)

Asha Dii pamoja na mengine naona unahama toka kwenye mada. Mada sasa inamuhusu zaidi prof mwakyusa na kilichomfanya kumtelekeza Mwalimu. Lakini katika kukujibu tu ni kuwa, si kweli kwamba vincent anatumia jina la Nyerere kimaarufu. Unajua maana ya ukoo? Au kwenu hakuna family tree? Nasi tutaamini sasa kuwa unatumiwa kupotosha mada kama unaamini katika mapandikizi
 
Sorry Raia... Ila ukifuatilia vizuri utakuta ni discussion ilo fika huko baada ya kujaribu eleweshana. Umeona Keil alivo nijibu... Hio post uloni quote nimejibu exactly mambo ambayo amegusia. Hata hivo usijali.... I believe the message has been delivered.
 
Keil,
Hapo hapo tutamkumbusha Lowassa kwamba yeye alichinja ng'ombe kusherehekea kifo cha Mwalimu. Hatujasahau na hatutasahau!
P.S. Mwambie Fairplayer kwamba tunajua.

Ha ha ha ha ha ha ... Jasusi unanivunja mbavu hapo kwenye bold, ningekuongezea LIKE ya pili ila haiwezekani.

FairPlayer atapita kusoma huu uzi muda si mrefu, maana yeye ndo rubani wa EL Airline Flight No. 2015, Destination - Magogoni. Msaidizi wake ni Pasco wa JF. Lazima wasome huu uzi ili ndege isije ikatunguliwa na maadui au ikakumbana na hali mbaya ya hewa na hivyo safari ya kuelekea Magogoni ikaishia Monduli.
 
Wakuu hivi kwanini Prof Mwakyusa ambaye nimesikia kuwa ni daktari wa watoto,aliteuliwa kuwa daktari wa Mwalimu(mtu mzima)?
 
Sorry Raia... Ila ukifuatilia vizuri utakuta ni discussion ilo fika huko baada ya kujaribu eleweshana. Umeona Keil alivo nijibu... Hio post uloni quote nimejibu exactly mambo ambayo amegusia. Hata hivo usijali.... I believe the message has been delivered.

turudi kwenye mada ya Mwakyusa basi. Unadhani ni kwa nini hakutimiza wajibu wake kama dakrari wa Mwalimu?
 
Stop fighting the Lost Battle. Hii teleNovela haina tija kwa Watanzania. He is Dead, let us say Bwana alitoa, na Bwana alitwaa jina lake Litukuzwe.
 
...naomba tamthiliya hii itavyoisha ifuate ya...

.."NYERERE ALIVYOMUUA SOKOINE"...
Wataalamu wa data wapo....watujuze.
 
Sikubaliani na wala siamini maneno yanayotolewa kwamba Profesor Mwakyusa alimpuuza Mwalimu Nyerere wakati wa ugonjwa wake uliopelekea kifo. Tutambue kama daktari bingwa Mwakyusa hakutarajiwa kumfanyia "Nursing" mgonjwa wake kwa kukaa naye masaa 24. Pia Mwakyusa Kama daktari bingwa aliendelea kumfanyia uchunguzi wa vipindi (periodic check ups) bila kuhitajika kuhamia Butiama na kuyaacha majukumu yake mengine na wagonjwa wake ( Uzi huu unataka kutuaminiisha kuwa hicho ndicho alichotakiwa kufanya). Kwakua Mwalimu alikua anaishi Butiama ni dhahiri alikua anaonwa na daktari aliye karibu Kama huyo daktari anaye tajwa.
Wakuu tuache kuchokonoa mambo ambayo hakika hatuna uthibitisho nayo na wala hatuna nia na wala uwezo wa kupata ukweli. Tunajivunjia hadhi kudakia mambo ya hisia za WATU ambao baadhi Yao afya ya akili zao inautata.(questionable mental health).jamii yetu inajiongezea ujinga kutokana na uvivu wa kuzisaka na kupata taarifa sahihi mfano kuna WATU wanaamini kwamba babu Seya alisingiziwa wakati wangeweza kwenda mahakama ya kisutu kupata mwenendo wa kesi na kusoma ushahidi wa watoto tisa wenye umri kati ya miaka 8 na 12 halafu ndio waseme amesingiziwa au la.
 
Back
Top Bottom